Ongezeko la utoaji Mimba ni kubwa sana

Ongezeko la utoaji Mimba ni kubwa sana

WE ARE ANONYMOUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Posts
217
Reaction score
284
Je unafahamu kwamba unaweza kufanya utafiti na kupata interest za watu wa jamii flani kwa kutumia search engine especially GOOGLE?

Search engine kama GOOGLE huwa inakusanya zile keywords zote ambazo watu wa eneo flani wanazi-search sana, halafu inazitengenezea "suggestion" kwamba mtu ukianza maneno machache tu, basi inaleta zile suggestions za maneno ambayo watu wanaya search zaidi ya mengine.

Basi leo nikawa nataka kufahamu jinsi ya kujiunga na vyuo vya ufundi (VETA) coz kuna dogo ameomba nimchekie, ikabidi nianze kuiuliza GOOGLE, kama kawaida nikafungua GOOGLE na kuandika neno JINSI YA..... kabla sijamaliza kuandika sentensi nzima nashangaa nakutana na suggestions hizi kama nilivyoweka hapa chini:

mimba.PNG

Kwa kweli nilistuka ikabidi nililete hili suala MMU, ili wadau mfahamu kwamba tunapowagegeda hawa warembo, basi tujitahidi kuepuka mimba ambazo hatuna mpango wa kuzilea ili kuepuka dhambi hii mbaya ya uuaji.

Wasalaam
 
Mkuu unashangaa nini wakati kuna nchi sheria imeruhusu kabisa?
Nilishangaa sana kuambiwa na daktari moja hivi kwamba wanaongoza kwa kutoa mimba ni wanandoa pamoja n watoto wa shule za sekondari. Umri wa katikati kama wanachuo wanatoa lakini siyo sana, washakuwa wajanja hawapati mimba za hovyo hovyo.
 
Swala sio kushangaa wala nchi flani kuruhusu, swala ni ONGEZEKO mkuu! Rate ni kubwa sana!
Uko sawa kabisa kiongozi, ndiyo maana hapo juu nikasema wanaopata mimba sana ni watoto wa sekondari na wanandoa. Vitoto viko kwenye balehe na kuvunja ungo huko shule havujui kitu wala kufikiria madhara unategemea nini? Upande wa pili wanandoa inafika kipindi wanapitiwa hata njia za uzazi wa mpango zinakuwa ngumu, hasa ukifikiria kwamba idadi kubwa ya Watanzania wanatoka kijijini na elimu hawana. Kutoa watatoa sana mkuu mara nyingine bila hata waume zao kujua.
 
Ni kweli mkuu, hatari sana!
 
unashangaa nini wakati mnagegedana hovyo hovyo tena peku peku bila malengo
 
Back
Top Bottom