Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
KUTHIBITISWA KWA KATIBU MKUU MPYA WA CHADEMA,USIKAE PEMBENI NA KUANGALIA(DON'T SIT ASIDE AND LOOK)
Na Kwilasa E
Nichukue nafasi hii tena kumpongeza katibu mkuu wa Chadema, Dr Vicent Biyegele Mashinji kwa kupendekezwa jina lake kisha Baraza kuu la Chadema kumthibitisha kwa kumpigia kura, aidha pongezi nyingi pia zimuendee kaka Mkubwa, kamanda wa anga, mtaalam wa kubadili gear angani Hon Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama Taifa kwa umakini mkubwa kupendekeza jina bora tena nje ya wale bora wengine tuliowatarajia na tuliokuwa tunashindana kubashiri.
Kiukweli Mwenyekiti wa Chadema taifa anastahili sifa ya kipekee sana, lakini pia hata alioshirikiana nao, alioshauriana nao wanastahili pongezi.
Makala hii si kwa ajili ya pongezi bali ni kutoa Rai kwa wanachadema wote, viongozi na wasio viongozi na wapenda mabadiliko wasio wanachama kwamba tusikae pembeni na kuangalia (don't sit aside and look) kwamba tuone sasa, si msomi, tuone atafanya nini, au katibu yupo, ni kijana msomi, hivyo chama atakijenga na kitaimarika tu.
Tukifanya hivyo litakuwa ni kosa la jinai, maana Dr Mashinji ,yeye ni mmoja tu katika taasisi, hivyo ili tunufaike na uongozi wake ni lazima tushirikiane, tushiriki katika ujenzi wa chama, maana chama hiki sasa kiko nchi nzima, hawezi kuwepo kila mahali kila muda ili atekeleze shughuli za ujenzi wa chama, ni lazima viongozi wa ngazi zote na wanachama na wapenda mabadiliko tumuunge mkono, tushiriki katika ujenzi wa chama.
Nitachambua kwa uchache mambo ambayo natarajia Dr Vicent Mshinji ataanza nayo kama mtendaji mkuu wa Chadema, nasi tutaungana nae katika utekelezaji.
1:Kukusanya taarifa (takwimu ) za awali (Collection of Baseline data)
Hili ni jambo nilishawahi kulijadili, labda si vibaya kuweka msisitizo kwamba, taarifa hizi ni za awali hukusanywa kabla ya kuanza kazi au shughuli, takwimu hizi husaidia kuweka malengo, kukadiria mabadiliko, kulinganisha hali na mabadiliko ya matokeo ya utekelezaji, pia huwa ni zana(tool) ya kukufanya ujue uko wapi kwa sasa na unataka kwenda wapi.
Natarajia takwimu za idadi ya viongozi wa chama na Mabaraza yake, rasilimali za chama, wawakilishi ktk vyombo vya maamuzi,Mafunzo kwa viongozi (Capacity building training) kutaja kwa uchache zitakusanywa, Natarajia ukaguzi wa kiutawala (Administrative Audit ) utafanyika haraka sana ili kuweza kujua mapungufu ya kiutawala ambapo kwa sehemu kubwa yanaifanya taasisi itekeleze majukumu yake.
2:Migogoro ndani ya chama
Natarajia Katibu mkuu mpya atajipanga haraka kuanza kushughulikia migogoro ndani ya chama, nadhani kazi hii itakuwa rahisi maana hatua ya kwanza ya Conflict Management ni kulitambua tatizo, kukubali kwamba tatizo lipo,Mwenyekiti taifa juzi amekiri kuwepo kwa migogoro ndani ya chama, hivyo tayari jambo hili limeshaanza kushugulikiwa.
Aidha natarajia focus itakuwa katika kumaliza au kupunguza vyanzo vya migogoro, ikiwemo rushwa, kutokuwajibika, uzembe na ubinafsi.
3:Kupanga safu bora ya watumishi na viongozi walio chini ya ofisi yake kiutendaji.
Wataalamu wa mambo ya ujenzi wanapotaka kuanza kazi katika mradi, kwanza jambo la kwanza huwa ni kufanya Site mobilization, baada ya hapo wanafanya Site Clearance.
Vivyo hivyo katibu mkuu ataanza kwa kufanya site mobilization ambayo itakuwa ni collection of Baseline data na kisha akiingia kwenye hatua ya kusafisha eneo la ujenzi (Site Clearance) kwa kuhakikisha anawaondoa wote wazembe, wapiga dili, wala rushwa, wabinafsi,ili site anayoenda kujenga iwe safi. ...
Kuna tuhuma nyingi za rushwa, hasa kipindi cha uchaguzi mkuu, rushwa ya fedha na ngono, kuna tuhuma kwa watu walioko chini ya ofisi ya katibu mkuu makao makuu, kanda na wilayani, hili si jambo la kuchekea si jambo la kulilinda kwa kisingizio chochote, ni jambo la hatari, Natarajia Katibu mkuu hatakuwa na mzaha na jambo hili. .
Ni matarajio ya wengi kwamba hili hatamuogopa mtu wala kumstahi mtu eti kwa kuwa anamjua, anajuana na mkubwa fulani, ni rafiki au ni anajulikana sana.
Suala la rushwa ndani ya chama linaua pia demokrasia ndani ya chama, lakini linaua moyo wa kujitolea (spoil the spirit of volunteerism),ni matarajio ya wanachadema wengi kwamba Dr Mshinji atalishugulikia hili perpendicular, maana tuhuma nyingi ziko wazi na watuhumiwa wapo na yamkini watu watakuwa na ushahidi, lakini hata pale ushahidi wa moja kwa moja utakosekana,basi mamlaka zao za kinidhamu watumie Circumstantial Evidence kuwawajibisha.
Asipofanya Site Clearance itakuwa ngumu kujenga nyumba (kujenga chama), ni ukweli wa kitaaluma ya ujenzi kwamba huwezi kuanza kujenga nyumba (walling) kabla ya kujenga msingi, na huwezi kujenga msingi wa nyumba kabla hujachimba msingi (trench excavation) na ukamwaga zege la chini (strip footing au bedding)na huwezi kuchimba msingi kabla hujafanya usafi, hujaondoa yasiyo hitajika kwenye site (Site Clearance) Lakini pia huwezi kufanya site clearance kabla hujafanya site mobilization, na kwa falsafa hii Site Mobilization ni kufanya Baseline data Collection. Hata hivyo huwezi kufanya site mobilization kama hujapewa tenda, na ukakubaliwa. ...hapa Mwenyekiti alimuona kitambo akamshort list, muda umefika amempendekeza na Baraza kuu limempitisha, na kwa maana hiyo amepewa tenda ya kusimamia ujenzi wa Chadema,
Dr Vicent apewe ushirikiano naamini atafanya, atatekeleza, ataijenga chadema kwa ushirikiano wetu pamoja.
4:Mpango Mkakati (Strategic plan)
Katibu mkuu atakuwa msimamizi mkuu wa utekelezaji wa mpango mkakati ambao pia Baraza kuu limeujadili na kuupitisha, mpango huu utakuwa na mpango kazi ambao utakuwa na mambo muhimu yaliyoanishwa, mojawapo ya mambo yanayotarajiwa kuwamo ni;
●Matokeo ya awali ya mpango kazi
●Shughuli/Kazi za kufanya kwa muda uliopangwa
●Kiwango cha utekelezaji (kwa kila shughuli/kazi/activities kwa kuonyesha idadi ya walengwa, idadi ya kata wilaya, mafunzo nk)
●Njia za kuthibitisha kuwa kila shuguli iliyopangwa imefanyika
●Muda wa utekelezaji kwa kila shughuli.
●Gharama za kila shughuli
●Nani muhusika na utekelezaji wa shughuli husika.
Tukimpa ushirikiano Dr Mshinji, kwa kutumia structure ya chama haya tunayotarajia yatatekelezeka na wote tutakijenga chama na wala si kukaa pembeni na kuangalia.
5:Mpango wa Utekelezaji
Natarajia ukisoma jedwali la utekelezaji wa mpango kazi wa chama uliopitishwa na Baraza kuu nitakutana na mambo kadhaa ya muhimu yanayoelekeza namna ya utekelezaji, ambao mfumo mzima wa viongozi, hasa watendaji watausimamia, mambo hayo ni pamoja na;
●Mabadiliko tunayoyatarajia yatokee ktk utekelezaji wa mpango
●Kiashira (Indicators) gani tumejiwekea kuonyesha mabadiliko tarajiwa?
●Taarifa za awali (baseline data) zinasemaje? Hali ikoje kwa sasa, mfano# wanachama, # Viongozi#ofisi# matawi# misingi# mafunzo ya uongozi nk
●Shabaha/Kiwango cha mabadiliko tunachotarajia kukifikia baada ya utekelezaji wa mpango.
●Tutayapimaje mabadiliko (njia au mbinu za kupima mabadiliko)
●Taarifa ya utekelezaji itakusanywa kila baada ya muda gani(Monitoring)
●Nani muhusika wa ufuatiliaji?
Yote hayo hayawezi kutekelezeka nchi nchi nzima huku Dr Mashinji peke yake akiwa mtekelezaji ni lazima structure ya uongozi iwepo na isimamie hayo kwa maelekezo na msimamizi mkuu wa utendaji ambae ni katibu mkuu, ndio maana nasema tena tusikae pembeni na kuangalia.
6:Kuboresha Usimamizi wa Rasilimali Fedha na Vifaa
Ni matazamio ya wanachama wengi kwamba ujio wa Dr Vicent utakwenda sambamba na mabadiliko makubwa ya mfumo wa kusimamia rasilimali za chama.
Minong'ono ipo tena ipo mingi na hata mifano ya kuthibisha manung'uniko hayo ni mingi kuanzia ngazi za matawi hadi Taifa.
Natarajia suala la Financial management litapewa kipaumbele Sana ktk kufanya maboresho ktk uwazi (Transparency),utoaji wa mrejesho (Financial accountability), matumizi ya vitabu vya mahesabu, hasa ngazi za matawi, kata wilaya mkoa na kanda.
Mara nyingi wadau wamekuwa wakichangia chama, lakini mrejesho hakuna juu ya zilizopatikana, na zilizotumika na ngapi zimebaki, lakini pia ukusanyaji wa mapato bila kutoa official receipt, ofisi nyingi hawana vitabu vya risiti ambazo vitabu vyake vimetengenezwa kwa idhini ya mamlaka, na vikasajiliwa kwenye Rejesta ya mali za chama kwa ngazi husika na kisha kutolewa kwa maandishi kwa ajili ya kutumika, hakuna account za ofisi au ngazi mbali mbali, hakuna vitabu wala taarifa za fedha, hakuna mrejesho kwa wadau, hakuna utaratibu wa kufanya changizo na mwisho inakuwa mzigo kwa wadau , sijawahi kuiona Financial manual, haya yote natarajia yatarekebishwa kwa ngazi zote.
Ni kosa kubwa kudhani kuwa fedha zinazotakiwa kufanyiwa accountability ni zile za Ruzuku tu, fedha zote zinazopatikana kutoka vyanzo halali vya mapato inatakiwa kufanyiwa accountability, hili limekuwa sugu kwenye ngazi za matawi, kata, Wilaya na hata Kanda.
Naamini tumepata katibu mkuu ambae atawezesha ushirikishwaji wa wanachama kwenye kutoa na kupokea huduma za chama (Facilitate Party Members Engagement) kupitia vikao, mikutano na taarifa kwenye vyombo vya habari.
6:Natarajia Tukimpa ushirikiano Dr Vicent Mashinji atasimamia vema utekelezaji wa mambo ya kimkakati ya chama (Strategic Party Issues), ikiwemo;
●Namna ya kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano ya ndani na nje ya chama(how to design, set up and implement internal and external communication strategy)
●Namna ya kupanua mtandao wa mashirikano ya kimataifa na kuongeza kutambulika kwa chama kimataifa (How to expand our International network and Increase international recognition)
●Namna ya kufanya ufuatiliaji na Tathimini (How to carry out Monitoring and Evaluation) Hili lilijitokeza sana wakati wa Chadema ni msingi na ndio chanzo cha utekelezaji hafifu wa project hiyo.
●Namna ya kuboresha usajili/utafutaji wa wanachama wapya, wagombea wa ubunge na viti maalum (How to improve members recruitment, member of parliamentary candidates and special seats.
Nk
Kuna mambo mengi kimsingi ambayo tunatarajia katibu mkuu ayasimamie katika hatua ya utekelezaji, lakini ili yatendeke na tuyaone ni vema kila mmoja wetu akatimiza wajibu wake, ni kila mmoja wetu akifikirie atafanya nini, atashiriki vipi ili ujenzi huo wa chama ufanyike kama timu moja kwa pamoja na wala si kukaa pembeni na kuangalia atafanya nini
Don't sit aside and look
Kwilasa E
14/3/2016