Ombi La kuonana na Rais Mstaafu Kikwete

Mkuu sio kula MTU unamuona eti kwa kuwa una mapenzi naye,tengeneza CV yako be somebody utapata urahisi wa kumuona.sio lazima use kwenye siasa angalia mfano akina Mpoki walikwenda Msoga kumcheki na kupiga story naye 2 tatu.
Akina Mpoki walipata fursa hiyo sio kutokana na majina yao bali kazi zao.
 
Hapafu Lowassa usemeje,Tanzania nzima MTU anayeongozwa kwa kupendwa na watu ukimtoa Nyerere ni Lowassa hata Kikwete analijiua hilo,wa 3 ndio Kikwete.
Kuna ukweli

Navyojua maradhi tu ndio yanamficha Baba wa Watu
Angeonekana km JK naamini upendo wa watu ungezidi
 
Mkuu nafikiri watu wanaoniponda humu kwa hili Ombi langu nililolileta hapa wana mtazamo na maoni kama yako,kuwa lengo langu ni "kujiliza Liza" kama ulivyoandika hapo,nikuthibitishie tu kuwa siko kama mnavyodhani..its just an appreciations only..
Nadhani nitapata furaha isiyo na kifani kwa kuonana nae.kuna vitu kadha wa kadha nitajifunza kutoka kwake ila sababu ya Wabongo mnatanguliza njaa mbele ndio mana kila kitu mnafikiri kwa namna ya njaa njaa tu..
Nikujuze tu kuwa mm ni muajiriwa kampuni moja hapa mjini Daslam ninachokipata Alhamdulillah familia mke na watoto si haba..Nina mengi ya kukujuza kuhusu mm ila naona haina tija naomba niishie tu hapa asante..
 
Ni MTU wa watu huyu Mzee hana Maneno na MTU,tunaojua umuhimu wake ktk hii nchi tunamuombea kwa Mungu azidi kumpa Maisha marefu kama ya Mzee Mwinyi mana hekima na busara zake bado tunazihitaji kama Nchi.
Vipo vingi vya kujifunza kwa huyu Mzee kama tu kichwa chako kinafanya kazi vizuri.naamini nitaonana nae tu Inshaallah
 
Unashilingi ngapi nikufanyie uwepesi umuone mzee fasta ndani ya wiki tu
Bahati mbaya sana si muumini wa kuamini kuwa fedha ndio kila kitu kuna vitu vingine Uvumilivu tu unatosha,asante kwa msaada wako Sheikh
 
Mkuu nakuelewa sana si kila CV inaweza kukupatia unachokitaka pasipokuwa na connection, kuna baadhi ya kazi Nature yake inagoma kuLink na baadhi ya watu pasipokuwa na MTU wa kukushika mkono sidhani kama unanielewa lakini..
 
Nenda chalinze.
chap utamuona..
au fika msoga. ukifika kwake eleza shida yako watakupangia appointment naye.

kama unaona njia hizo ndefu.
nenda chalinze fika kwa riz then utakamilisha utaratibu wa kumuona JK.

Nje ya hizo jilipue humu humu jukwaani wapambe wake watapita watamuonesha naye ata ridhia utapata PM.

Kwa msaada zaidi njoo PM

NB HEPUKA MATAPELI
 
Anaonekana ana roho nzuri sana.
 
Nashukuru kwa Ushauri Mkuu ntajaribu kuufanyia kazi

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreā€¦