Omba Omba Mitaani ni Jukumu la Nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Omba Omba Mitaani ni Jukumu la Nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by DSN, Apr 23, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Zamani kidogo wakati nakua sikupata kukumbuka kama kuna watu walikuwepo wanaitwa omba omba.

  Ghafla miaka ya mwishoni na tisini na kuna ongezeko kubwa sana la ombaomba mijini,na kwenye majiji yetu.Nomba mnijuze ni jukumu la nani na mzigo wa nani kushughurikia ombaomba.

  Nani analea hawa ombaomba, manake si kitambo, nimesoma kwenye gazeti na kuona picha ya mtoto wa miaka yapata minne akimuomba mpita njia huko Arusha.

  Kama picha hii, taifa na wanajamii nani kati yao wananchi na serikali anajukumu na swala hili la ombaomba.Na nini jibu la tatizo hilo, manake naona hivi hiyo ndio TASWIRA yetu, Je ni kweli hiyo ndio taswira yetu na kuwa hatuna majibu ya tatizo hilo kweli?.

  Ni wajibu wa nani?
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Jambo la kwanza wanaume tuache kuzaa hovyo hovyo mtaani, Jambo la pili serikali iboreshe huduma za jamii na mazingira mazuri ya kujipatia vipato vijijini.mfano mtu apate kibarua walau kwenye mashamba makubwa ya kahawa,chai,katani ili ajikimu na watoto wake.Tatu jamii yote iwe na jukumu la kulea yatima.mfano kila familia ingelea yatima au kusaidia vituo vya kulelea yatima kusingekua na watoto mitaani
   
 3. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  yanh mkuu mimi mwenyewe inanikera sana!sijui ni taifa gani linaandaliwa hapo baadae!siku hizi imekua ndio fashion,watoto wamejaa kila mahali na pia mama zao wamekaa pembezoni mwa barabara wanasubiria hesabu kama madaladala vile!
   
 4. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Mimi na wewe na hakuna mwingine zaidi.
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hii imekaa kisiasa zaidi, mimi na wewe tutahudumia omba omba wangapi ndugu yangu? Na majukumu mengine katika ukoo wako??
  Lazima kuwe kuna mfumo fulani katika nchi wa namna ya kushughurikia hii kitu...
  Sasa kama JK naye anapita na kuwapa pipi (refer ile picha ya kwenye kampeni zake za 2010, kama kuna mtu mwenye uwezo ai-uproad tujikumbushe) na kuondoka zake, nadhani inachukuliwa kama ni jukumu la wasamalia wema wenye uwezo wa kujitolea, sasa inapofika hao wasamalia wakaelemewa na mzigo ndio huwa wanawatuma kuja mijini kuomba omba, nina mfano wa kituo kimoja cha Kilimanjaro, Moshi kinaitwa Msamalia Children Centre, na baadhi yavituo vinawatumia kama dili kupatia misaada toka kwa wazungu!
  Ofcz ni jukumu la UMMA, lakini tujiulize umma ni nani? Kama ni hvyo basi mfumo hauwezi ukakwepa lawama hizo.
   
 6. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kwanza siyo kweli kwamba omba omba hawakuwepo, walikuwepo tangu miaka ya sabini ila hivi sasa wameongezeka sana idadi yao. Hapo zamani walikuwa wanatoka mkoa mmoja wa kati ya Tanzania (kumbuka sakata la Mh JSM???)

  Tuanowalea ni sisi wenyewe tunaopita mabarabarani na kuwarushia vijisenti. Kwa siku huwa anakusanya mapato mazuri bila ya kulipa kodi wala VAT. Siku za ijumaa na jumapili ndizo zenye baraka nyingi kwa watu hawa.

  Unakumbuka ilipozuka stori ya mkono wa manyoya na watu wakawachunia kuwapa msaada? Omba omba walilalamika sana kwa kukosa mapato yao, kitu ambacho kinadhihirisha wazi kuwa ni sisi ndiyo tunaowaweka hapa mjini.
   
Loading...