Ondoka kabla hujaondolewa kwa aibu

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
4,091
2,000
ONDOKA KABLA HUJAONDOLEWA KWA AIBU

Anaandika, Robert Heriel

Dunia ndivyo ilivyo, ONDOKA! Usisubiri AIBU! Dunia haitaki watu wanaosubiri. Dunia haitaki watu wasiojiongeza. Usipojiongeza dunia itakuongeza. Ondoka usisubiri.

Mchana huondoka na kuuacha usiku, nao usiku huondoka kuuacha mchaña. Hakuna asubiriye kuondolewa, kuondolewa ni Fedheha kubwa mno.

Kuku anapototoa, wakati vifaranga vikiwa vidogo kabisa Mama kuku huwa karibu Sana na wanawe, huwa na uchungu, huwa mkali Kwa yeyote atakayewasogelea watoto wake. Ni wakati hasa wa Mama kuonyesha upendo wake Kwa watoto wake. Huwakumbatia na kuwaficha katika mbawa zake na kuwapa joto Kwa sababu vifaranga havina mabawa.

Huwachakuria na kuwatafutia chakula Kwa sababu vifaranga bado kucha zao haziwezi kuchakura ardhi laini na wala haviwezi kujitafutia chakula.

Lakini kadiri muda unavyoenda, vifaranga vinavyozidi kukua ndiyo uangalifu wa mama hupungua, ukali nao hupungua, upendo Kwa watoto hupungua, hii ni kutokana na kuwa watoto tayari wanaweza kuhimili baadhi ya MAJUKUMU.

Vifaranga vinavyojielewa vikishaona vimekuwa vyakutosha huondoka chini ya uangalizi wa mama yao ili visiondolewe kwa aibu. Huondoka Kwa heshima pasipo kufukuzwa. Lakini vifaranga vile vinavyodeka visivyojiongeza, ambavyo havitaki KUONDOKA huondolewa kwa nguvu, hupigwa na Mama kuku, huondoka Kwa aibu.

Hivyo hivyo kwa NG'OMBE na wanyama wengine.

Ukiwa kama binadamu, uwe na hekima. Usiruhusu kuondolewa kwa aibu. Usisubiri kufukuzwa.

Unajua kuna kufukuzwa au kuondolewa Kwa aina nyingi ; kuna kuondolewa kwa maneno ya moja kwa moja, na kuondolewa Kwa matendo.

Vijana wa sasa lazima hili likae kichwani, usikubali dunia ikuondoe Kwa aibu, ondoka mwenyewe. Jitegemee. Usikubali kudhalilishwa.

Biblia unasema; usikubali mtu adharau ujana wako.

Ondoka kabla hujaondolewa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom