Ombi kwa CHADEMA; Iweke utaratibu mzuri wa kukusanya na kutangaza matokeo

muheza2007

JF-Expert Member
Mar 19, 2010
483
771
Tunakuomba sana katibu mkuu Mnyika. Tengenezeni utaratibu mzuri wa kukusanya na kutangaza matokeo.

Ile timu yetu iliyovamiwa mwaka 2015, tusifanye makosa hayo. Safari hii hiyo timu iwe nje ya nchi na ziwe timu zaidi ya mbili.

Vijana wapewe bundle. Matokeo yakitoka wanapiga picha na kutuma hapo hapo.
Wakusanya matokeo wana hesabu na Kisha kuyaweka online ili kila mtu ayaone.

Wakijifanya kuchelewesha matokeo wananchi wanayaona matokeo ya kweli mtandaoni.

Huo ndio ujanja aliwafanyia Hamad kule Zanzibar, wakashindwa kuiba ikabidi wafute uchaguzi mzima.

Msiruhusu kituo cha kuhesabu kikawa TZ. Tutavamiwa tena na hawa majambazi wa Ccm.
 
Wazo zuri, kwasababu CCM wao huwa na kituo/ vituo vyao, kina January Makamba 2015 ndio ilikuwa kazi yao, sasa Chadema itabidi mwaka huu wajipange vizuri, wahakikishe hicho kituo kitakuwepo mahala salama zaidi ambapo hapataweza kuingiliwa kwa namna yoyote na mtu au taasisi yoyote. Hili litasaidia sana kuepusha kuibiwa kura.
 
Hata Mimi nilishangaa kuona tukio nyeti kama lile tunawekwa kwenye Hotel hapa Dsm.haikuwa poa. Pia kuhusu watu watakaoenda kufanya hiyo kazi isiwe kama ile ya 2015.

Ambayo hata mtu humjui kama no Kamanda kisa tu amekuja na Lowasa Basi twende.Watafutwe Chaso wale wavyuo ili Wakae hata makundi 10, likikamatwa kundi hili Basi kundi lile linaendelea na kazi. Pia ni kheri wangefanyia kazi nje ya nchi Kama alivyosema mdau. Au huko Tunduru vijijini.

Hata hivyo Ccm nao Wana Communications center itakayokuwa inafanya kazi ya kuhesabu na kuhakiki kura zao. Hakuna ubaya safari hii.
 
Kafanye kimya kimya kama alivyofanya maalim Seif, wakitangaza tu kitatokea kilichomkuta Lowasa na wachina wake
 
CCM wao wanaruhusiwa. Dawa ya hawa watu ni kutangaza matokeo yetu mapema ili kama tukishinda tujiandae kwenda barabarani.

Hii tume ya Ccm haiwezi kutupa ushindi. Lazima tuutafute wenyewe.

Matokeo Yetu yawe wazi kabisa. Kika mtu awe na uwezo wa kuhakiki matokeo yetu na ya kituoni kwake ili kujenga credibility.

Baada ya hapo tukishinda hawataweza kutuzuia barabarani.
Hata Mimi nilishangaa kuona tukio nyeti kama lile tunawekwa kwenye Hotel hapa Dsm.haikuwa poa. Pia kuhusu watu watakaoenda kufanya hiyo kazi isiwe kama ile ya 2015. Ambayo hata mtu humjui kama no Kamanda kisa tu amekuja na Lowasa Basi twende.Watafutwe Chaso wale wavyuo ili Wakae hata makundi 10, likikamatwa kundi hili Basi kundi lile linaendelea na kazi.Pia ni kheri wangefanyia kazi nje ya nchi Kama alivyosema mdau. Au huko Tunduru vijijini.

Hata hivyo Ccm nao Wana Communications center itakayokuwa inafanya kazi ya kuhesabu na kuhakiki kura zao. Hakuna ubaya safari hii.
 
n sahihi sana lkn ata ivo ninawasiwasi juu ya kuzimwa kwa mitandao yote, Maana wanajua sie hatuna redio wala tv, ivo wakifunga mawasiliano tu, hatutaweza kupeana taharifa wala kumsikia Lissu wetu
 
Back
Top Bottom