On Star TV: TCRA na majibu kwa maswali juu ya Mfumo wa Digitali

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Kumekuwepo na hofu, masuala na sintofahamu nyingi kutoka kwa watanzania juu ya kubadilika kwa mfumo wa urushaji wa matangazo ya Radio na Luninga kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali.

Tumemualika mahususi Meneja wa Uhusiano wa TCRA Bw. Innocent Mungi kufafanua utata na sintofahamu inayowakabili watanzania katika kuelekea kwenye mbadiliko haya: karibuni kwa Maswali na maoni yenu wadau.

Kipindi kitaanza Saa Moja na Nusu Asubuhi ya Leo. Si vibaya akakutana na Maswali yenu Moja kwa Moja.

Nawasilisha
 
Mkuu Yahya kwani hakuna siku ya Tuongee asubuhi ya Masuala ya Technology? Tumezoea Jumapili mnajadili masuala ya Siasa.

Hata hivyo tutamsikiliza maana ni kweli kuna sintofahamu nyingi kuhusiana na mabadiliko haya.
 
Swali :Kuna baadhi ya channels mfano DTV,Capital,C2C,StarTV,ITV hazipatikani kwenye king'amuzi cha starTimes lini mtaanza kuzirusha humo? Au mnasubiri zimamoto hiyo Dec 31 kwanin tcra msiwaamulu haya makampuni yaanze kurusha mda huu ili ikifika dec 31 tuweze kujua mapungufu yake ili tuweze kuyarekebisha?

Maoni yangu:Naomba tcra myaambie hayo makampuni ya ving'amuzi yapunguze bei ya kulipia hyo elfu 9000 ni kubwa!
 
Kwa hakika ni Angalizo zuri Mkuu, mtuvumilie kwa Leo twende pamoja ktk mjadala huu hasa baada ya kuchanganywa utekelezaji wake na usimamimizi wa sera.
 
Je ni kweli kwamba zile free on air channels zitapatikana kwenye ving'amuzi vyote bila malipo? yaani hata kama mtu hatakuwa na uwezo wa kulipia kwa mwezi lakini channel hizi atakuwa na access nazo kupitia hivi ving'amuzi?
 
Mpaka August hii sioni chochote kinachoendelea hapa Mtwara juu ya matayarisho ya digitali, au ndio mtazomo wa kusini hakufai unaendelea?
 
Hata mie nilijua leo tutaendelea na siasa zetu, maana tuna mambo mengi bado ya kujadili mfano,
  1. Ruzuku kwa vyama vya siasa, kama tuendelee kuwapa wanasiasa zaidi ya 1.2b kila mwezi au hapana
  2. Rais wetu aendelee kutolipa PAYE (kama ilivoanishwa kwenye sheria mbovu ya sasa ya kodi ya mapato),
  3. Je tuweke ukomo wa chini wa elimu (minimum education qualification) kwa mtu kuwa mbunge?
  4. Serikali kupoteza kila kesi inayopelekwa mahakamani, kelele nyingi za ufisadi na kesi za hapa na pale lakini hakuna kigogo hata mmoja amewahi kuwa convicted.

Lakini tutamsikiliza Mungi.

Swali:

Walisema mtu hatalazimika kununua vinga'muzi zaidi ya kimoja kwa sababu hizi local channels zitapatikana kwenye ving'amuzi vyote tena bure (i.e kama king'amuzi chako kimeisha pesa basi hizi local channels utaendelea kuzipata, kama ilivo TBC1 kwenye startimes), Je, wamefika wapi na huo mpango? maana StarTV siwapati kwenye kingamuzi changu!
 
kwanini mkoa wa morogoro bado haujaunganishwa na mfumo wa digitali,tofauti na mikoa mingine ambayo tayari wameanza kutumia mfano startimes na mifumo mingine haijanza kurushwa ktk mkoa huu?
 
Natamani niulize swali lakini hapa nilipo siipati access ya tv sijui itakuwaje? Nimekuwa nikishangaa kila wanapoongeza station mpya na gharama zinaingezeka hii inaonyesha ni bora hata dstv maana haya makampuni yaliyopo nchini yamekosa uzalendo na hayana nia ya kuonyesha local station zetu kwa ujumla wake.
 
Nimesikia kuwa kutakuwa na punguzo la kodi kwenye ving'amuzi..suala hili litatekelezwa kwenye bajeti ya mwaka huu? na je nini faida ya mkonga wa Taifa wa mawasiliano kwenye kupunguza gharama za mawasiliano ikiwamo Internet?
 
kwanini bei ni kubwa sana hasa zuku,yaani unalipia elf arobaini halafu vipindi vyenyewe ni vibovu,kwann serikali wasiwe na utaratibu wa bei elekezi ili watu wa chini tuweze kumudu kulipia.
 
Kwa mkoa wa Kagera ndo kabisa sioni kitu. Wapo baadhi ya watu wanahangaika kununua madish. Kiukweli elimu haipo kwa wananchi juu ya mabadiliko haya. Isitoshe kuna kampuni moja juzi nanenane ilikuwa ikinadi ving'amuzi lakin bei yake hadi kufungiwa ni shs 420,000. Bado unalipa kila mwezi sh 20,000. Je gharama hizi wataweza watz kweli?? naomba ufafanuzi hapo.
 
Swali :Kuna baadhi ya channels mfano DTV,Capital,C2C,StarTV,ITV hazipatikani kwenye king'amuzi cha starTimes lini mtaanza kuzirusha humo? Au mnasubiri zimamoto hiyo Dec 31 kwanin tcra msiwaamulu haya makampuni yaanze kurusha mda huu ili ikifika dec 31 tuweze kujua mapungufu yake ili tuweze kuyarekebisha?

Maoni yangu:Naomba tcra myaambie hayo makampuni ya ving'amuzi yapunguze bei ya kulipia hyo elfu 9000 ni kubwa!

sio swali hilo: wewe unawasiwasi.
 
Nchi hii kuna mfumo mbovu wa utoaji elimu kwa umma?? Au wananchi kushindwa kufahamu mambo kwa muda mwafaka ndio iwe kipimo cha elimu ya watanzania?? Elimu ya watu wazima + Memkwa iamshwe usingizini
 
Pamoja na kuwa na washindani watatu wa huduma za digitali,waTanzania hatujaandaliwa.Pamoja na kufanya uhamaishaji kwa watu wengi lakini watu wa vijijini hawajafikiwa.

Swali: Je, lini wanatoa huduma za digitali wataingiza channel za ndani kwenye ving'amuzi vyao ili kuepusha watu kutumia ving'amuzi zaidi ya kimoja?
 
Kuna baadhi ya chanel hazipo kwenye zuku,je tcra mnasemaje kuhusu hili?swali la pili,ni king'amuz kipi mnashaur kutumiwa au makampun ya kuuza ving'amuz yamegawana maeneo mfano njombe star times hakuna ila makambako ipo,ufafanuzi tafadhali
 
Nawashangaa sana wenye dhamana na haya mambo! Wanashindwa kuwa na legitimacy katika hili; tumenunua ving'amuzi, ili ving'amue, suala la kuuziwa antena ni la nini? Wametoa antena za ndani, hazikamati...

Wwametufanya wajinga sana, wanatufanyia biashara kuuza bidhaa zao, kama ni antena king'amuzi tumenunua, iweje tununue antenna za nje na milingoti? Teknolojia ipi hapo mnayosema.

Hamuoni mmeshindwa kurusha mawimbi? Ukifika ofisini wanasingizia busta hazijafungwa, ni maendeleo ndio, na ni taratibu lakini tunalipa pesa, haiendi kihalali!
 
Back
Top Bottom