Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,833
- 27,747
maisha kama hayo niliwahi kuishi. ni yale maisha unaenda bucha kununua nusu kilo ya nyama au utumbo, unakaa foleni, mbele yako jamaa anapimiwa kilo 10 za nyama na kilo 2 za maini, na kilo 5 za samaki. anaenda kuviweka kwenye jokofu ale polepole. akimaliza kupimiwa, inakuwa ngumu sana kumwambia muuza bucha kwamba unaomba nusu ya nyama au utumbo, na pengine nyuma yako kuna mteja wake anayefahamu akifika huwa ananunua kilo kuanzia 5 za nyama. hivyo wewe wa nusu kilo uwasubirishe hao. nilikuwa najifanya sina haraka namwambia wapimie tuhao, naendelea kupiga story hadi wapungue. sasaivi sasa, nawaona watu wanavizia pia kununua nusu kilo wakati mimi nanunua kilo za kutosha tu. huyu Mungu mwacheni aitwe Mungu, anao uwezo kubadilisha kabisa maisha ya mtu.Kisa cha kwanza…
Nafika bucha na kuagiza kilo mbili za nyama kawaida. Kwa kuwa najua bei, natoa chenji kamili na kumkabidhi muuza bucha.
Anahesabu na kuniuliza mbona hela haitoshi? Napigwaa butwaa na kumuuliza kwani kulikoni? Ananijibu bei imepanda.
Naanza kulalama na ghafla nyuma yangu nasikia sauti, “Ee bwana kama huna hela tupishe, unatuchelewesha!
Sijakaa sawa sauti ya kike nayo ikadakia, “Wengine bwana, wapuuzi kweli kweli! Mtu huna hela kwani lazima ule nyama?
Taratibu nageuka na kukuta mstari nyuma yangu. Wote wamefura wakinitazama kama vile natoka sayari ya mbali.
Hakuna sura hata moja iliyoonekana kuniunga mkono au hata kushangaa kwa nini bei imepanda karibu mara mbili!
Mungu humwinua mnyonge toka mavumbini, na mhitaji toka jaani (jalalani), na kumketisha pamoja na wakui. yeye humwinua amtakaye, na humshusha amtakaye. wenye kiburi hushushwa na Bwana, bali wanyenyekevu huwapa fadhila.