Ongezeko la vifo vya wanaume........................

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,090
Jana wakati natizama taarifa ya habari ya saa mbili usiku kulipita habari moja ya uzinduzi wa kampeni ya kuondoa unyanyasaji wa kijinsia iliyokuwa inazinduliwa na Mh. Celina Kombani. Sasa mmoja wa watu waliokuwa pale akasema maneno yaliyonifanya nitafakari kidogo,

Akasema "Tangu hizi kampeni za usawa na habari za urithi zimeanza kumekuwa na ongezeko kubwa sana la ndoa kuvunjika tofauti na zamani" Hilo likanifanya nitafakari kidogo, ila kali zaidi likawa kwamba "Tangu hii habari ya urithi imepigiwa chapuo na hao wanaharakati vifo vya kina baba walioko kwenye ndoa, hasa wale wenye uwezo kidogo vimeongezeka maradufu" akataja na makabila ambayo yanaongoza kwa hilo (Nayahifadhi)

Hebu tulijadili kidogo hili, hivi lina ka ukweli?
 
Hiyo tafiti nayo wajameni! Juzi alikufa Mr. Ebbo na yeye ni Mmasai!
 
Hahahahaaa hapo sitii neno lakini nimesema kuna makabila ambayo yanasemekana wanawake wake wamekithiri kwa tabia hiyo ya kuwaondoa waume zao
 
mmmmh no comment hapa. acha waje wanaume ...leeeo!!!

ila wana data kamili? walifanya research ya ukweli au research zetu za magumashi?
 
Hiyo tafiti nayo wajameni! Juzi alikufa Mr. Ebbo na yeye ni Mmasai!
Hahahahaaa hapo sitii neno lakini nimesema kuna makabila ambayo yanasemekana wanawake wake wamekithiri kwa tabia hiyo ya kuwaondoa waume zao
 
bora na mimi nife, nina madeni ile mbaya na hadi muda huu sijapata mshahara, sijui hiyo morali ya kufanya kazi ntaipata wapi?
 
Hiyo kweli kabisa, kuna mtaa mmoja naufahamu, wababa wengi hawapo tena, wamama wamebaki wenyewe tuu,mm mwenyewe najiuliza ni coicidence au wanapanga??? mhhh naogopa sanaaa .....
 
Hahahahahaaa unaogopa kuoa au unaogopa kufa?
 
Musimo kwamba ongezeko la vifo vya wanaume linatokana na mambo vifo vingi ya urithi?...Well kwangu mimi hii habari naipa 50/50 sitaki kusema hiyo ndio sababu hasa kwa kuwa tumeshuhudia vifo vingi vikitokana na majanga mbali mbali kama vile kuumwa, ajali na kadhalika ingawa kuna baadhi ya imani watu hawajaondokana nazo
 
Kaka mi nakubaliana na wewe kabisa katika hili lakini kuna swali pia la kujiuliza, Kwanini wanaume zaidi?
 
Sasa km huu utafiti ni wa kweli huko mbele ya safari itakuwaje,hivi tunanyang'anyana wanaume hamtutoshi,mikizidi kufa sio itakuwa tabu tupu,mungu aepushie mbali au sie wanawake atupunguze kiaina ili namba ibalance na wanaume.
 
Niwahi mimi kabla sijawahiwa
 
Back
Top Bottom