Ombi: Ikulu ipuuze waraka wa Kakobe

Ombi: Ikulu ipuuze waraka wa Kakobe

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,829
WanaJF,

UZEMBE NI WA NANI MPAKA PCT IMEKOSA MWAKILISHI BUNGE LA KATIBA?

Ndugu zangu, hili suala limeshatolewa ufafanuzi na Ikulu na Watanzania wakaridhika maana kabla ya ufafanuzi Watanzania walikuwa wame-panic kuwa PCT imeonewa na kudhurumiwa haki yao ya kushiriki kuandaa katiba.

Ufafanuzi ulisema kwamba, baraza la maaskofu alikufuata maelekezo ya sheria katika kuwasilisha mapendekezo yao ya wawakilishi.

Jambo ambalo PCT walikosea ni kujipendekeza kama watu binafsi badala ya kuwa kwenye makundi kama ambavyo sheria ilielekeza. Hivyo serikali haikuwa na budi bali kupiga majina ya PCT kapuni na kupelekea wapentekosti kukosa mwakilishi.

Hivyo hapa mtajionea kuwa kosa lilikuwa la PCT na sio serikali.

KUANDIKWA KWA WARAKA IKULU:

Baada ya maelezo ya serikali kutolewa, baraza la maaskofu liliridhia kuwa wao ndio hawakufuata maelekezo ya sheria hivyo kukiri kuwa walikosea pia walitoa taarifa kwa umma kuwa wameelewana na serikali kuhusu sakata lao.

Lakini ghafla Watanzania tumeshangazwa na Kakobe ambae amejitokeza na kumuandika mhe. Rais ujumbe uliojaa vitisho na mambo mengi ya kusadikika.

Kusema ukweli hili ni jambo la ajabu, sijui Kakobe kakurupuka au vipi, maana kuhusu Pentekosti kukosa mwakilishi tayari Ikulu imelimaliza na aliyefanya kosa la kukosekana kwa mwakilishi wao kwenye bunge ni hao PCT wenyewe.

Sasa Kakobe tatizo lake hapa ni nini!? Nini ambacho hajakielewa katika ufafanuzi wa kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kuhusu hili suala!?

Nitoe angalizo kwa Kakobe: kama Kakobe alitaka arudishe umaarufu wake uliotoweka kupitia huu waraka, basi amepotoka big time.

Watanzania sio wajinga kama ambavyo Kakobe anadhani. Kama Kakobe alifanikiwa kudanganya baadhi ya Watanzania na kuweza kujitajirisha, basi asidhani kama ataweza kutudanganya Watanzania wote.
 
Mambo ya kusadikika ngoja mukutane na nguvu kubwa neno la mutumishi wa Mungu ni sheria. Eliya alishusha moto ukalamba maelfu. Mumuangukie mutumishi wa Mungu awaombee rehema kwa Mungu la sivyo mutamujua Mungu wake yule afukuzaye pepo wachafu wawatoke watu. Itakula kwenu soon. Nawahurumia.Teh teh teh!.
 
Waraka aandikiwe KIKWETE kulia ulie wewe majanga

Kweli wewe ni uneducated. Hivi Kikwete ni nani kwetu!? Hujui kuwa ni rais wetu sote? Sasa kweli maamuzi yake anayo yafanya huoni kama yana muathiri kila mwananchi?

Kama ungefanikiwa ku-attend vipindi vichache vya civics ya kidato cha pili usinge andika hizo pumba hapo. Ila sikulaumu, cha msingi urudi shule ukaondoe ujinga mkuu.
 
Kakobe amemwambia kuwa CCM inakufa , sasa akipuuza kuomba rehema za Mola si yatatimia hayo? Sasa unataka nini kupuuzwa ?
 
Mambo ya kusadikika ngoja mukutane na nguvu kubwa neno la mutumishi wa Mungu ni sheria. Eliya alishusha moto ukalamba maelfu. Mumuangukie mutumishi wa Mungu awaombee rehema kwa Mungu la sivyo mutamujua Mungu wake yule afukuzaye pepo wachafu wawatoke watu. Itakula kwenu soon. Nawahurumia.Teh teh teh!.

No offence, but to me Kakobe is a cone man. Namuona tapeli kama walivyo matapeli wengine.

Kwanza heshima yangu kwake niliipoteza tangu alivyo kimbia ile ishu ya TANESCO. Yani nilikuwa napita nakuta walaghaika wake wakikesha eti kuomba umeme usipite. Yani kuna watu wajinga hapa duniani.

Hivi sasa kote kumewekwa nguzo na mradi wa TANESCO umesonga mbele huku Kakobe akiambulia aibu na kukimbiwa na waumini wake.
 
ata kama upo sawa, siku zote wewe unaisemea serekali na ccm...wewe ni nani na ninani anae kutuma?..
una lipwa na nani? mbona una humuattack mtu personal ? kama ame kula ile za
 
Ipo kazikubwa sana kwa jk na ikulu yake..kakobe km amemfumania vile Jk hana ujanja tena..zaidi ya kuja lalamika jukwaani
 
Wewe ni msemaji wa Ikulu??? Umejitokeza juitetea Ikulu kama nani sasa!!!

Ufafanuzi wao juu ya suala la kuachwa Maaskofu wa PCT kwenye Bunge la Katiba umejaa hadaa na dharau.

Wamezoea kusimamia mambo kimzaha mzaha Wewe una Akili Timamu,Majina yaliwasili Ikulu mapema na kila kitu kilikuwa sawa.

Nini kiliwafanya Ikulu isichukue wawakilishi kutoka kundi hili la Wapentekoste lenye watu Milioni 11?

Iache Ikulu ilibebe furushi lao wenyewe.
 
Mambo ya kusadikika ngoja mukutane na nguvu kubwa neno la mutumishi wa Mungu ni sheria. Eliya alishusha moto ukalamba maelfu. Mumuangukie mutumishi wa Mungu awaombee rehema kwa Mungu la sivyo mutamujua Mungu wake yule afukuzaye pepo wachafu wawatoke watu. Itakula kwenu soon. Nawahurumia.Teh teh teh!.

Na wataweweseka kweli! si unaona wameanza. waraka aandikiwe kikwete majibu atoe huyu demu HAMMY D.
 
Wewe ni msemaji wa Ikulu??? Umejitokeza juitetea Ikulu kama nani sasa!!!

Ufafanuzi wao juu ya suala la kuachwa Maaskofu wa PCT kwenye Bunge la Katiba umejaa hadaa na dharau.

Wamezoea kusimamia mambo kimzaha mzaha Wewe una Akili Timamu,Majina yaliwasili Ikulu mapema na kila kitu kilikuwa sawa.

Nini kiliwafanya Ikulu isichukue wawakilishi kutoka kundi hili la Wapentekoste lenye watu Milioni 11?

Iache Ikulu ilibebe furushi lao wenyewe.

Unaposema Ikulu ujue kabisa una maanisha jumba la Watanzania. Hivyo usidhani pale ni kwa Kikwete, lah hasha. Kila Mtanzania ana haki ya kuonyesha na kueleza hisia zake juu ya mambo ya kitaifa, ikiwemo hili.

Kuhusu idadi ya Wapentekosti: hata wangekuwa million 40, ila kama hawakufuata maelekezo na matakwa ya sheria isinge leta tofauti yoyote. Majibu yangekuwa ni hayo hayo waliyo jibiwa.

Kwa maana hiyo basi, namba na idadi yao isiwape uhalali wa wao kupuuza maelekezo ya sheria. Ingawa personally I doubt hata kama wapentekosti wanafika millioni moja.
 
Uitaji Kakobe wala mungu kukwambia sehemu isiyo na nidhamu/rules na mwongozo thabiti lazima iwe na nyufa tu.

Hivi wazazi wangekuwa wanawaachia watoto ambao wapo nyumbani wajiamulie wakitaka kurudi masaa yoyote ya gizanene sawa, wakiamua kwenda shule au kutokwenda sawa, wakifika nyumbani chakula kilichopikwa siku hiyokama hawajisikii kukila waende jikoni wajiamulie wale nini, na mwisho wasiku wanajibizana na wazazi kila mara wasipokubalina. Unajua wazi familia hiyo itakuwa si imara na kutakuwa amna adabu wala uongozi makini kwenye kuwa guide watoto.

Mambo yanayoendelea sasa kama kweli tunavyosoma ni ishara ya uongozi legelege ndani ya CCM, wahusika inabidi wakae chini maana chama kina pande mbili kama ni serikali moja, mbili au tatu na kuweka wazi mlengo wao wa kichama likishafahamika hilo anaevuka mstari the right procedures have to follow kama ni warning au adhabu, lakini kwa sasa chama cha mapinduzi unaweza sema akina serious party whips vinginevyo wote wangekuwa wanasema kura ya wazi na serikali mbili na watu wapo kwenye mstari. Kama wakishindwa hayo ni commonsense tu ya uelewa wa taasisi zilivyo chama akitamaliza migogoro uitaji kuoteshwa na mungu kuona trend na future implications zake.

Watu hawawezi kukopi vitu kutoka kwa wazungu kama whip na kuwapa nafasi watendaji halafu wasijue shughuli ya party whip ni nini, na kwanini alibuniwa in the first place. kama watu wawili wanaweza wasikubaliane sembuse uwingi wa wanachama cha siasa, lazima watu wajifunze wengine wana handle vipi misimamo iliyo ya kichama, matatizo kama haya hayapo kwenye siasa za afrika tu bali kote duniani ispokuwa huko kwenye liberal democracy when it comes to crunch time mwanachama aombwi kutetea msimamo wa chama na itikadi zake bali ni jukumu lake or else.
 
Unaposema Ikulu ujue kabisa una maanisha jumba la Watanzania. Hivyo usidhani pale ni kwa Kikwete, lah hasha. Kila Mtanzania ana haki ya kuonyesha na kueleza hisia zake juu ya mambo ya kitaifa, ikiwemo hili.

Kuhusu idadi ya Wapentekosti: hata wangekuwa million 40, ila kama hawakufuata maelekezo na matakwa ya sheria isinge leta tofauti yoyote. Majibu yangekuwa ni hayo hayo waliyo jibiwa.

Kwa maana hiyo basi, namba na idadi yao isiwape uhalali wa wao kupuuza maelekezo ya sheria. Ingawa personally I doubt hata kama wapentekosti wanafika millioni moja.

Mkuu,Acha kujikanganya hakuna Maelekezo wala sheria iliyovunjwa na Vionhozi hao wa PCT.

Kila kitu kilikuwa dhahiri na mihuri ya Ikulu ilithibitisha kupokelewa majina hayo pasipo kasoro wala doa.

Labda useme kama una maslahi binafsi kwa kukosekana kwa wawakilishi wa Wapentekoste.

Na kuhusu idadi ya Wapentekoste tafuta taarifa ya mwisho ya Sensa kwa Watz utajionea mwenyewe ukweli wa mambo na hutakuwa na haja ya KUBASHIRI KAA MGANGA WA KIENYEJI.
 
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa hakukuwa na swali lolote linalohusu dhehebu ya mtu kwenye maswali ya sensa. Sasa sijui ni jedwali gani unalo lizungumzia.

Kuhusu kuvunjwa kwa sheria: hivi kwanini tuna bishana kitu ambacho baraza la maaskofu wenyewe wamekiri kuwa wao ndio wenye makosa kwa kutokujua kwao matakwa ya sheria na kuwapelekea kutuma majina yao kiholela holela hivyo kukosa wa kuwawakilisha. Hili mbona lipo wazi na hata uki-google taarifa yao utaiona ya kukiri makosa.
 
Kweli wewe ni uneducated. Hivi Kikwete ni nani kwetu!? Hujui kuwa ni rais wetu sote? Sasa kweli maamuzi yake anayo yafanya huoni kama yana muathiri kila mwananchi?

Kama ungefanikiwa ku-attend vipindi vichache vya civics ya kidato cha pili usinge andika hizo pumba hapo. Ila sikulaumu, cha msingi urudi shule ukaondoe ujinga mkuu.

PUMBA za hali ya juu, hazitofauti na ufahamu wako mdogo...

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha
 
No offence, but to me Kakobe is a cone man. Namuona tapeli kama walivyo matapeli wengine.

Kwanza heshima yangu kwake niliipoteza tangu alivyo kimbia ile ishu ya TANESCO. Yani nilikuwa napita nakuta walaghaika wake wakikesha eti kuomba umeme usipite. Yani kuna watu wajinga hapa duniani.

Hivi sasa kote kumewekwa nguzo na mradi wa TANESCO umesonga mbele huku Kakobe akiambulia aibu na kukimbiwa na waumini wake.
Mkuu naona unatoka povu tu hpa

Hivi ule umeme uliwaka???

Ripoti toka kwa Mainjinia wa pale UDSM inasema chanzo chakutowaka ni nini??

Wapi Ngeleja??

Chezeya watumishi wa Mungu weyeeee
 
HAMY-D Completely... Hapo nakuunga mkono 100%

Siasa na DINI ni vitu viwili mbalimbali --- SERIKALI YA NCHI HII HAINA DINI... kwahiyo walichofanya ni kwa BENEFIT ya NCHI na sio DINI...
 
Last edited by a moderator:
Kweli wewe ni uneducated. Hivi Kikwete ni nani kwetu!? Hujui kuwa ni rais wetu sote? Sasa kweli maamuzi yake anayo yafanya huoni kama yana muathiri kila mwananchi?

Kama ungefanikiwa ku-attend vipindi vichache vya civics ya kidato cha pili usinge andika hizo pumba hapo. Ila sikulaumu, cha msingi urudi shule ukaondoe ujinga mkuu.

Acha kimbele front.... Pumba.vuuuuu!
 
iombe ikulu yako inayokuweka mjini,ipuuze na waraka mpya wa mtikila.
 
Back
Top Bottom