Online relationships don't run faster than your legs !

Online relationships don't run faster than your legs !

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,190
Mapinduzi makubwa ya teknolojia yamerahisisha mambo mengi sana. Moja ya taasisi inayopokea chungu na tamu ya kupanuka kwa mawasiliano ni ndoa. Mahusiano ya kimapenzi kupitia mitandao yanakua kasi, yanakutanisha marafiki, ndugu, waliopoteana na kuibua mahusiano mapya, ambayo kweli yamesaidia kutibu mioyo iliyopondeka.

Lakini hakuna sarafu yenye upande mmoja, pamoja na mitandao kuleta furaha, amani, maelewano n.k pia imeleta kutoaminiana, kupotezeana wakati na mengineyo!

Kutafuta mwenza katika mitandao sio jambo baya, ni jema kabisa, lililo rahisi na linalotuweka karibu.
Yapo ambayo ukiwa mtu makini unapaswa kuyazingatia, machache kati ya hayo ni yafuatayo:

I: JIHADHARI NA WAONGO
Kuna watu walio mitandaoni hawaoni tabu kuanzisha uhusiano na wewe ili tu kukujaribu, kukutumia kama jojo kisha kukuacha, wanaweza kutumia mwavuli wa dini ili kuleta mvuto wa wewe uwakubali na kweli ukaingia. Mitandao imejaa wasanii wa mapenzi. Wanadanganya kuanzia umri, ukweli kuhusu watoto, kazi zao n.k.
Claudia mwana dada wa kimarekani mwaka 2010 ameshuhudia namna ambavyo alikutana na mwanaume twitter na siku tatu kabla ya harusi, alikuta ujumbe ktk email ya mume mtarajiwa kutoka kwa mkewe na watoto wake wakimuuliza lini atarudi nyumbani..
UTAMJUAJE MUONGO
Jipe muda

II: JIHADHARI NA MARITAL STATUS
Ukitembea profile yake iwe facebook, twitter,n.k utakuta kajieleza kuwa yuko single, au recent out of relationship n.k
Wapo ambao kweli wanasema wakimaanisha lakini wengi wao bado wapo ktk mahusiano ila wamekosa uvumilivu wa matatizo madogo madogo ktk mahusiano yao, na hivyo wanatafuta mahali pa kuweka kambi.

III JIHADHARI NA PICHA UNAZOPOKEA
Sehemu kubwa ya picha ktk mitandao ya kijamii ni ile yenye mivuto, inayoita, inayoshawishi..ni picha zenye kuteka macho yako. Zimesafishwa vema na kompyuta kiasi cha kukufikirisha kuwa kuna malaika wamekuja kufanya tour duniani. Mf Joan ni mwanadada wa Afrika kusini, katika mkasa uliowahi kumpata ni kupokea picha za mwanaume handsome,iliyomtega, kumvuta na kujitoa tayari kwa lolote. Siku walipoonana alishangaa sana, sura ilikuwa ile aliyotumiwa hata hivyo udadisi wake ulibaini baadae kuwa zilikuwa za miaka mitano iliyopita, tayari mengi yalishapita ktk nyuso zake

IV JIHADHARI ZA BLOGI ZA WALIO SINGO
Bila shaka umekutana na blog ambazo ni maalum kwa wale walio single? Kama bado subiri, moja ya changamoto ktk blog hizi ni kuwa, kuna watu wamegeuza suala la kutafuta wachumba kama sehemu ya kipato. Maisha magumu bwana! Waishije mjini?? Hawa wanajua ku-fake maisha, maneno matamu, na wapo tayari kukulainisha ili tu uache pesa ya matumizi. Wanataka u-sign up, ukiingia huko basi watakugeuza nyumba ndogo.

V: JIHADHARI NA MASHUSHUSHU
Ktk hili, zipo taasisi au kikundi fulani ambacho ---------- tu kujua taarifa zako, kazi yako, we ni nani, unaishije n.k Hawa ni mabingwa wa ku-hack mawasiliano yako. Kama wewe ni mwanaume, wanapenda kutumia mbinu ya yule jasusi wa kijerumani aliyevumbua mbinu maarufu ya romance ktk upelelezi. Watatumia wanawake kukunasa! Ama sivyo watajitahidi kujua weak point yako lakini ukweli hawapo kwako kwa ajili ya mahusiano ya kujenga familia au ndoa na wewe!

MWISHO, Sio wote wana nia mbaya bali wachache tu wanawaharibia. La msingi jitahidi kutokuwa mwepesi wa kuamini, kujitoa maana ndoa inahitaji muda wala si mashindano.
Online relationships, don't run faster than your legs !!
(Joshua Fruhlinger is hereby acknowledged)
 
Shukraan rafiki...Ni kweli usemayo watu wa mtandaoni si wakuaminika...Kila mtu yupo kimaslahi yake....

^^
Hakika, umakini unatakiwa sana, ukimwona Mapi mwambie apite hapa tusikie maoni yake na watu8
^^
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Himidini umeeleza bayana kabisa mimi nakubaliana na wewe 100%!!!!!!

Wengi maisha yametuumiza ina one way or another na ni kweli tunahitaji consolation ili kuendelea kuishi ila tusiwe "victim of technological advancement" eti tu sababu ni rahisi kupata consolation kupitia mitandao hii!!!!!!

Ni zimwi linatutafuna kimyakimya thanx mkuu kwa kupaza sauti juu ya zimwi hili,mwenye masikio na asikie!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
wadada ndio tupo at risk sana kwa hawa wanaume wa mtandaoni wanaojifanya wanataka kutuoa! mtu anakutangazia ndoa hata kwa sura hakujui si majanga haya?

^^
DEMBA umesema kweli, wadada ndo wapo ktk mapenzi ya mitandaoni, kuna mdada mmoja mkoani mwanza, walikutana Facebook tatizo alifeki kuwa ana maisha bora, matokeo yake mdada akaingia king, na baada ya mwezi kafika rafiki wa mwanaume, kamnyanganya sofa, tv, kapeti na kitanda kwa madai mkataba wao umeisha. Ilibidi mdada atulizane.. Ukweli upo kiasi sana
^^
 
Last edited by a moderator:
wadada ndio tupo at risk sana kwa hawa wanaume wa mtandaoni wanaojifanya wanataka kutuoa! mtu anakutangazia ndoa hata kwa sura hakujui si majanga haya?
kwasababu mnaamini uongo kwa haraka na kwa wepesi kuliko ukweli
 
kwenye No. I umesema kuepuka waongo tujipe muda, sikubaliani na wewe kwani wapo waongo wa kudumu, kila kitu kwao ni fake, hana ukweli hata siku moja...sijui njia ya kuwaepuka, usije ukaniuliza labda mtu asipate tu hiyo bahati mbaya
 
Daima naamini hamna watu wanaokutana kwenye hizi sosho nertworking wakafikishana mbali

Kwanza naona ni vigumu kumantain kule kuheshimiana kati yenu kutokana na mazingira mliyokutana

Love doesnt ask why..hatukatai ila sio mbaya kujiuliza swali la kizembe kama hili; mtaani,kazini,chuoni na jamii zoooote zinamzunguka hakuona wa kumfaa mpaka alipokuona wewe kwenye blog!!!!!

Sanasana either she ataliwa MWILI au he aliwe MALI

Correct me with concrete evidence if am wrong.
 
Daima naamini hamna watu wanaokutana kwenye hizi sosho nertworking wakafikishana mbali

Kwanza naona ni vigumu kumantain kule kuheshimiana kati yenu kutokana na mazingira mliyokutana

Love doesnt ask why..hatukatai ila sio mbaya kujiuliza swali la kizembe kama hili; mtaani,kazini,chuoni na jamii zoooote zinamzunguka hakuona wa kumfaa mpaka alipokuona wewe kwenye blog!!!!!

Sanasana either she ataliwa MWILI au he aliwe MALI

Correct me with concrete evidence if am wrong.
You are absolutely right 🙂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom