Ongezeko la kasi la ujenzi wa vituo vya kujazia mafuta (Petrol & Diesel)

bmk

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
571
857
Heri ya mwaka mpya?

Kama wewe ni msafiri maeneo mengi sana nchini yanajengwa Vituo vya kujazia mafuta. Mfano ukitoka Dar es salaam kuelekea tunduma...Njiani ni mamia ya vituo yanajengwa hasa kampuni ya "LO". Dah aisee hii kampuni inavituo jamani yaani huwezi tembea 200km hujakutana na kampuni hii...

WACHUMI MTUSAIDIE:
• Hii inamaanisha nini kiuchumi? Kwamba uchumi unakua vizuri hasa ukizingatia moja ya drive za uchumi ni MAFUTA?

• Kama mmegundua ujenzi huu wa kasi umeanza kuanzia mwezi wa nne mwaka 2021...Hii inamaanisha nini kwamba raisi hayati Jpm alibana watu wasijenge AU lile bomba limetengenezewa koki ya pembeni baada ya kuondoka kwake?

• Kama mafuta ni mengi kwa maana ongezeko limekuwa kubwa, kwanini hayashuki bei?

Nitafurahi nikipata majibu hasa ya kiuchumi zaidi.

Ahsante.
 
Aisee ni kweli kabisa..nawe macho yako yanaona kama mimi. Hawa Lake Oil wanafungua kila uchwao. Mbaya zaidi unakuta petro station zinafuatana mita chache tu.
Tunawashukuru kwa kutengeneza ajira, ila kuna nini kwenye hiyo biashara? Seem like FAIDA ni kubwa ndiyo maana biashara hii inashamili sana.
 
Heri ya mwaka mpya?

Kama wewe ni msafiri maeneo mengi sana nchini yanajengwa Vituo vya kujazia mafuta. Mfano ukitoka Dar es salaam kuelekea tunduma...Njiani ni mamia ya vituo yanajengwa hasa kampuni ya "LO". Dah aisee hii kampuni inavituo jamani yaani huwezi tembea 200km hujakutana na kampuni hii...

WACHUMI MTUSAIDIE:
• Hii inamaanisha nini kiuchumi? Kwamba uchumi unakua vizuri hasa ukizingatia moja ya drive za uchumi ni MAFUTA?

• Kama mmegundua ujenzi huu wa kasi umeanza kuanzia mwezi wa nne mwaka 2021...Hii inamaanisha nini kwamba raisi hayati Jpm alibana watu wasijenge AU lile bomba limetengenezewa koki ya pembeni baada ya kuondoka kwake?

• Kama mafuta ni mengi kwa maana ongezeko limekuwa kubwa, kwanini hayashuki bei?

Nitafurahi nikipata majibu hasa ya kiuchumi zaidi.

Ahsante.
Kinachofuata hapo, ni marekebisho ya kanuni/sheria za ugavi, ili kuruhusu magari ya serikali kununua mafuta kwenye hivyo vituo. Back to ufisadi 101.
 
Wafuta wanapandsha Bei kisa wanamiliki sheli.. ×4

Namimi nampango wa kufungua petroleum station..
 
Barabara ya MBEZI - GOBA - MBEZI BEACH ina urefu 16 km tu lkn kuna Petrol Stations kama 20 hv na bado zinajengwa!
 
Back
Top Bottom