Ombaomba huyu nimemchoka nimfanye nini?

Kuna ombaomba ni wakorofi halafu Wana maneno ya shombo unaweza ukamtembezea kichapo.

Kuna sura inatakiwa umuangalie nayo akikanyanga hapo kwako na jicho kali, halafu umpige mkwara wenye maneno machache sana lakini yanayochoma kama vile we mzee Kuna siku nitakuitia umati wa watu kwa kukuita mwizi wakupe kipigo ili usikanyage dukani kwangu, kama huamini endelea kuja kuja hapa uone kitakachokutokea.

Ukifanya hivyo kwa umakini anaweza akakuogopa akaacha kuja hapo. Pole ndugu kwa changamoto
 
Kuna siku jioni kama yapata saa 1, natembea barabarani alinifuata mtoto mdogo wa kike akanambia "kaka mama anakuita", kugeuka ni mama flani wa makamo amevaa kiheshima , ikabidi nimsikilize "mwanangu baba wa hawa watoto kaondoka na hatujui tutapata wapi chakula,tusaidie chochote tupate hata mkate", kulikuwa na kibinti kingine kidogo....

Nikaingia mfukoni nikampatia yule mama 2000, nikaendelea na safari yangu....

Imepita kama wiki kadhaa, nipo sehemu nyingine akaja binti mdogo "kaka mama anakuita"... kumtazama huyo mama ni yule yule..., nahisi alini claim kwa maana baada ya kugeuka aliona haya... nilimfuata nikamwambia aache hio tabia...

Yule mama ni bonge ya tapeli yaani ukiwa unaongea nae, unaona kama macho yanalenga machozi kama ana huzuni saaana mpaka unamuonea huruma, anavitumia vitoto viwili vya kike vidogo umri 10-12...

Kumbe ni tapeli, wewe unampa 500 au 1000 mwenzako kwa siku anaingiza hata 50000/=,

Nikushauri mkuu huyo si mtu mzuri kama anaanza kukuambia masuala ya ushirikina si mtu mzuri, kama hio dawa anayo atumie yeye aache kuomba watu...
Kuna siku utampatia pesa atakufanyia vitu vya ajabu, ujue hata kwenye uislamu na ukisoma hadithi uchawi upo hata mtume alirogwa na aya(dua) ikashuka ya kuondoa uchawi...

Kwenye biblia pia uchawi upo ukisoma waganga wa Pharaoh jinsi walibadili fimbo kuwa nyoka ule ni uchawi wa hatari... tuwe makini...
 
Salamu wana JamiiForums
Baada ya salamu acha niende kwenye mada husika kama kichwa kinavyo sema hapo juu. Kuna siku nilikuwa naongea na rafiki yangu dukani kwake akatokea mtu mzima akasema:- wanangu baba yenu nina njaa sana naomba hela nikale naona haya kuomba ila sina budi. Nikamchukuwa kona kuna genge la vyakula nikamnunulia chakula na juisi. Nikaondoka baada ya miezi 4 huyu mzee alikuja dukani kwangu. Akaniomba hela nikamwambia mzee wangu hali ya biashara ngumu kwa leo sina. Aliguna na kuniangalia huyo akaondoka, baada ya wiki akaja tena nikamjibu vilevile. Aliguna(mmhh) tena akaangalia dukani kila kona halafu akaniambia mambo magumu unayataka mwenyewe. Halafu akaondoka zake baada ya wiki akaja tena siku hii alokuja nilikuwa nafanya hesabu ya dukani. Nimeinama nikiwaza nusu ya mwezi mauzo yake kama ya siku 5 tu(mauzo madogo). Akanisalimia nikamwitikia kama kawaida yake akaomba tena nikaangalia hela mfukoni mwangu nilikuwa na misimbazi tu nikamjibu njoo siku nyengine. Mara alikuja mteja na kuulizia bei ya bidhaa hakununua na kuondoka. Hapa ndipo huyu ombaomba akanambia mwanangu kuna njia za kuleta mafanikio kama wenzako wanavyo fanya. Nikamjibu inshallah Mwenyezi Mungu ataleta kheri, akasema mwanangu tuongee nikufanyie mambo yawe mazuri kwakweli sikuwa na furaha kutokana na hesabu ya mauzo, nikamjibu jifanyie wewe hayo mafanikio ili maisha yako yabadilike. Aliniangalia kama dakika 1 halafu huyo akaondoka, hapa ndipo kijana mmoja wa hapo kazini akanambia boss. Huyu Mzee anakuja kila siku na mimi nishamchoka manake alikuja na vitu akanipa nifukize humu ndani nilikataa. Yaani alisema huja pale na kumtaka afanye mambo ya kuvuta wateja kwa kutumia uchawi. Sasa hapa alipofikia na hizi tabia zake nimemchoka kwakweli. Naomba kwenu ushauri nitumie njia ipi ya kistaarabu kuongea nae ili asije tena Dukani kwangu au kama atakuja basi asilete maneno yake ya kuvuta wateja kichawi.

Nb:- Huwapa ombaomba hela ila sio kila siku na kuna wengine wajeuri sana kwakweli

Huyo mzee anakaa wapi
 
Kuna siku jioni kama yapata saa 1, natembea barabarani alinifuata mtoto mdogo wa kike akanambia "kaka mama anakuita", kugeuka ni mama flani wa makamo amevaa kiheshima , ikabidi nimsikilize "mwanangu baba wa hawa watoto kaondoka na hatujui tutapata wapi chakula,tusaidie chochote tupate hata mkate", kulikuwa na kibinti kingine kidogo....

Nikaingia mfukoni nikampatia yule mama 2000, nikaendelea na safari yangu....

Imepita kama wiki kadhaa, nipo sehemu nyingine akaja binti mdogo "kaka mama anakuita"... kumtazama huyo mama ni yule yule..., nahisi alini claim kwa maana baada ya kugeuka aliona haya... nilimfuata nikamwambia aache hio tabia...

Yule mama ni bonge ya tapeli yaani ukiwa unaongea nae, unaona kama macho yanalenga machozi kama ana huzuni saaana mpaka unamuonea huruma, anavitumia vitoto viwili vya kike vidogo umri 10-12...

Kumbe ni tapeli, wewe unampa 500 au 1000 mwenzako kwa siku anaingiza hata 50000/=,

Nikushauri mkuu huyo si mtu mzuri kama anaanza kukuambia masuala ya ushirikina si mtu mzuri, kama hio dawa anayo atumie yeye aache kuomba watu...
Kuna siku utampatia pesa atakufanyia vitu vya ajabu, ujue hata kwenye uislamu na ukisoma hadithi uchawi upo hata mtume alirogwa na aya(dua) ikashuka ya kuondoa uchawi...

Kwenye biblia pia uchawi upo ukisoma waganga wa Pharaoh jinsi walibadili fimbo kuwa nyoka ule ni uchawi wa hatari... tuwe makini...

Duh hatari sana halafu unajua kuna ombaomba wengi sana. Na wengi wao wamama tena huwezi kujua kama ombaomba yaani juzi alikuja mmoja aliniomba nimebaki kumshangaa nikampatia huyo akaondoka. Na asilimia kubwa wanasema hawana nauli pia alikuja jamaa alisema anatokea Kenya ila hana nauli ya kurudi kwao akasema msikitini washampatia nauli ila anahitaji ya mpaka kufika nyumbani kwake na chakula halafu jamaa kavaa kweli angenambia mkuu wa mkoa basi ningeliamini jinsi alivyo vaa
 
Mkuu mimi mwenyewe jana tu nakutana na kijana tu ilikuwa jioni natoka kazini ananiambia "bro samahani, habari ya jioni, bro giza ndio hilo linaingia na sijapata chochote..." kabla hajaendelea kwa sababu imani ilishanitoka juu ya hawa watu nilimkatisha tu "kaka sipo vizuri..." akaenda zake... nilimsindikiza kwa macho alikuwa anaelekea mahala wanauza pombe...

Kuwa nao makini, wanapokuja wahoji...
yeye ni nani, ana shida gani, kwa nini hafanyi kazi, anaishi wapi, ana familia, ana mapungufu yapi yanamfanya asifanye kazi kuingiza kipato...
mfano hao wa nauli unamuuliza kenya sehemu gani, nauli sh ngapi n.k, au na mimi naelekea huko uendako upo tayari nikulipe usafiri?

Kwa maswali hayo ukiwa makini lazima ajichanganye kama ana nia ovu, na mwenye shida utamjua tu...,
 
Acha kugawa hela hovyo kwa watu utafilisika hasa omba omba asilimia kubwa sio watu wazuri ni heri umnunulie msosi na sio kutoa hela. Be careful sio kila omba omba ni ana shida wengine ni agent of evils.
Umemaliza 🙌yaan asirudie kabisa,tena huyo mzee akija amfukuze kwa kumkaripia ikibid na viboko juu ,au hata akashtak kwa uongoz wa huo mtaa,tena hiyo ishara ya kuguna ni ya kichawi kabisa ,nyie mi yalinikuta mwaka Jana tena mtu wng alinionya mpaka akawa anamuita yule ombaomba anirudishie pesa yangu ,yy(mtu wng)angemnunulia chakula Cha bei zaid ya hiyo hela lakin yule ombaomba alikataa na kukimbia na nilipoteza milion moja na nusu bila kujua zimeenda wap ,coz hiyo pesa nlompa huyo ombaomba niliitoa kwny hilo bunda,mtu Wang akanambia pesa nizihamishe lakin wap,toka siku hiyo niliapa cji saidia ombaomba never ,naombwaga Sana but sitoi ,naishia kutukanwa nao ombaomba na half Wala nin,yaan nimewachukia,cjui sura ya huruma,nikisaidia Sana labda yatima na wagonjwa(tena kwa kuwafata mahospitalin)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom