Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,463
- 113,537
Wanabodi,
Jumamosi ya kesho ndio siku ya uchaguzi wa marudio majimbo ya Kinondoni na Siha, japo kuna vyama vingi vinavyoshiriki uchaguzi huu, lakini ukweli ni kwamba, washindani wawili wakuu ni Chadema iliyokuwa ikiyashikilia chini ya mwamvuli wa Ukawa, na CCM, inayotaka kumpokonya mtu tonge mdomoni.
Hili ni bandiko la wito kwa mafahali wawili hawa, kukubali matokeo kwa sababu, asiyekubali kushindwa sii mshindani!.
Kwa Nini Matokeo ya Uchaguzi wa Kinondoni na Siha ni Muhimu Sana kwa Chadema?.
Uchaguzi huu ni muhimu sana kuutumia kama kipimo cha awali cha matokeo ya jumla ya uchaguzi wa 2020. Chadema ikishindwa kuyatetea majimbo haya mawili tuu kwa sasa, then haitaweza kuyatetea majimbo yake yote 2020, hivyo matokeo haya yatatuma ujumbe mzito kwa wabunge wote wa upinzani waliopo bungeni ndani ya bunge hili, kuwa kama bado wanataka kuendelea kuwa wabunge bunge lijalo, the nao ni lazima wajiunge CCM, wasimamishwe kupitia CCM ndipo watarudi bungeni!. Ombi langu kwa watu wa aina hii, nawaomba tuu kwa sasa wawe wavumilivu, wasijitoe, kwa kuwahurumia masikini wa Tanzania, kuingia gharama za uchaguzi wa marudio, wasubirie tuu hadi 2020 bunge litakapovunjwa, waende salama.
Kwa Nini Matokeo ya Uchaguzi Huu ni Muhimu Sana Kwa CCM ndio Maana CCM Wanatumia Nguvu Kubwa Sana?.
Kwa vile CCM wanakijua walichokifanya hadi wabunge hawa kuachia ubunge wao na kuhamia CCM, hivyo ili kuhalalisha kuwa CCM inapendwa sana na inakubalika sana kwa wapiga kura, kuweza kuwanunua wabunge na madiwani wa upinzani kwa bei rahisi tuu na kuwapokonya majimbo yao, hivyo watatumia mbinu hizo hizo kuwapendesha wapiga kura, ndio maana CCM inatumia nguvu kubwa sana na line-up nzito ya heavy guards wake akiwemo mkuu wa mhimili wa Bunge. Kwenye hili la heavy guards, lazima niipongeze CCM kwa reservations za ile top brass yake, hivyo huu ni uugwana mkubwa!. Maana ile top brass ingetia timu, sijui Chadema wangeambulia nini?!. Thanks to CCM for this!.
Mshindi wa Matokeo ya Kinondoni na Siha, ni Uthibitisho Ushindi wa Usaliti, Ulaghai, Rushwa, Dhulma, Ubatili, Ufisadi na Ubadhilifu, Dhidi ya Haki, Ukweli, Uadilifu na Uzalendo.
Hakuna asiyejua kinachofanyika behind the closed doors hadi wabunge na madiwani kuhamia CCM. Hii ni vita kati ya usaliti na uzalendo, ni vita kati ya ulaghai na ukweli, ni vita kati ya rushwa na uadilifu, ni vita kati ya dhulma na haki, no vita kati ya ufisadi, ubadhirifu, na matumizi mabaya ya fedha za umma dhidi ya ukereketwa wa kweli wa umasikini wa nchi hii na rasilimali zake. Upande wowote utakaoshinda, ni kielelezo cha hivi ndivyo Watanzania tulivyo!.
Ruswa: Wahamaji ni Wasaliti na Walarushwa, Wamehongwa!. Na Huu ni Uthibitisho!.
Mtu ukiishachaguliwa diwani au mbunge, unabeba dhamana ya wananchi wa eneo husika, kujiuzulu ni usaliti kwa watu hao. Sasa msaliti anaporudi tena kuomba nafasi ile ile aliyoisaliti, akichaguliwa tena, kunatuma ujumbe mzito type ya wapiga kura wetu!
Japo tulionyeshwa ule ushahidi wa rushwa ya wazi wazi kwenye zile video za Nasari, japo zimekataliwa ila wenye macho tumeona!.
Hii inatuma ujumbe mzito kuhusu hili lidudu linaloitwa PCCB, nalo ni shina tuu la CCM!.
Ushahidi wangu wa rushwa ni huu. Utaratibu wa kujiunga na CCM unafahamika, utaratibu wa mtu kugombea ubunge ndani ya CCM, unafahamika ni mchakato fulani. Sasa mtu anajiunga leo CCM, kesho anateuliwa mgombea bila utaratibu na mchakato kufuatwa. Huu ni uthibitisho wa rushwa ya ahadi, kisheria inaitwa "promissory estoppel" ambayo ni ushahidi usiotia shaka mtu alihongwa ahadi ya kusimamishwa yeye kama atajitoa!. Ndicho kilichofanyika Kinondoni na Siha, na kitaendelea!. Rushwa sio lazima iwe ni pesa tuu!, hata ahadi ya uteuzi ni rushwa!, halafu hili lidudu li PCCB lipo tuu, na mijitu imejazana ofisini inakula tuu kiyoyozi, eti tunapiga vita rushwa!.
Uchaguzi wa Kinondoni na Siha ni Ufisadi na Ubadhirifu Wenye Uhalali wa Kisheria Kwa Jina la Demokrasia!.
Ukizisikia gharama za chaguzi hizi za kujitakia, utakubaliana na mimi kuwa huu ni ubadhirifu na ufisadi wa kujitakia. Haiwezekani nchi masikini kama Tanzania, to spend such amounts kwa jambo la kujitakia kama hili. Hizi ndio akili zetu sisi Watanzania!.
Wito Kwa Main Players, Chadema na CCM, Fuateni Sheria, Taratibu na Kanuni za NEC.
Huu ni wito kwa hawa two main players, hakikisheni kesho mnazingatia sheria, taratibu na kanuni. Watanzania ni wapenda amani. Tunataka uchaguzi wa amani. Kama kuna kitu hakiendi sawa, fuateni taratibu, jazeni fomu za malalamiko sio kulalamikia kwenye media pekee!.
Wito Kwa Refa, NEC, Japo Uwanja Hauka Sawa, Tendeni Haki na Haki Ionekane imetendeka!.
Kwenye hili la NEC, naomba ku declare my interest kuwa naifahamu vizuri NEC, ni Tume Huru, na pia nimetokea kumfahamu Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima ni mtu mwenye impeccable integrity kuendesha uchaguzi huru na wa haki. Hapa NEC yeye ni refa tuu, sie yeye aliyetengeneza uwanja wa mechi, wala aliyepanga timu, yeye kazi ni kuchezesha tuu hii mechi. Ombi kwa refa wetu NEC kuwa japo uwanja wetu ni mshazari na umekaa tenge kwa kuegemea upande mmoja, tunamuomba aichezeshe mechi hii ngumu kwa haki, na haki hiyo ionekane imetendeka, ili atakayeshinda, ashinde kwa haki, na atakayeshindwa, ashindwe kwa haki, watu wayakubali matokeo na maisha yaendelee.
Mwito Kwa Wana Kinondoni na Wana Siha, Uchaguzi ni Wenu, Hatuwachagulii, na Tutaheshimu Chaguo Lenu!.
Uchaguzi ni kwa Wana Kinondoni na Wana Siha, tumieni haki yenu kuwachagua viongozi mnaowataka. Sisi wengine tumewafanyia kazi ya uelimishaji umma kwa kuamini baadhi yenu hamjui mnatakiwa kuchagua kiasi kwamba mnaweza kuletewa ujinga na mkauchagua ujinga huo kwa kutojua kuwa mmeletewa ujinga. Lakini baada ya kuelimishwa kuwa hiki ni kitu kizuri, na huu ni ujinga, mkiamua kuchagua kitu kizuri mko huru ni chaguo lenu, ila hata mkiamua kuchagua ujinga kuwa ndio chaguo lenu, sisi wengine wote tutaheshimu chaguo lenu kwa ile ile kanuni ya
"Choose your love, and love your choice", anayekijua kitanda ni anayekilala ndie ajua kunguni wake.
The choice is yours.
All the best!
Paskali