Elections 2010 Ombi la JF kwa ITV

Mambo Jambo

JF-Expert Member
Jul 11, 2008
1,100
81
Heshima mbele wazee.

Kutokana na watu wengi kulalamika kukatiwa umeme jana wakati kituo cha ITV kinarusha matangazo ya moja kwa moja na mgombea kiti cha urais kutoka chama cha CHADEMA Dr W.P. Slaa, nashauri watu wote wanaoitakia mema Tanzania kwa kuwa vyama vya upinzani havina bajeti kubwa za kampeni basi itakuwa jambo jema kwa kituo cha ITV kurudia mdahalo ule (recorded version) next week na iwe kipindi cha jioni au usiku ili watanzania wengi waweze kuona na kusikiliza sera, dira na majibu ya moja kwa moja kutoka kwa Dr Slaa.

Naomba watu wenye mapenzi mema tuandike email ITV kuwaomba warudie mdahalo ule (recorded) nadhani wakipokea email nyingi wanaweza kulifanyia kazi na kuutangazia umma ni lini kipindi kitarudiwa.

Ili kufanikisha zoezi hili tuma email kwenda:- info@itv.co.tz

Mimi wa wife tumekwisa tuma, kazi kwenu.



Taifa mbele vyama vya upinzani siyo adui.

MJ
 
MJ.

Nimeshatuma, na nimewatumia text jamaa zangu wawili wa kanada ya ziwa ambao walikatiwa umeme jana wakati wa mdahalo huo ili waongezee nguvu.
 
haya tuweke mafuta mwendo mkali, mie nsha tuma na washkaji kibao nawasiliana nao ili watume ujumbe kwa itv.
 
Hiyo sahihi kabisa, tunaomba ITV wapokee kilio hiki cha watanzania. Mzee MENGI anapambana na mafisadi na wazee wa unga, tunajua naye mpambanaji pia, tunamuomba KIPINDI MAALUM tena kwa watanzania kumsikia mkombozi wa taifa, Dr SLAA aweze kufikisha majibu kwa taifa na wale wote tuliojaa kiu nae. Chonde chonde MZEE MENGI, historia yako inaandikwa kwa taifa na mioyoni mwa watanzania.
 
Sounds good.
Wakati member wa JF wanatuma e-mail ITV.
Wasemaji wa Chadema wangetujuza what was the Deal between them and ITV.
Is it offer or they pay for the show! and from here we know who to reguest to show again .......................................................
Ni wakati mzuri na muhimu kama tunawasemaji wa Chadema humu Jf kutuweka sawa kwa baadhi ya mambo ambayo hayaendi ndani sana ya mikakati ya Ushindi 31/10/2010
 
Mie nashukuru mungu nilikuwa mmoja wa wale tuliojaliwa kuyaona mahojiano yale tangu mwanzo hadi mwisho. Ombi langu ni kurudiwa kipindi kile kila siku hadi October 30 na kama Kikwete atakataa Rais mtarajiwa Dr Slaa asishiriki hapo October 29 basi baada ya mahojiano ya Kikwete mahojiano na Dr Slaa yarudiwe tena.
 
tITLE IMEONYESHA KAMA mj NDIO MSEMAJI WA jf... SOMETHING NEEDS TO BE IMPROVED THERE
 
chama tawala kilifanya mambo.. kukata umeme! hehehe! i love ccm
 
tITLE IMEONYESHA KAMA mj NDIO MSEMAJI WA jf... SOMETHING NEEDS TO BE IMPROVED THERE

Unapenda sana kukosoa hata pasipo na msingi, mimi na jamaa kadhaa ambao ni member wa JF tumeona tuliweke hili wazo hapa ili wana JF baadhi wakiona ni wazo zuri watume email ITV na kuomba ITV warudie kipindi kile, hii inatokana na vyama vya upinzani kuwa na bajeti ndogo ya kampeni za uchaguzi, vyama vingine wamekuwa wanatengeneza documentaries na kuzilipia kwenye baadhi ya TV station hapa Tz ili ziwe-aired.

Keep in mind kuwa nikituma email ni natuma kama mimi na siyo admin wa JF na barua yenye JF letterhead.

Tuendelee kumkoma nyani.
 
poleni wakuu mliokatiwa umeme, ombi kwa ITV lipelekwe kurusha marudio, ilikuwa nzuri sana jana!!
 
Asante sana Selous.

Hii itakuwa kitu safi sana kwa democrasia ya Nchi yetu, watu waone, wachambue, wachague.
 
Back
Top Bottom