Ongezeko la watu wanaofuatilia video za Hayati Magufuli limenishitua

Kiturilo

JF-Expert Member
Sep 27, 2021
709
2,858
Rais Samia jikite kufungua na kuanzisha miradi, jikite kupambana na mfumuko wa bei, jikite kuhamasisha viwanda .

Viwanda ndiyo vitanunua mazao ya wakulima ,viwanda ndiyo vitazalisha ajira nyingi sana.

Huwezi kupeleka nchi uchumi wa kati kwa kukutana na Mbowe mara kwa mara.

Juzi Profesa Lipumba amenukuliwa akisema Rais Samia atashinda kwa kishindo mwaka 2025.

Zito Kabwe ndiyo hivyo tena amekuwa kasuku wa ccm kila siku ni kusifia tu.
James Mbatia ndiyo hivyo tena kutwa kusifia mama anaupiga mwingi.

Inasikitisha sana chadema kununuliwa, Lisu na Lema huko wanakolelewa wamekuwa kama misukule hawajui washike lipi waache lipi maana mwenyekiti wao hatabiliki, muda wowote anabadili gia angani kama alivyofanya mwaka 2015 kwa kununuliwa na Lowasa.

Mbowe alipotoka tu akakimbilia Ikulu kwenda kunywa chai badala ya kuwashukuru kwanza waliompigania!!.

Sasa tumaini pekee liliobaki kwa wapenda mabadiliko na ulinzi wa kweli wa rasilimali za nchi yetu ni UMOJA PARTY.

Mungu ibariki Umoja party ipate usajili haraka .
 
Sukuma gang mtakuca kwa msongo wawazo. Mtajeni sana tu huyo shetani wenu wa Chato lkn hafufuki tena na hatutawaruhusu mrudi ikulu tena.

Kama unaumia nenda kazikwe naye Chato
 
Mkuu kama una ile video ya magufuli kipindi cha tetemeko la bukoba iupload tuone vitu
 
Umenikumbusha Ucheshi wa JK NYERERE uliokuwa ukichanganywa na ujuzi,taarifa &maarifa yake: aliwahi kusema "congo zaire sasa nasikia wanavyama 100,sijui bado havijawatosheleza", NB:CCM NCHI HII WALISHASHINDWA KULETA MAENDELEO,KWA MTU MAKINI HILI HALINA MJADALA:
 
Mwacheni mama afanye kazi.. Acheni maneno maneno..
Uchumi umeshaanza kupaa kutoka ukuaji wa around 4% p.a alipopokea nchi na mpaka sasa umefikia just over 5% p.a huku matarijio yakitegemewa kuwa close to 7% p.a ndani ya muda mfupi.
Usilazimishe Samia atawale kama JPM. Kila kiongozi ana style yake ya kuongoza Taifa.
Mama anajitahidi sana kurudisha taswira/heshima ya Tanzania iliyojijengea kimataifa tokea uhuru. Heshima ambayo ilivurugwa na mtangulizi wake.
Mkiona anasafiri sana mjue hii ya kurudisha heshima ya Taifa ni moja ya kazi kuu alizopangiwa na mpaka sasa matunda tumeanza kuyaona na heshima ya nchi imeanza kurejea kama wakati wa nyuma.
Wapumbavu wasioelewa wanabeza safari zake nje. Hawa watu ni wa kuwapuuza tu.
...
..
.
 
Back
Top Bottom