Ondoka Dar, unapoteza muda!

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,864
Reaction score
3,979
ONDOKA DAR, UNAPOTEZA MUDA!

Vijana wengi tunakimbilia Dar es Salaam tukiamini kwamba ndipo maisha yanapojengwa. Tunatumia miaka mingi kutafuta riziki kwenye jiji ambalo gharama za maisha ni kubwa, huku tukisahau fursa zilizopo mikoani.

Wenzako waliobaki mikoani wanakamata heka za viwanja, wanajenga nyumba, wanawekeza kwenye mashamba na kuanzisha miradi ya muda mrefu.

Wewe umeng'ang'ana Dar, kila siku unapambana kuuza karanga, kulipa kodi, nauli na gharama nyingine za maisha. Miaka inapita, lakini huna hata kipande cha ardhi cha kuwarithisha watoto wako.

Dar es Salaam ni mji mzuri wa kutafuta biashara, kutumia vipaji na kutengeneza connection, lakini si lazima uwe sehemu bora ya kujenga utajiri wa muda mrefu kwa kila mtu.

Jiulize maswali haya:

  • Unafanya kazi kwa bidii, lakini unawekeza wapi?
  • Miaka 10 ijayo utakuwa na nini cha kuonyesha?
  • Watoto wako watarithi nini kutoka kwenye juhudi zako?
  • Kwa nini usitumie kipato unachopata mjini kuwekeza mkoani?

Ndiyo maana unaona watu wengi wakistaafu wanarudi mikoani. Wengine wakipata changamoto za kifedha wanarudi nyumbani kwa sababu huko wanaweza kuwa na ardhi, familia na gharama nafuu za maisha.

Ukweli ni kwamba, si lazima uishi mjini ili uwe tajiri. Wakati mwingine, utajiri wako unaweza kujengwa sehemu ambayo wengine wanaikimbia.

Vijana, tusikimbilie maisha ya mjini bila mpango wa maisha ya baadaye. Tafuta kipato mjini kama kuna fursa, lakini usisahau kuwekeza nyumbani.

Mimi ni kijana wa mkoani, na naamini fursa za kujenga maisha hazipo Dar es Salaam pekee.

Mkoani pia kuna maisha, ardhi na fursa kubwa za uwekezaji!

NB: MKOANI SIO KIJIJINI mkoani kuna maeneo yanayokua kwa kasi sana ambayo yapo mjini
 
Ungetaja tuende kijiji gani ambacho tutaenda wekeza bila mtaji
Pili ungetuambia hayo mashamba tutakayoenda wekeza ni haya haya tuliozaliwa tukakua nayo tukilima bila mafanikio hadi tukakimbilia mjini au ni mashamba mengine?
 
Unawakosea sana wakazi wa dar, ningekuwa ni Mimi ningewashauri wabakie maana maisha ya dar ni ya kawaida sana na hayana utofauti na maisha ya mikoani...Sema dar wageni ni wengi kuliko wazawa ndio maana.

Ondoka Dodoma nenda mikoani maana gharama za maisha Dodoma ni kubwa sana ...utatumia nguvu kubwa sana kutafuta pesa alafu utazitumia hizo pesa kununulia chakula tu sababu ya gharama kubwa ya maisha. Hatuishi milele tucheze na fursa kwa ajiri ya ustawi wa maisha yetu.. (ugumu wa maisha ya dar hauwezi kuufikia ugumu wa maisha yaliyoko Dodoma)
 
Wenzako waliobaki mikoani wanakamata heka za viwanja, wanajenga nyumba, wanawekeza kwenye mashamba na kuanzisha miradi ya muda mrefu.
Sio ukweeli km unavyosimuliwa mkuu hizo zipo kwenye PDF kwenye ground ni tofauti kabisa, nishawahi enda huko bush yes nikakuta wanakodi mashamba makubwa kwa bei ndogo sana ila kilimo ni cha kubet yaan ukiotea umeula ukikosea umeliwa, nilishauriwa hilo pia kabla sijaingiza miguu yangu na kweli kipindi nilichoenda kilikua cha ukame hakuna alielima mpunga na mashamba yalikua wazi nikaambiwa humu unamomuona mvua ikinyesha maji yanajaa sana na mpunga unastawi mno ila kipindi kile kulikua kukame kumekauka na hakuna anaelima sasa usishangae unapowaona wapo Dar huko shamba ni kukame unataka wakalime nini mawe?
 
Dar is Overated,
Nimebahatika kukaa Mikoa mbalimbali kwenye miji tena kama Mgeni.Kwa Mkazi wa Dar kuondoka DAR sio suluhu ya Changamoto zake ili kutoka nje ya Dar kwa ajili ya kutafuta FURSA ndio Suluhu.

DAR sio ya kuikimbia.Kimsingi kila mpambanajia anahitajia kuanzia au kumalizia DAR.Huko Kwingine PITA utumia FURSA ila Kilele au Msingi uwe ni DAR maana Hela yote inaanzia DAR na KUISHIA DAR.

Kama Dar inakushinda hata huko kwingine ukikimbilia huko Patakushinda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…