Ombi kwa mheshimiwa bakhresa

Shedafa

JF-Expert Member
May 21, 2008
802
173
Mheshimiwa,
Mimi kwa niaba ya watanzania wenzako, ninaomba utufanyie msaada wa kuhamisha lango la kuingilia malori yanayopakia/pakua mizigo ktk kiwanda chako cha Bug/Tazara. Uingiaji na utokaji wa malori kiwandani hapo umekuwa kero kwetu watumiaji wengine wa barabara za Nyerere na Mandela, mfano ni leo majira ya saa 5 asubuhi magari katika barabara hizi yalisimama kwa zaidi ya dak 10 yakisubiri lori lililofunga barabara likisubiri kuingia hapo kiwandani.
Madereva wetu wangekuwa wastaarabu hali isingekuwa mbaya kama ilivyo, kwani hawajui kusubiri. Dereva aliyefunga barabara aliona mwenzie amezuiwa kuingia kwa ajili ya taratibu zao hapo getini lakini yeye akaamua kuliingiza lori lake na kuifunga kabisa barabara mpaka aliyezuiwa aliporuhusiwa.
Kwa hiyo chonde chonde mheshimiwa tunaomba, tunajua ukiamua huwezi kushindwa kupata njia mbadala.
 
Yaani pale bakhresa ya buguruni maeneo ya tazara kweli wanakera.
 
Ahamishe ..
Hali ya sasa ya msongamano ni mbaya,
tofauti sana na zamani kiwanda hicho kilipokuwa chini ya national milling.
Seriakali imtafutie huyu pedeshee kiwanja nje ya mji ili kutupunguzia usumbufu.
 
That is a genuine request kuna siku yalinikuta si unajua responcible citizen nikashuka nikamchimba bit dreva kuwa ntamwambia bosi wako na kibarua kitaota nyasi akalisogeza roli eti kisa alikuwa anabishana na mlinzi.nonesense kabisaaaa.bakresa ni muungwana sana tatizo atalipataje ili ombi?
 
Kwa kuwa wanaopita humu ni wengi, naamini ombi litamfikia tu. Ila tuombe limfikie likiwa ni katika dhamira nzuri, si unajua tena taarifa ya kusikia inaweza kuja na maana nyingine kabisa.
 
Kwa kuwa wanaopita humu ni wengi, naamini ombi litamfikia tu. Ila tuombe limfikie likiwa ni katika dhamira nzuri, si unajua tena taarifa ya kusikia inaweza kuja na maana nyingine kabisa.

kwanini usijitume uandike barua umtumie au uende tu pale ofisi yake, mzee ss ni mtu mzuri sana na msikivu huwezi kuamini
 
Nasikia huyu kumwona ngumu, bora unaweza kumwona kirahisi Mzee wa Kilimo Kwanza, maana waswahili wengi sana wanamsumbua kuombaomba unga!
 
Nasikia huyu kumwona ngumu, bora unaweza kumwona kirahisi Mzee wa Kilimo Kwanza, maana waswahili wengi sana wanamsumbua kuombaomba unga!

hapana, you just need to press the right button... kama anataka aniPM nimpe namba ya kupiga
 
hapana, you just need to press the right button... kama anataka aniPM nimpe namba ya kupiga
Kumbe basi wewe unaweza kutusaidia kuufikisha ujumbe, si lazima nikaonane naye au mtu akaonane naye.
 
ntakupa namba, ila pia umeleze wapi unataka ahamishie hiyo turn
Nitashukuru mkuu, kama kweli huyu ni mtu mwenye huruma huenda akaihurumia jamii. Tukitaka serikali ichukue jukumu lake la kupafanyia matengenezo ya kitaalamu tutakuwa kama tunampigia mbuzi gitaa. Bora wewe nipe # halafu mimi ntajaribu kumpigia, akiliona la maana itakuwa kheri, ikiliona la kipuuzi ujumbe utakuwa umemfikia.
 
Back
Top Bottom