Online relationships don't run faster than your legs !

Daima naamini hamna watu wanaokutana kwenye hizi sosho nertworking wakafikishana mbali

Kwanza naona ni vigumu kumantain kule kuheshimiana kati yenu kutokana na mazingira mliyokutana

Love doesnt ask why..hatukatai ila sio mbaya kujiuliza swali la kizembe kama hili; mtaani,kazini,chuoni na jamii zoooote zinamzunguka hakuona wa kumfaa mpaka alipokuona wewe kwenye blog!!!!!

Sanasana either she ataliwa MWILI au he aliwe MALI

Correct me with concrete evidence if am wrong.

Concrete evidence ni nini kwa tafsiri yako!!!???
 
well said Himidini usemayo ni ukweli 100% inabidi kuwa makini sana, thanks kwa ushauri
 
Last edited by a moderator:
Mapinduzi makubwa ya teknolojia yamerahisisha mambo mengi sana. Moja ya taasisi inayopokea chungu na tamu ya kupanuka kwa mawasiliano ni ndoa. Mahusiano ya kimapenzi kupitia mitandao yanakua kasi, yanakutanisha marafiki, ndugu, waliopoteana na kuibua mahusiano mapya, ambayo kweli yamesaidia kutibu mioyo iliyopondeka.

Lakini hakuna sarafu yenye upande mmoja, pamoja na mitandao kuleta furaha, amani, maelewano n.k pia imeleta kutoaminiana, kupotezeana wakati na mengineyo!

Kutafuta mwenza katika mitandao sio jambo baya, ni jema kabisa, lililo rahisi na linalotuweka karibu.
Yapo ambayo ukiwa mtu makini unapaswa kuyazingatia, machache kati ya hayo ni yafuatayo:

I: JIHADHARI NA WAONGO
Kuna watu walio mitandaoni hawaoni tabu kuanzisha uhusiano na wewe ili tu kukujaribu, kukutumia kama jojo kisha kukuacha, wanaweza kutumia mwavuli wa dini ili kuleta mvuto wa wewe uwakubali na kweli ukaingia. Mitandao imejaa wasanii wa mapenzi. Wanadanganya kuanzia umri, ukweli kuhusu watoto, kazi zao n.k.
Claudia mwana dada wa kimarekani mwaka 2010 ameshuhudia namna ambavyo alikutana na mwanaume twitter na siku tatu kabla ya harusi, alikuta ujumbe ktk email ya mume mtarajiwa kutoka kwa mkewe na watoto wake wakimuuliza lini atarudi nyumbani..
UTAMJUAJE MUONGO
Jipe muda

II: JIHADHARI NA MARITAL STATUS
Ukitembea profile yake iwe facebook, twitter,n.k utakuta kajieleza kuwa yuko single, au recent out of relationship n.k
Wapo ambao kweli wanasema wakimaanisha lakini wengi wao bado wapo ktk mahusiano ila wamekosa uvumilivu wa matatizo madogo madogo ktk mahusiano yao, na hivyo wanatafuta mahali pa kuweka kambi.

III JIHADHARI NA PICHA UNAZOPOKEA
Sehemu kubwa ya picha ktk mitandao ya kijamii ni ile yenye mivuto, inayoita, inayoshawishi..ni picha zenye kuteka macho yako. Zimesafishwa vema na kompyuta kiasi cha kukufikirisha kuwa kuna malaika wamekuja kufanya tour duniani. Mf Joan ni mwanadada wa Afrika kusini, katika mkasa uliowahi kumpata ni kupokea picha za mwanaume handsome,iliyomtega, kumvuta na kujitoa tayari kwa lolote. Siku walipoonana alishangaa sana, sura ilikuwa ile aliyotumiwa hata hivyo udadisi wake ulibaini baadae kuwa zilikuwa za miaka mitano iliyopita, tayari mengi yalishapita ktk nyuso zake

IV JIHADHARI ZA BLOGI ZA WALIO SINGO
Bila shaka umekutana na blog ambazo ni maalum kwa wale walio single? Kama bado subiri, moja ya changamoto ktk blog hizi ni kuwa, kuna watu wamegeuza suala la kutafuta wachumba kama sehemu ya kipato. Maisha magumu bwana! Waishije mjini?? Hawa wanajua ku-fake maisha, maneno matamu, na wapo tayari kukulainisha ili tu uache pesa ya matumizi. Wanataka u-sign up, ukiingia huko basi watakugeuza nyumba ndogo.

V: JIHADHARI NA MASHUSHUSHU
Ktk hili, zipo taasisi au kikundi fulani ambacho ---------- tu kujua taarifa zako, kazi yako, we ni nani, unaishije n.k Hawa ni mabingwa wa ku-hack mawasiliano yako. Kama wewe ni mwanaume, wanapenda kutumia mbinu ya yule jasusi wa kijerumani aliyevumbua mbinu maarufu ya romance ktk upelelezi. Watatumia wanawake kukunasa! Ama sivyo watajitahidi kujua weak point yako lakini ukweli hawapo kwako kwa ajili ya mahusiano ya kujenga familia au ndoa na wewe!

MWISHO, Sio wote wana nia mbaya bali wachache tu wanawaharibia. La msingi jitahidi kutokuwa mwepesi wa kuamini, kujitoa maana ndoa inahitaji muda wala si mashindano.
Online relationships, don't run faster than your legs !!
(Joshua Fruhlinger is hereby acknowledged)
Dah umeumbua wengi!
Kuna thread moja nilisoma jamaa kaandika "Mke anahitajika haraka sana" akaweka hadi tarehe kamili ya ndoa...Leo kaja na nyingine ameandika "Kama mke nimekosa basi nahitaji mwanamke yeyote yule"
 
Well spoken Himidini....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
wadada ndio tupo at risk sana kwa hawa wanaume wa mtandaoni wanaojifanya wanataka kutuoa! mtu anakutangazia ndoa hata kwa sura hakujui si majanga haya?

Ushajipendelea hapo, siku wadada ndo noma na kibaya zaidi wao siku zote wanaaminika na hivyo ni rahisi kumpata mwanamme na kumtumia apendavyo.

Si unaona wale wanaijeria huwa wanatumia picha na majina ya wadada
 
Daima naamini hamna watu wanaokutana kwenye hizi sosho nertworking wakafikishana mbali

Kwanza naona ni vigumu kumantain kule kuheshimiana kati yenu kutokana na mazingira mliyokutana

Love doesnt ask why..hatukatai ila sio mbaya kujiuliza swali la kizembe kama hili; mtaani,kazini,chuoni na jamii zoooote zinamzunguka hakuona wa kumfaa mpaka alipokuona wewe kwenye blog!!!!!

Sanasana either she ataliwa MWILI au he aliwe MALI

Correct me with concrete evidence if am wrong.

Hapo naona unakatisha tamaa wote wanaojaribu bahati zao humu.

Mimi naamini hata humu mnaweza kukutana na mkafikishana mbali tu kama wote mna malengo chanya na mnaambizana ukweli. Na mtu kama una heshima utamheshimu tu haijalishi mmekutana wapi.

Cha msingi na sekondari kabisa, ni kuwa na muda wa kutosha kumfahamu huyo mtu
 
Shukraan rafiki...Ni kweli usemayo watu wa mtandaoni si wakuaminika...Kila mtu yupo kimaslahi yake....

"Tulipo endelea, tuliwaona maelfu ya watu kwenye
mateso,Wakati roho inapo mwona Bwana,
zilijitahidi kumfikia kwa mikono isiyo na
ngozi.Nilimwona mwanamke aliye anza kupiga
makelele alipo mwona Bwana Yesu. Alilia, "Bwana
tafadhali nirehemu! nitoe mahali hapa!" Alikuwa
akiteseka sana na aliunyoosha mkono wake kwa
Bwana.Aliendelea kumwomba Bwana amtoe eneo
lile hata kwa sekundr moja.
Alikuwa yuu uchi kabisa na alifunikwa na tope.
Nywele zake zilikuwa ni chafu na minyoo ilikuwa
ikijongea mwilini mwake .Alijaribu kuiondoakwa
mikono yake lakini kila alipo mwondoa mmoja
mingine ilijizisha zaidi.Minyoo ilikuwa na urefu
karibu inchi 6-8.Neno la Bwana linasema katika
Marko 9:44, "Ambamo humo funza wao hafi, wala
moto hauzimiki."
Ilikuwa ni ya kutisha sana kumwona mwanamke
huyu na kusikia kilio chake kwa jinsi minyoo ile
kwa hasira ilivyo kuwa inaila nyama za mama
huyu. Kulikuwepo na bango la chuma lililo kifuani
mwake ambalo lisingeweza kuharibiwa na moto.
Lilisomeka , "Nipo hapa kwa ajili ya Uzinzi." Kwa
jinsi ile ile ya dhambi yake, mwanamke huyu
alilazimishwa kufanya uzinzi kuzimu na nyoka wa
kutisha mnene..Nyoka huyu alikuwa na miiba
mikubwa kuuzunguka mwili wake, ni kama ya
uerfu wa inchi 6-8 hivi.Nyoka humwingia mama
hyu sehemu zake za siri na kusafiri hadi mwilini
mwale hadi kwenye koromeo lake. Nyoka alipo
mwingilia hivi, alianza kulia kwa makelele .
Alimwomba Bwana kwa nguvu sana amtoe eneo
lile, "Bwana, nipo hapa kwa ajili ya uzinzi,
nimekuwepo hapa kwa miaka 7, tangu UKIMWI
ulipo niua. Nilikuwa na wapenzi sita6, na nipo
hapa kwa ajili ya uzinzi." Kule kuzimu alitakiwa
kuirudia dhambi yake tena na tena.
Hakuna kupumzika usiku na mchana, akiteseka
kwa jinsi ile ile kila mara. Alijaribu kuunyoosha
mkono wake kwa Bwana, lakini Bwana
alimwambi, "Blanca, kwako tayari umechelewa.
Minyoo itakuwa ni kitanda chako, na minyoo
itakufunika." (Isaya 14:11) Wakati Bwana alipo
sema maneno hayo, blanketi la moto lilimfunika,
na siku mwona tena."
TUACHE ZINAA TUFUNGE NDOA NI UJUMBE KWA
VALENTINE DAY
 
^^
Hakika, umakini unatakiwa sana, ukimwona Mapi mwambie apite hapa tusikie maoni yake na watu8
^^

Sijawahi kuamini katika mahusiano ya mtandaoni, na wala sitaweza kuyaamini.

Sipendi vya kunyongewa napenda vile ninavyowinda, kuvikamata na kuvitafuna mwenyewe.

Kwa nini kujificha nyuma ya screen wakati uwanja wa mapambano upo wapi???
 
Umeona thatha Himidini unavyokremisha?
Hawa viumbe ni wa kwanza kulalamikia mapenzi, bila kutambua na wao ni viruka njia!

asante sana na mimi nawatumia kama jojo
Khaa! Mpaka mimi jamani unanitumia hivyo? Thkupendi tena! Tena uthimdipu tena!

Soooo true,ya sosho netiweki yaishie sosho netwekini...
Yamekua hayo? Thkudoei tena!

Shukraan rafiki...Ni kweli usemayo watu wa mtandaoni si wakuaminika...Kila mtu yupo kimaslahi yake....
Khaa! Ubora wote wa mapenzi ya mitandaoni haukuuona? Utadhani hao waliokusaliti wote uliwapata mtandaoni! lol!

wadada ndio tupo at risk sana kwa hawa wanaume wa mtandaoni wanaojifanya wanataka kutuoa! mtu anakutangazia ndoa hata kwa sura hakujui si majanga haya?
Thi majnga beiby! Coz mimi nipo kwa ajili yako, afu mimi ni miongoni mwa hao wachache tuthioumidha!

Daima naamini hamna watu wanaokutana kwenye hizi sosho nertworking wakafikishana mbali

Kwanza naona ni vigumu kumantain kule kuheshimiana kati yenu kutokana na mazingira mliyokutana

Love doesnt ask why..hatukatai ila sio mbaya kujiuliza swali la kizembe kama hili; mtaani,kazini,chuoni na jamii zoooote zinamzunguka hakuona wa kumfaa mpaka alipokuona wewe kwenye blog!!!!!

Sanasana either she ataliwa MWILI au he aliwe MALI

Correct me with concrete evidence if am wrong.

Thi unaona hapo? Hata hayo mapenzi nje na mitandao ya kijamii Rule yako inapply mutatis mudandis!
 
Mapinduzi makubwa ya teknolojia yamerahisisha mambo mengi sana. Moja ya taasisi inayopokea chungu na tamu ya kupanuka kwa mawasiliano ni ndoa. Mahusiano ya kimapenzi kupitia mitandao yanakua kasi, yanakutanisha marafiki, ndugu, waliopoteana na kuibua mahusiano mapya, ambayo kweli yamesaidia kutibu mioyo iliyopondeka.

Lakini hakuna sarafu yenye upande mmoja, pamoja na mitandao kuleta furaha, amani, maelewano n.k pia imeleta kutoaminiana, kupotezeana wakati na mengineyo!

Kutafuta mwenza katika mitandao sio jambo baya, ni jema kabisa, lililo rahisi na linalotuweka karibu.
Yapo ambayo ukiwa mtu makini unapaswa kuyazingatia, machache kati ya hayo ni yafuatayo:

I: JIHADHARI NA WAONGO
Kuna watu walio mitandaoni hawaoni tabu kuanzisha uhusiano na wewe ili tu kukujaribu, kukutumia kama jojo kisha kukuacha, wanaweza kutumia mwavuli wa dini ili kuleta mvuto wa wewe uwakubali na kweli ukaingia. Mitandao imejaa wasanii wa mapenzi. Wanadanganya kuanzia umri, ukweli kuhusu watoto, kazi zao n.k.
Claudia mwana dada wa kimarekani mwaka 2010 ameshuhudia namna ambavyo alikutana na mwanaume twitter na siku tatu kabla ya harusi, alikuta ujumbe ktk email ya mume mtarajiwa kutoka kwa mkewe na watoto wake wakimuuliza lini atarudi nyumbani..
UTAMJUAJE MUONGO
Jipe muda

II: JIHADHARI NA MARITAL STATUS
Ukitembea profile yake iwe facebook, twitter,n.k utakuta kajieleza kuwa yuko single, au recent out of relationship n.k
Wapo ambao kweli wanasema wakimaanisha lakini wengi wao bado wapo ktk mahusiano ila wamekosa uvumilivu wa matatizo madogo madogo ktk mahusiano yao, na hivyo wanatafuta mahali pa kuweka kambi.

III JIHADHARI NA PICHA UNAZOPOKEA
Sehemu kubwa ya picha ktk mitandao ya kijamii ni ile yenye mivuto, inayoita, inayoshawishi..ni picha zenye kuteka macho yako. Zimesafishwa vema na kompyuta kiasi cha kukufikirisha kuwa kuna malaika wamekuja kufanya tour duniani. Mf Joan ni mwanadada wa Afrika kusini, katika mkasa uliowahi kumpata ni kupokea picha za mwanaume handsome,iliyomtega, kumvuta na kujitoa tayari kwa lolote. Siku walipoonana alishangaa sana, sura ilikuwa ile aliyotumiwa hata hivyo udadisi wake ulibaini baadae kuwa zilikuwa za miaka mitano iliyopita, tayari mengi yalishapita ktk nyuso zake

IV JIHADHARI ZA BLOGI ZA WALIO SINGO
Bila shaka umekutana na blog ambazo ni maalum kwa wale walio single? Kama bado subiri, moja ya changamoto ktk blog hizi ni kuwa, kuna watu wamegeuza suala la kutafuta wachumba kama sehemu ya kipato. Maisha magumu bwana! Waishije mjini?? Hawa wanajua ku-fake maisha, maneno matamu, na wapo tayari kukulainisha ili tu uache pesa ya matumizi. Wanataka u-sign up, ukiingia huko basi watakugeuza nyumba ndogo.

V: JIHADHARI NA MASHUSHUSHU
Ktk hili, zipo taasisi au kikundi fulani ambacho ---------- tu kujua taarifa zako, kazi yako, we ni nani, unaishije n.k Hawa ni mabingwa wa ku-hack mawasiliano yako. Kama wewe ni mwanaume, wanapenda kutumia mbinu ya yule jasusi wa kijerumani aliyevumbua mbinu maarufu ya romance ktk upelelezi. Watatumia wanawake kukunasa! Ama sivyo watajitahidi kujua weak point yako lakini ukweli hawapo kwako kwa ajili ya mahusiano ya kujenga familia au ndoa na wewe!

MWISHO, Sio wote wana nia mbaya bali wachache tu wanawaharibia. La msingi jitahidi kutokuwa mwepesi wa kuamini, kujitoa maana ndoa inahitaji muda wala si mashindano.
Online relationships, don't run faster than your legs !!
(Joshua Fruhlinger is hereby acknowledged)
Well, kwa mtzamo wangu ni 50~50%... wapo wakweli na wapo wadandiaji....
No generalizashen.
 
Nilipomuomba Mungu,nilimuomba anipe mume na sio boyfriend,na sikumlimit jinsi ya kumpata huyo mume.as i told him"unanijua kuliko ninavyojijua,utanipatia kilicho chema".
Akatokea huyu mwanaume through social network,he told me he loved me and wants to marry me,i was like this cant be and i refuse his propasal....as time goes by kuna kitu ndani yangu kikaniambia he is the one dont let him go.....well some people thought i was crazy kukubali kuolewa with the man i met on social network.bt nikasema if its a mistake will be my mistake not urs...well i wouldnt ask for anything......he is a blessing,he is my man,my friend,my baby's father.As every single day goes by..I THANK GOD THAT I FIND HIM.he is my life.
 
Umeona thatha Himidini unavyokremisha?
Hawa viumbe ni wa kwanza kulalamikia mapenzi, bila kutambua na wao ni viruka njia!

Khaa! Mpaka mimi jamani unanitumia hivyo? Thkupendi tena! Tena uthimdipu tena!

Yamekua hayo? Thkudoei tena!

Khaa! Ubora wote wa mapenzi ya mitandaoni haukuuona? Utadhani hao waliokusaliti wote uliwapata mtandaoni! lol!

Thi majnga beiby! Coz mimi nipo kwa ajili yako, afu mimi ni miongoni mwa hao wachache tuthioumidha!

Thi unaona hapo? Hata hayo mapenzi nje na mitandao ya kijamii Rule yako inapply mutatis mudandis!
Tuheshimiane Mashaxizo!!nani kiruka njia?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom