Ongezeko la maji Bwawa la Mtera wananchi watahadharishwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limewatahadharisha wananchi wa vijiji vilivyopo kandokando mwa bwawa la Mtera na Kidatu ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, uvuvi na makazi kuwepo kwa ongezeko kubwa la maji kwenye bwawa la Mtera hivyo shirika hilo kulazimika kuyafungulia maji hayo yaliyohifadhiwa kwenye bwawa hilo.

Wakizungumza katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera kilichopo mpakani mwa Iringa Na Dodoma uongozi wa TANESCO umesema wanalazimika kufanya hivyo kutokana na bwawa hilo kujaa maji kupita kiasi ambapo wasipofanya hivyo kutaathiri uzalishaji wa umeme katika vituo hivyo.

Aidha, baadhi ya wakazi wanao tegemea bwawa hilo katika shughuli zao za kiuchumi wamebainisha kuwa tukio kama hilo limewahi kufanyika miaka ya nyuma na kuwaathiri kiuchumi.

Chanzo: ITV
 
Aisee mheshimiwa samahani, Hivi hiyo nyama inayouzwa kwa fujo hapo Izazi ni ya Mbuzi kweli!! Au ni ya yule mlinzi wetu wa usiku?

Huwa napita pita sana hapo! Ila nimekuwa nikiihofia kama nihofiavyo ile nyama ya wale Wamasai wa kule Mikumi.
kwa nn uhangaike.si ule samak wale rena wamama wale wanapandaga nao bado wamoto kabisa. ila mtera kujaa asee noma mana darajan pale ukiangalia kwa chin kile kina balaa.asee
 
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limewatahadharisha wananchi wa vijiji vilivyopo kandokando mwa bwawa la Mtera na Kidatu ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, uvuvi na makazi kuwepo kwa ongezeko kubwa la maji kwenye bwawa la Mtera hivyo shirika hilo kulazimika kuyafungulia maji hayo yaliyohifadhiwa kwenye bwawa hilo.

Wakizungumza katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera kilichopo mpakani mwa Iringa Na Dodoma uongozi wa TANESCO umesema wanalazimika kufanya hivyo kutokana na bwawa hilo kujaa maji kupita kiasi ambapo wasipofanya hivyo kutaathiri uzalishaji wa umeme katika vituo hivyo.

Aidha, baadhi ya wakazi wanao tegemea bwawa hilo katika shughuli zao za kiuchumi wamebainisha kuwa tukio kama hilo limewahi kufanyika miaka ya nyuma na kuwaathiri kiuchumi.

Chanzo: ITV
Daaah, tuongeze tu mitambo ya gesi kinyerezi
 
Back
Top Bottom