Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 11,136
- 19,872
Mh. Mkuu wa nchi hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwanza nakupongeza sana kwa uzalendo na kujituma kwako, ningependa nikufahamishe haya au nitoe kilio changu kwako nikiwa na kusudio Jema kabisa la kuboresha taifa na ustawi wa watu wake,
Nilikuamini sana na bado nakuamini kuwa unaweza kuibadili Tanzania yetu kuwa taifa kubwa lenye uchumi mzuri na ustawi safi wa watu wake. Fahamu/kubali yafuatayo:-
1. Taifa linakabiriwa na njaa,
Hapa Mh.Rais lazima uukubali ukweli huu ya kuwa sehemu kubwa ya taifa letu ina ukame na upungufu mkubwa wa Chakula kwa wananchi, serikali yako lazima ikubaliane na uchungu huu ili kunusuru wapiga kura ( wanyonge) waliokupeleka ikulu.
2. Kauli zako majukwaani Vs mategemeo ya wananchi wako.
Tafadhali mkuu wetu wa nchi Fahamu kuwa wewe ndio mlezi na mshauri ama mfariji mkuu wa watu wako, kauli zako zimekuwa zikikatisha mategemeo ya watu wako walioamini kuwa wewe ndiyo mtatuzi wa kero zao, kauli zako kuhusu baa la njaa ni moja ya mitihani midogo sana inayotaka kukuangusha.
Jaribu kuwa na namna nyingine bora ya kuwasilisha ukweli wako
"....sitatoa Chakula.." Kipande hiki cha hotuba hakiakisi kuwa kiliwasilishwa na mkuu wa nchi anayependa watu wake.
3. Haya yote ni kipimo kwako,
Mh rais wewe ni muumini wa ukiristo bila shaka umeshajisomea maandiko matakatifu na habari za watawala kama King Solomon, Daudi na wengine ambao walishinda vita na majaribu mengi kwa kuomba HEKIMA kwa Mungu,
Yawezekana majanga ya matetemeko, ukame na njaa ni kipimo cha mwazo kabisa ambacho Mungu ameruhusu kitokee kwenye nchi hii, cha kufanya kuwa karibu na watu wako unaowaongoza muwe na sauti moja kwa Muumba, usijitokeze peke yako kupinga hali halisi iliyopo nchini, Epuka kuwa na misimamo ya kukandamiza watu,
4. Kubali kushauriwa,
Sina uhakika sana juu ya nguvu au ushawishi wa washauri wako dhidi yako, huku nje picha inayojitokeza ni kuwa labda washauri wako hawana nguvu ya kukudhauri,
5. Epuka kutilia maanani kejeli, tilia maanani ukosoaji, wewe ni binadamu, usiendelee kudhibiti maumivu ya utawala wako kwa kuwakamata au kufukuza kazi wasema ukweli juu ya mwenendo wa serikali yako,
Tafadhali mkuu wa nchi ujumbe huu ukufikie, hata wasaidizi wako wakiuona wasiogope kukuambia,
Mungu ibariki Tanzania