Hongera kwa uamuzi wako! Nina maswali mawili tu,
1. kwa nini mashabiki wako wengi waliomo humu ni manazi wa CCM, huoni inakutia doa?
2. Vijana wengi wa ACT waliomo kwenye jukwaa hili wamekuwa wakiishambulia chadema, mfano ACT yachukua wanachama wa chadema. Pamoja na yote haya, hatujasikia kauli ya chama juu ya hili. Houni hili bandiko lako haliwiani na kile kinachoendelea kivitendo?
Siasa ni mapambano. Siwezi kuacha mapambano. Sijawahi fanya usaliti wowote. kuitana majina hayo hakusaidii lolote zaidi ya kufurahisha ego zetu tu. ACT Wazalendo ina shabaha moja tu nayo ni kupambana na mfumo wa uchumi unaonyonya watanzania. Ku surrender mapambano hayo ndio usaliti. Tutaendelea kupambana
Tumeshaonya wanachama wetu wote kutoshambulia chama chochote cha upinzani. Walikuwa wanachokozwa na wao kujibu mapigo. Hata hivyo haina tija na tumeamua kuwa hata tukichokozwa tunasema " tumeshapiga mstari. Forward ever backward never". Hatutachokozeka tena. Kazi yetu kueneza Sera za ACT Wazalendo
Tumeainisha vizuri sana kwenye ilani yetu ya uchaguzi mwaka 2015 na tutafafanua zaidi kwenye Azimio la Arusha lililohuishwa. Moja ya sera zetu ni kukomesha kabisa uporaji wa ardhi nchini kwa kuhakikisha wananchi wanamilikishwa ardhi ya kilimo na ufugaji. Mashamba yote yaliyokuwa ya NAFCO yakabinafsishwa yatarejeshwa kwa wananchi na kugawiwa kwao kwa kilimo kwa mfumo wa outggrowers scheme.
ACT Wazalendo imeamua kusimama masuala yanayohusu wananchi. Naomba upate nakala ya ilani yetu uweze kujisomea
Zitto nini chanzo cha mapato ya Chama cha ACT maana ninajua hampati ruzuku.
Utafikiri kweli, kweli wanasiasa mmetufanya sisi maboyaTumeweka utaratibu wa kuweka vyanzo vyetu vya mapato wazi na kukaguliwa na CAG. Tutaweka kwenye tovuti ya chama