Omegle: 'Natumika kuvutia watu kuangalia ngono mtandaoni bila kujua'

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Ilani: Taarifa hi inahusisha mada za ngono.

Michael alikuwa na miaka 14 alipoingia kwenye tovuti ya video za ngono unaoitwa Omegle.

Aliusikia mtandao huo kwa mara ya kwanza akiwa shuleni na kuvutiwa nao.

Ndani ya saa chache toka alipoingia mtandaoni, akaunganishwa na mwanamke ambaye alikuwa na umri mkubwa zaidi yake na akamshawishi kumuonesha uume wake.

"Sina hakika kama alikuwa mtu mzima ama la, lakini alikuwa mkubwa kuliko mimi."

"Ninakumbuka akiniuliza kama nilitaka kumuona akiwa uchi. Nakumbuka akiniambia nipige punyeto huku nikimuangalia. Nilifanya hivyo kwa kuwa nilikuwa mjinga. Laitani ningeliweza kurudisha muda nyuma, ningelijizuia kufanya hivyo."

Michael akatoka mtandaoni haraka baada ya tukio hilo na akaendelea kusalia na hofu juu ya kilichotokea.

Lakini hamu na udadisi wake ukamshinda na akarudi tena katika mtandao huo akiwa na miaka 18.

Hatua hiyo ikasababisha kufanyika kwa mlolongo wa matukio ambayo mpaka sasa si bado tu yanamzonga, lakini yanamfanya kujiuliza iwapo mwanamke yule wa awali alikuwa ni mtu kweli ama la.

'Nikapa uraibu'

"Nikaanza kuingia kwenye mtandao mara kwa mara na kufanya 'vitu' mbele ya camera na watu tofauti tofauti. Ngono ya viodeo."

Michael anasema akapata uraibu wa ngono na ikamlazimu "kuachana" na mtandao huo baada ya miezi kadhaa ya kufanya vitendo hivyo mtandaoni kwa ridhaa yake.

Akaendelea na maisha yake na kuishau kabisa Omegle mpaka siku moja alipokuwa hana cha kufanya akiwa anajitenga kuepuka maambukizo ya corona mwaka jana.

"Nikaamua kuingia tena mtandaoni. Mara niakunganishwa na video yangu kwenye mtandao huo. Kuna mtu alirekodi video yangu na akawa anaitumia kwa zaidi ya mwaka mmoja."

Michael anasema alijigundua mara moja katika video hiyo na alijua vifeo hiyo ilikuwa ikitumia kitapeli.

Aliingia woga lakini akataka kujua nini kinachoendelea na akaanzisha mazungumzo na mtu aliyekuwa akiitumia.

Ghafla, akajitokeza na akajaribu kumshawishi Michael kwenye vitendo vya ngono.

"Ilikuwa ni mfumo wa hali ya juu wa mpangilio wa video. Waliibadili video yangu kurubuni watu kuvua nguo zao huku wakifanya nionekane kama mimi pia navua nguo. Wakaibadili badili mpaka kuonesha mimi nikipiga punyeto."

Kushawishi watu kufanya ngono
Michael (ambaye hakutaka jina lake halisi litajwe) anasema vido hiyo ina ushawishi.

Ana hofu pia kuwa watu wengine wanaweza kudanganywa na kuingia katika vitendo vya ngono kwa njia kama hiyo.

Michael aliwasiliana na BBC baada ya kuripoti kuwa watoto walikuwa wanajiingiza katika vitendo vya ngono kupitia mtandao wa Omegle.

Omegle inasema "imeshtushwa sana" na kilichomkuta Michael na "inaboresha njia zake za ukaguzi ili kuondosha" tabia hiyo mtandaoni.

Mtandao huo wenye maskani yake Marekani ambao unatumia lugha nyingi, ulianzishwa mwaka 2009, lakini ulipata ufuasi mkubwa wakati huu wa janga la corona ukitembelewa na watu milioni mbili kwa siku.

Umekuwa ni mtandao mkubwa zaidi kupitia video zake kupakiwa kwenye mitandao mingine mikubwa kama TikTok na YouTube.

Maelfu ya watu wanauwezo wa kuwa pamoja mtandaoni kwa wakati mmoja. Kuna ilani kuwa baadhi ya watu huenda wakawinda wenzao ama watoto wa chini ya miaka 18 ambao japo hawaruhusiwi lakini hakuna namna ya kuhakikisha umri wa watumiaji wake.

Hakuna namna ya kutuma malalamiko ama kuwasiliana na mtandao huo.
Michael, 21, anatokea nchi za Scandinavia, anasema anaweka wazi aliyoyapitia ili watu wajifunze na wajiulize nani wanaingia naye mtandaoni kufanya vitendo vya ngono.

"Napatwa na msongo wa mawazo, lakini walau napata amani kwa kuwa uso wangu haupo. Lakini inaniuma kuwa natumika kuwaumiza watu wengine. Naamini hii ni namna ambayo nilishawishiwa kuingia katika mtandao huu nikiwa na miaka 14, japo sina namna ya kuthibitisha kuwa mwanamke yule alikuwa ni wa kweli ama la."

Sarah Smith, kutoka taasisi ya usalama mtandaoni iitwayo The Internet Watch Foundation (IWF), anasema aina hizi za ushawishi wa kiulaghai zipo nyingi.

"Naweza kuvuta picha ni namna gani inaumiza kukuta video yako inatumika kwa namna hii, ulaghai huu unatumika sana kuwashawishi watoto kuingia katika vitendo vya ngono," anaeleza Bi Smith.

"Tumekutana na kesi ambazo watoto wakioneshwa video za watoto wengine wakiambiwa video hizo ni mubashara huku tukifahamu kuwa hilo haliwezekani kwa kuwa video hizo tuliziona kwengineko.

"Tumeliona hilo katika mitandao mingi ya video za ngono ambazo watoto hushiriki
IWF inasema ingependa kuona namna bora za ukaguzi wa maudhui mtandaoni na namna bora ya kuhakikisha umri wa watumiaji ili kuwalinda watoyo.

"Tunawataka watumiaji kuwa makini na ulaghai huu."

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom