Ombi kwa Mohammed Said kuhusu Saigon Club

Dah... Ni kweli hii club ilikuwa na uwezo wa kushawishi nani awe nani katika nafasi za Kisiasa katika nchi hii?
Rohombaya,
Watu wanalikweza hili jambo.
Ukweli ni kuwa mwanasiasa yeyote mtaji wake mkubwa ni watu.
Saigon ina wanachama na wapenzi wengi wenye sauti katika jamii
wake kwa waume.

Sasa ukiwapata Saigon kukuunga mkono kwenye jambo lako lolote
uwezekano wa wewe kufanikiwa utakuwa mkubwa.

Angalia mfano huu mdogo.

Saigon ukiwaalika mfano harusi basi wao ndiyo watakuwa waandaaji,
watakuwa walinzi na watafanya kila litakiwalo bure na hata masheikh
wa kusoma maulid watakuwa wao.

Kwa kweli inastaajabisha sana.
Hata ukiwaambia unataka usafiri wanachama wataleta magari yao.

Saigon ni hodari wa kuingiza nguvu mpya katika chama na hii ndiyo
siri ya mafanikio yao.

Wanachama wapya wanakuja na fikra mpya na rasilimali nk.nk.

Sasa hili la kuwa nguzo katika jamii la pia kuwa watumishi wa jamii
ndilo linalofanya Saigon wakikuombea uongozi inakuwa nadra sana
kukosa.

Kuna msemo wa Kiarabu unaosema, "Yule awatumikiae watu ndiyo
bwana wao."

Sasa vipi uagizwe jambo na bwana wako ukatae kulifanya?
 
mzee Mohamed Said,ni ushawishi wa namna gani club ya Saigon ilichangia/inachangia/ktk kuleta mabadiliko ya kiuongozi wa nafasi mbalimbali za kisiasa nchini?
 
Katika watu ambao natamani kukutana nao ni huyu bwana Mohamed Said
Kuna raha unaposikiliza historia ya kweli ( sio zile za kuungwa ungwa za shuleni)
 
Asante,nimeisoma mzee.
Kadoda,
Ahsante watu wanajitisha bure.
Unajua katika hizi kawaida za taasisi kuna mambo wasomi wameyaona.

Taasisi ikiwa kubwa sana inafikia mahali hata wanachama na viongozi
wanakuwa hawajui nini kinafanyika katika taasisi yao.

Nadhani Saigon huko ndiko wanakoelekea.

Watu wanaamini ukitaka kushinda ubunge Kariakoo lazima uwepo
mkono wa Saigon.

Unataka uongozi TFF lazima Saigon watie mkono wao nk. nk.
Huenda upo ukweli katika hayo...
 
Giuseppe,
Karibu sana mie sasa ni mstaafu na uzee ndiyo huu ushapiga hodi.
Mzee anaweza mambo mawili kwa uhakika.

Kulala na kupiga soga.
Kuna kipindi niliwahi comment kwenye mada moja humu kuwa, hazina tulizo nazo kama mzee Mohamed Said ndo zaondoka hivyo kutokana na umri, je mzee mmewekeza kiasi gani kwa kizazi hiki na kijacho kuhusu historia hii ya nchi yetu, historia ambayo haijatiwa chachu?
 
Mlaleo,
Hilo sina hakika ila ninachojua si watu wa kupenda siasa kwa kiwango
cha majadiliano lakini sidhani kama inavunjwa baraza kwa ajili ya siasa.

Nilichokuwa na uhakika nacho ni mazungumzo ya mpira yanapendwa
mno hata kwenye Dar es Salaam Saigon Group mazungumzo mengi ni
ligi ya Uingereza na Simba na Yanga.

Kila watu wana mila yao.
Na wengi ni mashabiki wa Majogoo? Au Sunderland
 
Mzuzuri alikuwa hawapendi watu wa mikoani,usemi wake mkubwa ni wamekuja mjini na gari la jicho mmoja(train)
Ditto alikuwa Mwingi wa habari kuna story kaka yangu alinihadithia juu ya ujanja wake almanusura akamatwe ugoni jamaa aliruka ukuta huko mitaa ya kinondoni apumzike pema
 
Kuna kipindi niliwahi comment kwenye mada moja humu kuwa, hazina tulizo nazo kama mzee Mohamed Said ndo zaondoka hivyo kutokana na umri, je mzee mmewekeza kiasi gani kwa kizazi hiki na kijacho kuhusu historia hii ya nchi yetu, historia ambayo haijatiwa chachu?
Giuseppe,
Ilikuwa dua yangu kuwa Allah anijaalie niandike historia ya TANU.
Allah ameniwezesha Alhamdulilah.

Hili Allah kaiwezesha na nimeandika kitabu cha historia ya uhuru
wa Tanganyika nikipitia katika maisha ya Abdulwahid Sykes na
nilifanya hivi kwa makusudi ili kuondoa ile dhana kuwa TANU
iliundwa na Mwalimu Julius Nyerere dhana ambayo ilikuwa tayari
imeota mizizi katika historia rasmi ya Tanganyika.

Historia hii sasa imeshahifadhika na watu wanaisoma.

Nimefungua blog www.mohammedsaid.com ambamo nimeandika
kila jambo nililoona lina umuhimu katika historia ya nchi yetu.

XtXnkAEKxPs_ty_SPHYF0zxx0p5OZOp1AALQU4SdhX3TX-0oWJtntLl94YB5hP7hJwUXxdUeaqFtVijC7m_4p_AOpCPNXA-kyYFuN6MVruWG_m-1cGDaI_1JjoKPz943DO1SEy_T6X8uJmGrQ-jZ7q7Vhv1z10XxBZy2uexpRTFcFqgbfRmN3sw0KiH3Nw8Qmp-KYCRUtRkwReAh6SDuMak9u_GrHHzWWzhj6Ptcu3G1i7cbCYV9T8WAPmHDXDxr99s1jIJ3MEoCOiVVTKG5BNDvKrEWQXN2fD4qKxAaWNbnqvgpy2y3B4wyY3FT_t1Bw74iN2fG-0wEXeb4yZ9zfJcKFoxu739Cs9BO-kLwaLiXw2v59RCEDmkLhxJRVGgP3L03LALVuNkIzO04ZXB22uAcmYA-q-hV03NLmN9fyZDkgnfDC2ps0W6jimF6k0Qe9PNclMMH_brWNuGtGGY2x_XNautGToi-VXSA6gGAdKBAqScamPh1YSQf5DE-HSpvXjhf-2FsIV548Iv8s6gam-nSO_L_hyoFADbXUxzBs-unfDDi-vxDCYoCL5QlzE1kDezcUjIocOQWbolnUg_eKch0fbqwl9SsJCVYbxxLvpdCeAkFo5bT=w923-h692-no
 
Giuseppe,
Ilikuwa dua yangu kuwa Allah anijaalie niandike historia ya TANU.
Allah ameniwezesha Alhamdulilah.

Hili Allah kaiwezesha na nimeandika kitabu cha historia ya uhuru
wa Tanganyika nikipitia katika maisha ya Abdulwahid Sykes na
nilifanya hivi kwa makusudi ili kuondoa ile dhana kuwa TANU
iliundwa na Mwalimu Julius Nyerere dhana ambayo ilikuwa tayari
imeota mizizi katika historia rasmi ya Tanganyika.

Historia hii sasa imeshaifadhika na watu wanaisoma.

Nimefungua blog www.mohammedsaid.com ambamo nimeandika
kila jambo nililoona lina umuhimu katika historia ya nchi yetu.

XtXnkAEKxPs_ty_SPHYF0zxx0p5OZOp1AALQU4SdhX3TX-0oWJtntLl94YB5hP7hJwUXxdUeaqFtVijC7m_4p_AOpCPNXA-kyYFuN6MVruWG_m-1cGDaI_1JjoKPz943DO1SEy_T6X8uJmGrQ-jZ7q7Vhv1z10XxBZy2uexpRTFcFqgbfRmN3sw0KiH3Nw8Qmp-KYCRUtRkwReAh6SDuMak9u_GrHHzWWzhj6Ptcu3G1i7cbCYV9T8WAPmHDXDxr99s1jIJ3MEoCOiVVTKG5BNDvKrEWQXN2fD4qKxAaWNbnqvgpy2y3B4wyY3FT_t1Bw74iN2fG-0wEXeb4yZ9zfJcKFoxu739Cs9BO-kLwaLiXw2v59RCEDmkLhxJRVGgP3L03LALVuNkIzO04ZXB22uAcmYA-q-hV03NLmN9fyZDkgnfDC2ps0W6jimF6k0Qe9PNclMMH_brWNuGtGGY2x_XNautGToi-VXSA6gGAdKBAqScamPh1YSQf5DE-HSpvXjhf-2FsIV548Iv8s6gam-nSO_L_hyoFADbXUxzBs-unfDDi-vxDCYoCL5QlzE1kDezcUjIocOQWbolnUg_eKch0fbqwl9SsJCVYbxxLvpdCeAkFo5bT=w923-h692-no
Mzee Mohamed hata mimi napenda sana kusoma maandishi yako na ni kweli ni hazina ya Taifa letu hasa katika nyanja ya historia za uhuru ,historia za jij la Dar Es Salaam na wakazi wake,pia nilisoma kuhusu Marehemu mzee Abdu Jumbe,katika yote hayo kwa kuwa sisi ni binaadamu na hakuna mwanaadamu aliye mkamilifu ,mimi nakwazwa na kitu kimoja tu,nadhani umefika Utanzania na utaifa ukauweka mbele zaidi kuliko udini,kwani dini ni mambo ya kibinafsi na nchi yetu haina dini,pia kila mtu ana dini yake,ila tunapozungumzia mambo ya kitaifa basi udini tuuweke pembeni kwani hapo sio mahala pake.Ziaidi ya yote nakushukuru sana kwa michango yako murua na kwa kusimamia kila unachokiamini.
 
Kadoda,
Ahsante watu wanajitisha bure.
Unajua katika hizi kawaida za taasisi kuna mambo wasomi wameyaona.

Taasisi ikiwa kubwa sana inafikia mahali hata wanachama na viongozi
wanakuwa hawajui nini kinafanyika katika taasisi yao.

Nadhani Saigon huko ndiko wanakoelekea.

Watu wanaamini ukitaka kushinda ubunge Kariakoo lazima uwepo
mkono wa Saigon.

Unataka uongozi TFF lazima Saigon watie mkono wao nk. nk.
Huenda upo ukweli katika hayo...
binafsi huwa napenda sana kushiriki mijadala mbalimbali inayoendeshwa ktk vijiwe vya wazee mjini.

miaka ya nyuma nilikuwa addicted na kile kijiwe cha shule ya Uhuru pembezoni mwa kilipo kituo kipya cha mabasi ya UDART.

nikitoka tu ktk shughuli zangu mida ya jioni,breki ya kwanza ilikuwa pale.tatizo la kijiwe,mijadala mingi ilikuwa inahusu dini na siasa kidogo.

nilivutiwa na nidhamu ya wachangia mada.utani wa maneno na ujengaji wa hoja vilikuwa vinaleta Raha sana kusikiliza.

najaribu kuvuta picha burudani waipatayo watu wanaotembelea kijiwe cha saigon.

mnaruhusu vijana wa kikazi hiki cha dijitali kuhudhuria mijadala yenu?
 
Kadoda...
Karibu sana.
Kachukue form uwe mwanachama kabisa.
 
Back
Top Bottom