Ombi: Jiji la Dar es Salaam lishushwe hadhi

guzman_

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,277
Reaction score
2,443
Kwa takribani miaka mi3 nilikuwa sijafika posta na kariakoo. Jambo la kustaajabu nilichoshuhudia siamini kabisa. Ni kwamba hii serikali imeruhusu machinga kiwango hicho kilichopo. Yaani machinga wamepanga bidhaa hata sehemu ya kutembea hamna mpaka kwenye space zile katikati ya barabara za mwendokasi. Si karume, si kariakoo, si posta, si ubungo, si Mbagala.

Inshort hakuna utofauti wa mbagala na Kariakoo. Machinga wamefurika huko hata ile hadhi ya jiji sasa haipo na kwa taarifa za mnyetishaji wangu hawa jamaa wameizidi nguvu serikali na hata serikali inawagwaya kulinda kura za 2020. Hivi hakuna wataalamu wanaoelewa effects za informal sector kwenye uchumi kweli?

Wenzetu wanatafuta njia za kutoa informal sector sisi ndo tunaimwagia mafuta ipambe moto. Kilio walicho nacho wafanya biashara wenye milango yao kariakoo nadhani ni kikubwa sana. Kariakoo ni centre of business kwa nchi jirani Zambia, Malawi, Kongo, Burundi, Rwanda ila sasa sidhani kama inahadhi hio ya kuwa center ya biashara.

Hili jiji sasa lishushwe hadhi tu ieleweke.
 
Jiji limekuwa na vibanda kama kibera, uzuri wa jiji umemezwa ma machinga jiji zima, barabara yote ya mwendo kasi ni mavibanda ya mbao yameezekwa kwa maturubai kama kambi za wakimbizi kisa kura chaguzi kwa maslahi ya kina bashite, aibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani tuko wengi tusiolipokea hili jambo ni kweli wanatafuta hela ila si kwa staili hii. Jiji limekuwa la hovyo sana.
 
Tatizo hawa wanaopika na kusambaza ugonjwa wa ini, itafika wakati cancer za ini zitatupata wengi.
 
Nilikuwa naumia sana kwa hali hii ila baadaye nilituliza nafsi ila wadau hali hii ni special program ya muda mfupi tu tena kisiasa.
 
Kuna tatizo la ajira nchini lazima watu wajiajiri kwa biashara hizo. Pia ipo siku hao unaoona "wamefurika" jijini biashara zao zitakuwa na kuajiri hata wewe, mtoto wako au hata mjukuu wako. Riziki apangaye ni Mungu.
 
Kuna kitu kinaitwa cost-benefit comparison, naweza kukuhakikishia kuwa by all metrics the cost of machinga program au wajasiliamali (by whatever name you can call it) is far higher than its expected benefit. Loss tu wanayopata kwenye kodi inaweza ipita faida yake achilia mbali adha wanazosababisha hao jamaa.
 
Je mfumo wa kodi wa Tanzania unaona ni sahihi?
 
Huko ni mada nyingine. Mfanyakazi analipa 500,000 kodi kwa mwezi (6m kwa mwaka) mshahara 2m kwa mwezi. Mfanya biashara anayepata faida ya 5m kwa mwezi analipa 2m kodi kwa mwaka. Machinga nao wanalipa 20,000 mwaka mzima na wanamaduka nje ya utaratibu.
 
Nataka kukufahamisha jambo moja. Unazungumza kwa kuwa hujawahi kufanya biashara na unazungumza kama unapata faida ya kimasihara tu, na kodi ya TRA inalipwa kimasihara tu. Mkuu biashara hapa Tanzania kuna vimashine vya TRA vya risiti vile vimashine ni hatari kwa biashara. Makadirio ya kodi kwa mauzo ghafi wakikukadiria TRA unaweza ukaishiwa nguvu. Halafu bado kuna service levy hapo za halmashauri. Bado wafanyakazi hawajaiba kidogokidogo. Mishahara ya wafanyakazi. Na wewe kama mfanyabiashara ule na ulishe familia yako. Gharama za sehemu unayofanyia biashara. Marejesho ya benki pamoja na saccoss. Bado hujaanza kupanua mtaji na kuongeza mzigo kwenye biashara pamoja na usumbufu wa tozo mbalimbali. Na bado pamoja na juhudi zote na gharama zote watu fedha mifukoni hawana yaani unajikalia kwenye biashara yako unaangaliana na bidhaa zako.

Ni bora ujikatie 20000 za vijana 10 wauze mzigo waumalize.

Shukuru Mungu kwa ulipo ila usiwaone wengine kwamba hawako sahihi.

Maneno ya faida 5m ni kwa watu wenye mtaji mkubwa na connection kubwa. Na maneno ya motivation speakers tu.
 
BBC hua wanaiita Dar ni KIJIJI KIKUBWA CHA WAVUVI.

dodge
 
Kumbe wale tunadhani machinga wamejiajiri, wafanyabiashara genious sana I love this group

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom