Ombi kwa Mohammed Said kuhusu Saigon Club

SAUL BERENSON

Senior Member
Jan 31, 2017
150
154
Hii ni klabu hapa Dar es salaam ambayo kila Rais wa Tanzania alikuwa member (sina hakika kama huyu wa sasa, Magufuli naye ni member)

Wazee wetu na walikuwa members toka miaka hiyo sisi tunakua ya 1980's (wengine tumekuja kuiona baada ya kuhamia Kariakoo Mtaa wa sikukuu).

Mohammed Said tunaomba utupatie history ya club ya Saigon na why ilikuwa influential na ilikuwaje au factors zipi zilipelekea kushuka au kufa kwake?

Kwa nini haikuendelea kama social clubs zingine? Je wana assets na influence yao ilikuwa inaishia Dar tuu au au Dar and beyond?

Je Zanzibar kulikuwa na club similar to Saigon club?

Je bado wanafanya Khitma na kuftarisha mwezi wa Ramadhani?

Membership yao kupata nafahami ni ngumu na mpaka pewee reference, lakini je kuna restrictions zozote zile?

Kuna kipindi Iddi Simba walianzisha social club inaitwa wazawa je ilikuwa ni splinter group ya Saigon au?

Why the name Saigon?

Je kulikuwa na social members only social clubs zingine hapa Dar apart from Saigon and later on Dar Islamic Club?

Kwa nini Khitma lazima zifanyika pale kariakoo? Watu tumekuwa wengi na nafasi ndi ndogo kwa nini hizi annual events zisifanyika Mnazi Mmoja?

Je wameifanyia nini jamii? Halafu naomba unieleze what is this emotional attachment na hii club?


KLABU YA SAIGONI YAWAREHEMU WAZEE





Balozi Cisco Mtiror akisimamia ugawaji wa pilau baada ya kisomo cha kuwarehemu wazee wa Klabu ya Saigon mtaa wa Sikukuu jijini Dar Jumapili hii. Klabu hiyo ya michezo ni maarufu sana kwa watoto wa mjini ambapo wadau wengi mashuhuri waliitumia kwa kubadilishana mawazo na kucheza soka.


Mgeni rasmi katika Hitma hiyo, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Mh. Dk. Gharib Mohamed



Mjumbe wa kamati kuu ya saigoni, Mohamed Haruni (shoto) akiwa na mwanachama mwandamizi wa saigoni Ally "Stone" Mzuzuri




Balozi Cisco akiwa na wanachama wa zamani na wa sasa wa Saigoni
 
Saigon...what positive contribution does it have in the society? Wengi waliokuwa wanachama wake mhhhh
 
Niliambiwa hata Rais mstaafu Kikwete alikuwa mwana Saigon-sielewi significance ya Saigon-Wazee wetu walivyokuja mjini wakiisikia hii Saigon-lakini inaelekea uanachama ulikuwa open kwa wenyeji wa Dar tu
 
Niliambiwa hata Rais mstaafu Kikwete alikuwa mwana Saigon-sielewi significance ya Saigon-Wazee wetu walivyokuja mjini wakiisikia hii Saigon-lakini inaelekea uanachama ulikuwa open kwa wenyeji wa Dar tu
Jackline,
Nakujibu kama mwanachama wa Saigon na natanguliza hili ili ujue
kuwa Saigon una uongozi wake unaoweza kukupa majibu rasmi.

Saigon iko wazi kwa mtu yoyote haibagui.

Hapo tulipoanza katika miaka ya 1960 tulianza kama club ya mpira
wa mitaani na umri wetu wastani ulikuwa kiasci cha miaka 15 kwa
hakika tulikuwa watoto wa shule za msingi na waliokuwa sekondari
walikuwa wachache sana.

Siku hizo tulikuwa Mtaa wa Narungombe na hata chumba cha club
hatuna tumetundika bao na club ikijulikana kama Everton.

Baada ya kutoka katika utoto tushakuwa watu wazima club ikawa
bado ipo sasa inaitwa Saigon ingawa mpira hatuchezi lakini tunakutana
kwa kila siku kwa mazungumzo yaani ikawa ndiyo barza yetu.

XnZ9m0n_t36eZHaOYMzruahAQf2W2tz_ho8mvzuyyBJXq094MZKfYnFoEq_CbM4LmXXEax3gcqG6-IPGEAAG1jzBB-rwsxKtuWbinUbbc6ED3xSZ_r6X53nXDToJwHGY1ef8cqkoTCsZIxr9ic7tBCeCTcafG9dZ1zF93uwR2B6xAr9ilqwYMsNNEKfzwmSlTAu3txweuNPbtl0cH1rH9_KmPZ3hZN9k3XeVN_KatFktGj51cRjW3-6S_Be792TXpIQ-Xd3LvrWVE0tni6pjBOysqq1HgotfU4nmQoWUKIwUovv7ELyudMYbIaxosTPZtzPjmzAOL2ZtxDeU-eR2-25ShrDIOUsBjS7UDAW5PH2wWsugM74MXEProWT0otp8yeQAZQ3YX3DGjbmzywLq8nqb-2UQsLgFdTfFLz617Y6rUgkCoW7fT5cq703HdCpw9tHxLnPFsl6Q6kzAQPK3UGdiSaqGkpTtBcQIpXgViWenwBKvE2MYu5r-hdlwdlhIsAqV2bHqCopWEa1DJKXbhiz2vAcb4cx0X78sPgdR8kPjrk2HB8rdSY-Q_CNkakOxPac-zSYz487D2oW0EwReei48bK6i-qURevb7yFUdhFvm5PHWibQb=w1231-h692-no

Saigon Club Mtaa wa Narung'ombe 1970s
Kushoto ni Marehemu Ahmed Abdallah, Mwandishi na Boi Juma Risasi


Hii ilikuwa miaka ya 1970 na sasa tumehamia Mtaa wa Sikukuu na
Narung'ombe na tuna kijichumba cha upenuni tumepewa wala
hatulipi kodi.

Huo mlango hapo kwenye picha ndiyo mlango wa club yetu.

Tunakutana hapo kuna mabenchi tunakaa, kuzungumza na kupiga
soga.

TPmpURBP1F2b42J7yHiz0yqoPRoDfpQonEUA4iwDpNb7_83KqUg-EKQu8ODtwEYz6FHBEfiePWewBszwshKJIDyg4I3zZpRFlNtYZ9L-EEfSuuwYO7PwLb3tSSJ3YzbMtF40V8EvgzcjWMgdng-WHD7ug_WQ0fG1y0LnqRKEZyBWKuc9Q4bWKPA3T60f32AD1BHUQ8exLLAuc1GDHrU0Evk0aPExsjw5IfBKIkRU8CZG57LXozd2BfceihGbFOeVoIFLDeillKLjpMZyATCSopUt8wj0Xkqseg2kco1792aijYNH5IK2xVjMnqVhvOBiINqFk6zI_Mlnjyw0PXijg02X8oSuflast-t6jEELHxPbAMhBIO6TMJHg1KMW88z-pVcXlYuTHpRCQqYX3-7oCqnQig0TLrPoXQ-cGRkKMEUXDzPhXND5qwL2GnLQkJA4VsjMZELClGT8Z-CZ_zkp2CNQO1l5RWkYHmpRBemLh034eRasZBpGEpQ6leTaH8ykUPvpmSzzVxExSt_hjdo11Ulo-noN2W5KUs1CGpa_Wc1sWsbtflQ7E-B0_k0jRyzmm4aFZpBo83p-X1vP6Z5Un3Djvb8W_-b2qKxQJHLu2djkrusc-m22cw=w923-h692-no

Dar es Salaam Saigon Club Mtaa wa Narung'ombe na Livingstone siku ya Khitma

Baadae hii nyumba iliuzwa na tukapewa sasa sehemu nyingine ya club
ambayo ilikuwa katika jengo jipya la kisasa Mtaa wa Narung'ombe na
Livingstone ambako ndipo club ilipo hadi leo.

Uzuri wa Saigon ni kitu kimoja.
Ukifika mara moja basi unakuwa kama vile umelogwa.

Lazima utavutiwa na mazungumzo ya barza na utarudi tena na tena
na mwishowe unakuwa mwanachama.

Kama wewe unapenda kucheka tayarisha mbavu zako vizuri kwani
ikiwa ni ubishi wa Simba na Yanga utavisikia hadi vituko vya 1960
enzi ya Sunderland siku hizo ikiitwa Abidjan na Yanga ikiitwa Kuala
Lumpa.

Washabiki wa timu hizi mbili wanavyopambana na kushambuliana
kama vile hawana akili nzuri.

Lakini hao wote ni wanachama wa Saigon na wengine marafiki wapenzi
ila kwa hili la Simba na Yanga wanakuwa pande mbili tofauti.

Hata Saigon wakifanya shughuli zao ambazo nyingi huambatana na
chakula iwe pilau ya khitma au futari ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
majamvi yatatandikwa na hakuna mgeni anaefukuzwa.

Mtu yeyote atakaa kwenye jamvi na atapewa sahani ya wali au futari
na hakuna atakaemuuliza katokea wapi.

Utamaduni huu wa kufanya karamu kila mwaka ulikuwapo hata Yanga
na Simba ila sijui imekuwaje siku hizi haupo tena.

Red Star walikuwa wakifanya hivi pia kila mwaka lakini kwa sasa club
hii haipo tena baada ya kuuza club yao Mtaa wa Kongo.

Kuhitimisha Saigon si ''open'' chembelecho kuwa ni kwa watu wa Dar
es Salaam tu peke yao.

Yupo Ahmed tena kaoa dada yetu katika ukoo wa Hassan Machakaomo.
Huyu Machakaomo alipata kuwa rais wa Yanga katika miaka ya 1940.

(Baba yake Hassan Machakaomo alikuja Tanganyika na Von Wissman pamoja
na Sykes Mbuwane na wote wakiishi Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Kleist
Sykes
).

Hawa ni Wazulu kutoka Mozambique Imhambane kijiji cha Kwa Likunyi.

Ahmed ni Mmasai na mwanachama wa Saigon wa miaka mingi na kama
nilivyokudokeza katuolea dada yetu.

Yuko Juma Mlonji Mmakonde wa Lindi.
Yuko Shirima Mchagga wa Kilimanjaro.

Mifano iko mingi sana wa jamaa kutoka bara kabisa ambao ni wanachama
na viongozi wa Dar es Salaam Saigon Club.

Sisi hatukufunzwa ubaguzi na wazee wetu.

KsgpSBSs03pzYNE4Im_gKSa1-h-qwikDX0ZhoRpSGRVlEIplLfarQqhpY2iN5B0oXn2g1ku45xaSwzgmi71uryjC74IORdVFR2K0yBxoMiwJWzCk4GEd2CNllcdp7iIaxnzn7PA3jRWOYEDCQ54s63Ld4BiV9VhVtIN3tGIN9Jd70Y8dkeGIMiYsjqPjbTxUihKgoSbfD4NkDJsat7UhcczwHXcwy58l4PMiGuWk1GtpMZHn-_f0wuWyBJNn-hivbkc4G8gWWRbgbCOJHfidB8MC_tkkKiHn3bWWFmTLidmZV1JSLMc_tHhgf2_ijWIsJFq1MaM2RuNcF10Osiu7IVfObO-e0_HxlRcvTsPMginWgtPknpqu2bfPgXGVjdWqZhDqpqnuaGVjLfvivdPbx0U5Ao_SNTQP-uAv9uD_X4EfAVE7hmmxwA8dEN93NT9QPI061qvz6S4HWgESGwFrCfscYOIwzyG4Q0Y0x4wdYAz-0vB5-l9UyCvfKs80DudRshU4oZAYWE0eTBzxLH-0iJicOeei_Hn1vyPWQ3_f-vogljhqomYeGyeERk-MFapILvw-q4vzLEQ-lsNe5u2eMF-wYnn_mRo4WJX1bYWSnQYKZTGG3-QQ=w360-h480-no

Mzee Mshume Kiyate na Mwalimu Nyerere 1964.
Mzee Mshume alijuana na Nyerere 1954 na akamchukua
kama mwanae.


Soma historia ya TANU uone wazee wetu waliwapokea watu gani kutoka
Bara wakawachukua kama ndugu na kuishinao kwa hisani kubwa wengine
ndani ya majumba yao.

Haya yanayopitika Saigon hivi sasa ni urithi kutoka kwa wazee wetu.
 
Hakuna baya lakini kuna baadhi yetu uwa wanakerwa sana unapogusia historia ya TANU na waasisi wake ndio maana nakwambia subiri mapovu
Mumba...
Sasa sisi tufanye nini?
kaja mtu na hisia kuwa Saigon wabaguzi wanataka watu wa Dar es Salaam tu.

Hii si sifa nzuri katika dunia hii tunayoishi.

Mandeala na ANC wangedai uhuru kwa nia ya kuwafukuza Makaburu kwa kuwa
Afrika Kusini si kwao dunia isingewaunga mkono.

Haliadhalika wazee wetu wangeunda TANU na kudai hii ya Waswahili tu hawataki
watu wengine wangejikuta wako peke yao hakuna ambae angewaunga mkono hata
hao Waswahili wa Dar es Salaam wangewapinga.

Leo Saigon imekuwa maarufu na kuwa na nguvu kubwa kwa kuwaleta watu wote
katika umoja bila ya ubaguzi.

Haya sisi tumeiga kutoka kwa wazee wetu kuwa ubaguzi haujengi.
Zuberi Mtemvu kagombana na wenzake kwa kuwakataa Wazungu na Waasia katika
TANU 1958.

TANU ikapata nguvu kwa kuwaleta akina Amir Jamal, Sophia Mustafa, Dereck Bryson,
na Ratansi katika chama.

Unadhani hawa walikuja TANU mikono mitupu?
Walikuja na ''resorces,'' fedha na ujuzi na nchi nzima ikanufaika.

Historia hii ndiyo iliyojenga hata taswira za baaadhi yetu hii leo kwa hiyo ni sehemu ya
maisha yetu.

Ikiwa mtu hapendezewi na historia ya wazee wetu hii ni bahati mbaya.
 
Rage hakosekani pale
Chapa...
Ngoja nikuwekee kisa cha Rage na Kamanda Chico jana kaniletea kijana
mmoja:

''[04/02, 11:47 a.m.] Advocate Saleh Afif: Assalaam alaykum, nimesoma tanzia yako na ya Alhaj Abdallah Tambaza, kuhusu kifo cha mpendwa wetu Mohamed Awadh "Chico".

Wallah kwa kweli mliishi maisha ya kupendana sana, Allah awarehem waliotangulia na awakutanishe Jannah Inshallah.
[04/02, 11:57 a.m.] Advocate Saleh Afif: Nimepata kuhadithiwa na Mzee wangu Mussa Shagow kisa kifuatacho kuhusu Mzee Chico.

" Kipindi ambacho Chico Alikuwa RPC Moshi, Aden Rage alikuwa safarini kutokea Nairobi, akasema apite kidogo Moshi amsalimie Swahiba wake Chico, Aden alimkuta Chico yupo kwenye kikao yapata saa 8 mchana hivi, wakasalimiana vzr na Chico akamuomba Aden kuwa siku hiyo alale Moshi wapate kufurahi pamoja na kupiga soga, kwa bahati mbaya sana Aden akakataa katakata na kusema ana haraka.

Unakijua alichokifanya Chico kwa kuonyesha mahabba yake kwa rafiki yake?

Aden aliondoka na gari yake na alipofika Mwanga alikuta, ''road block,'' traffic wakamzuia na wakamwambia tumepokea amri kutoka kwa RPC tukuzuie, hivyo Aden alishindwa kuendelea na safari hatimae alirudi kwa Chico na wakafurahi pamoja siku nzima"

Hayo ndio yalikuwa mahabba ya Chico kwa jamaa zake, hata kwenye kazi hakuona shida kuunga udugu wake bila kuharibu kazi.

Ahsante.''

0NsWPpykEE6Cz_iQaAXU7GBtpeTmcMDnj68kdp3YzUxnCXHe0Ok_ffyKkxUYbEiwEhLR4YLMcGMYuybOvZwT0xSDtWpbw621G-auDV7vE69AWIOEdHa5LLQlhaSt3QPTXeUDa23mZkfr9frYYNgFBRFkgmeEqfrJ4FX26T_Ne331luHab22XpgwXIwzXvpbcXdDHNtCoJP0nWc8NWKpUHX9HrcdmDP08dr-UoMJjtlNQy6KzEhw1JtElEJHy3llHWIyHw4AH9wf1dttcCdiA-3qW3D-uG5ip6oWMnkYdKmyEdAQ02tvyOPny4uaUGaLF_If8c1h4-Ol7Dr6DV7fv1ihktMDWyfMh_sc8eOFSgx3l6Vv3yL5GjHiewqqnRgM1xLptHsepS8y_a-N3FA6DqYuSIKVAOtO1tQZSawOIWFkA9jQOgPZ-BDBn-ql5RHxGbItQqLNs85-2EgYj0ShPolUStIuzNP2nxTH9wjBVWs5mkRAsOniN_tGm3fV-wq9PUMtXDyvgTljoQ8sVyWK-heYaH0GjSWnU7IXVEAx7WExut-avjho4ThBzlyM_X-_i4sp-qTBddfzNpIs7AQBe3BHxuusOnLYHc8YmOMRdLBqhM4QveaaD=w1038-h692-no

Kulia: Abdallah Tambaza, Mwandishi na Aden Rage na Selemani Pazi Khitma ya Saigon 2012
 
Naam.

Na jirani yangu mwingine wa Udoe kila nikipita Saigon nnakutana nae, Hussein Yanga.
Maalim Faiza,
Hussein jina lile la ''Yanga,'' ni ''nickname,'' tulimpa kwa kuwa wakati
Young Africans club yao iko Sukuma na Mafia alikuwa hapungui hapo.

Unajua sote sisi tulikuwa na ''nicknames,'' na kwa wengine zikaua hata
majina yao halisi kabisa.

Juzi wakati naandika taazia ya Chico nikamtaja Garincha jina lake halisi
silijui kabisa ikabidi niulize na niliyemuuliza akanambia na yeye halijui
lakini usiku akanipigia simu akambia anaitwa Ramadhani Mohamed
Kondo
.

Wote hawa ni marehemu.
Allah awarehemu.

Amin
 
Mumba...
Sasa sisi tufanye nini?
kaja mtu na hisia kuwa Saigon wabaguzi wanataka watu wa Dar es Salaam tu.

Hii si sifa nzuri katika dunia hii tunayoishi.

Mandeala na ANC wangedai uhuru kwa nia ya kuwafukuza Makaburu kwa kuwa
Afrika Kusini si kwao dunia isingewaunga mkono.

Haliadhalika wazee wetu wangeunda TANU na kudai hii ya Waswahili tu hawataki
watu wengine wangejikuta wako peke yao hakuna ambae angewaunga mkono hata
hao Waswahili wa Dar es Salaam wangewapinga.

Leo Saigon imekuwa maarufu na kuwa na nguvu kubwa kwa kuwaleta watu wote
katika umoja bila ya ubaguzi.

Haya sisi tumeiga kutoka kwa wazee wetu kuwa ubaguzi haujengi.
Zuberi Mtemvu kagombana na wenzake kwa kuwakataa Wazungu na Waasia katika
TANU 1958.

TANU ikapata nguvu kwa kuwaleta akina Amir Jamal, Sophia Mustafa, Dereck Bryson,
na Ratansi katika chama.

Unadhani hawa walikuja TANU mikono mitupu?
Walikuja na ''resorces,'' fedha na ujuzi na nchi nzima ikanufaika.

Historia hii ndiyo iliyojenga hata taswira za baaadhi yetu hii leo kwa hiyo ni sehemu ya
maisha yetu.

Ikiwa mtu hapendezewi na historia ya wazee wetu hii ni bahati mbaya.
Umetaja jina Mzee Said LA wahindi Rattansi,yes kuna mtoto ni doctor by professional alikuwa Tumbi hospital anaitwa Noushed Rattansi ni ndugu wa huyo bwana maana naye wanadai alikulia Kariakoo
 
Maalim Faiza,
Hussein jina lile la ''Yanga,'' ni ''nickname,'' tulimpa kwa kuwa wakati
Young Africans club yao iko Sukuma na Mafia alikuwa hapungui hapo.

Unajua sote sisi tulikuwa na ''nicknames,'' na kwa wengine zikaua hata
majina yao halisi kabisa.

Juzi wakati naandika taazia ya Chico nikamtaja Garincha jina lake halisi
silijui kabisa ikabidi niulize na niliyemuuliza akanambia na yeye halijui
lakini usiku akanipigia simu akambia anaitwa Ramadhani Mohamed
Kondo
.

Wote hawa ni marehemu.
Allah awarehemu.

Amin

Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Hussein amefariki?

Kuhusu Chico nilipata habari, Allah amrehemu yeye na aturehem nasi pia.
 
Uwa nafurahi sana kwa simulizi zako,waswahili tunasema kwenye Ukweli Uongo hujitenga,mwenyezi azidi kukujaalia afya njema
Mumba...
Allahuma Amin.
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Hussein amefariki?

Kuhusu Chico nilipata habari, Allah amrehemu yeye na aturehem nasi pia.
Mumba...
Amin.
yawezekani nimeandika sivyo hiyo sentensi.

Hussein yu hai na Allah ampe maisha tawil.

Waliofariki ni Chico na Garincha..
Hussein yuko msikiti wa Manyema vipindi vyote anaswali hapo.

Humkosi.
 
Back
Top Bottom