Onja rosella wine - camarador

Onja rosella wine - camarador

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,615
upload_2016-8-25_13-40-44.jpeg

MNAKARIBISHWA CAMARADOR ESTAMINET - IGOMA MWANZA KUBURUDIKA NA WINE YA ROSELLA ILIYOANDALIWA KWA UMAHILI MKUBWA..
LINI: JUMAPILI TAREHE: 28 AGOST, 2016
WAPI: CAMARADOR ESTAMINET IGOMA MWANZA (NYUMA YA ST. MARY SCHOOL)
MUDA: KUANZIA SAA 08:00 MCHANA
NYAMA CHOMA, VITAFUNWA MBALIMBALI VITAKUWEPO.
 
Alcohol content ngapi? Bila hiyo tangazo lako ni sifuri. Na hiyo Rosella Juice ndiyo nini?
 
Alcohol kwenye wine huwa inaongezeka kulingana na muda unavyokuwa mrefu, ndo maana wine halisi haipaswi kuwa na expiry date.
Swali jingine mkuu!
 
Weka alcohol content ya wine yako acha maneno mengi. Waswahili bwana! Angekuwa mzungu angekuwa ameshasema 13.3% mjadala kwisha.

Kama hutaki kusema basi kanywe hiyo juice na familia yako!
 
Hakuna shida, najua hata kufika sehemu husika huwezi, wabongo mkiambiwa tembea uone mnakimbilia mjini kati, ingia sehemu za watu wanaoheshimu natural view!
 
Ndiyo maana hata biashara zenu hazitoki. Wakati wenzenu wanatumia mamilioni ya dola kutangaza biashara zao leo wewe mfanyabiashara uchwara umepata bahati ya kutangaza biashara yako bure hapa hata kuelezea biashara yako vizuri umeshindwa.

Mimi nimeuliza swali la msingi sana. Hiyo wine yako kwa sasa ina alcohol content kiasi gani? Badala ya kujibu swali unaanza uswahili. Nina collection ya wine hapa na huwa napenda kujaribu vitu vipya. Badala ya kunijibu umeanza malumbano na blah blah nyingi.

Wafanyabiashara wa Tanzania badilikeni na jaribuni kuwa siriazi na biashara zenu ikiwemo matangazo na customer service. Mko nyuma sana katika mambo haya ndiyo maana hamuwezi kushindana na wenzenu wa nje mf. Kenya.

Asante na ubarikiwe. Nitakuwa Mwanza Septemba 15 ndiyo maana nilikuwa naulizia specifics za hiyo wine yako. Bahati mbaya tumeshindwa kuelewana!
 
N

Nashukuru kwa ushauri wako mkuu,
Tunajifunza kutokana na makosa, kama nisingetangaza hapa nisingejua hayo mapungufu ambayo sasa nimeyaona. Jambo uloniuliza kiukweli ni la msingi; nami nilivyokujibu sio kwamba ni blahblah, la hasha!
Wakati nakusanya vitendea kazi nilitafuta Alcohol-meter maduka karibia yote jijini Mwanza sikupata. Hivyo kiukweli siwezi kujibu swali lako kwa kuwa ni la kisayansi - nami sitaki kukudanganya. Nikifanikiwa kupata hicho kifaa cha kupima alcohol content kwenye vinywaji nitakupatia jibu.
Ubarikiwe na Bwana Yesu.
 
Asante. Yaani umetengeneza wine hata hujui alcohol content yake? Ukiendelea hivi kuna siku utakuja kuua watu. Umeshawahi kusikia ile mikasa ya watu wanakunywa pombe halafu wanakufa au kudhurika maini na wengine kuwa kwenye coma. Kuwa mwangalifu mkuu utakuja kunywesha watu wine haina alcohol (juice) au ina alcohol content 90% unaona wanaanza kudondoka mmoja mmoja.

Sikukatishi tamaa bali chukulia hili kama challenge za kawaida katika ujasiriamali.
 
Ahsante sana mkuu, nashukuru kwa walokuja wananitumia ujumbe kwamba ni nzuri sana, mi niko safari, kesho niko nao ili nipate mawazo yao kuhusu hiyo wine
 
hongera kwa kujirudi na kuwa muelewa .... kwa style hii ya kusikiliza unayo shauriwa utafanikiwa

I wish you all the best
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom