Omba omba huyu anastahili viboko!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Omba omba huyu anastahili viboko!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchajikobe, Feb 24, 2010.

 1. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Habari zenu ndugu wana JF,leo hapa jamvini kuna kitu nataka kuwajuza,kwa wale watumiao barabara ya Ali Hassan Mwinyi na ile ya umoja wa mataifa pale karibu na trafic lights za Salender kuna omba omba mmoja mimi binafsi naamini anastahili viboko ili aache utani na awaombao.Huyu ombaomba ni mvulana ambaye amekuwa pale kwa miaka mingi kidogo akijitafutia ridhiki,lakini kinachonisababisha nimtafutie bakora ni kwamba hana ubunifu na kazi yake,huyu jamaa ana kidonda kikubwa sana mguuni na hicho ndicho kimpatiacho ridhiki,kinachonishangaza kwa huyu bwana ni kwamba kila siku anaomba hela ya kwenda kujitibu,lakini kila mwaka kidonda kiko vilevile na hakikauki,sijui kama ni kidonda kweli au ni sanaa,maana kwa mtu wa kawaida ukiwa na kidonda kama kile huwezi fika miezi miwili bila kukatwa huo mguu!Nimetafakari kwa kina nikaona huyu jamaa anatutania sisi ombwaombwa,ile inaweza ikawa ni sanaa,sababu mtu gani hahisi hata maumivu,wala kidonda hakiongezeki wala kupungua?Huyu mimi naona anastahili viboko ili aache ujinga wake huo!!
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,116
  Likes Received: 2,413
  Trophy Points: 280
  Hata mimi huwa anainiboa anavyolazimisha tutizame hicho kidonda chake! Kwa kweli tunatatizo kubwa sana. Wengi wa hawa ombaomba wanao uwezo wa kujitafutia kipato bila kuomba.

  Hii attitude ya kuomba ni mbaya sana inapokuwa kwa mtu mojamoja lakini ni mbaya zaidi inapokuwa kwa taifa. Viongozi wetu wanazunguka huku na huko kujipendekeza na kuombaomba wakati uwezo tunao (very simila to hawa ombaomba!).
   
 3. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Binafsi hii inakera sana,

  Jana kwenye luninga eti ombaomba wameandamana kupinga kuwa mwenzao kamgeuza mtu mkono ukawa na manyoya, halafu hiyo stesheni inatupotezea muda kuturushia hewani. Hivi hao ombaomba hawana akili. Kuna mwenzao China ambaye ukimwona hata wao ni wazima sana, lakini anamiliki duka lenye slogan "Half Man, Half Price"
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,181
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Cjui kama ni kweli ila mi niko huku Serengeti National. Huku tunasikia kuwa kuna ombaomba mmoja hapo salender bridge kamwomba mama moja chapaa afu huyo ombwaombwa akaota manyoa, halafu ghafla ombaomba na ombwaombwa wakapotea katika mazingira ya kutatanisha. Yakweli hayo?
   
 5. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kama viongozi wetu wanaomba kwa nini omba omba wasiandamane jamani?
   
 6. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 259
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  KWA TAARIFA YAKO ILE NI NGOZI YA NG'OMBE ANACHUKUA MACHINJIONI KILA SIKU. Bado yupo mbona nasikia ndiye aliyehusika na manyoya ya mkononi yaani nyaunyau?
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna kidonda pale angeshakufa kwa kidonda kama ile tangu nimuone zamani sana huwezi kuishi na kidonda kama ile..feki
   
 8. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Duu wewe kiboko ulifanyaje utafiti mgumu kiasi hicho hadi ukagundua hilo gozi la ng'ombe,sasa huwa ananunua au hupewa bure?
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Msiwakasilikie hawa ombaomba, kwani OMBAOMBA NI UTAMADUNI WA KITAIFA!!!
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Una maana hata Muungwana ni Omba Omba?
   
 11. k

  kamaghe Member

  #11
  Feb 24, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mh
  hapa sina comment
   
 12. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Pale yupo na kijana mwingine mikono yake kama vile imeathirika na ukoma, yule kijana alifukuzwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kwa kuwa ni mlevi kupindukia na anavuta sana bangi.,waliokuwa wanamlea wanasema kuwa alikuwa pia ana kamchezo ka kulawiti wenzake hapo kituoni na mara kwa mara alikuwa anatoroka na kuingia mitaani kuomba mwisho wake wakamtimua kabisa na hata sasa inasemekana kila jioni akifunga mahesabu anaenda bar na kuanza kuangusha moja moja, sasa mtu kama huyu hata kama mikono yangu haitaota manyoya kwanini nimsaidie .
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2010
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
   
 14. Mwananzuoni

  Mwananzuoni JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 291
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mjini shule!
   
 15. m

  mnyakyusa JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 248
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inawezekana anapaka damu ya ng'ombe...au ndio kama chuma ulete
   
 16. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  EeKa ni kweli ombwaombwa kaota manyoya na kuishia baada ya kutoa mshiko...
   
 17. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,464
  Likes Received: 26,354
  Trophy Points: 280
  Masanilo, swali lako ni sawa na kuuliza "kanzu inavaliwa Comoro?" jibu ni nini?
   
 18. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tena yeye ndio kiongozi wa ombaomba.,hebu imagine tunaomba michango ya sherehe, pesa za maendeleo ya nchi, wazee wa manyoya nao wanaomba pesa za kujikimu kimaisha n.k. sasa ni nini hiki kama si taifa la ombaomba.
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 42,107
  Likes Received: 37,480
  Trophy Points: 280
  Anajiita papaa ya pesa nyingi.
  Hana kidonda wala nini, usiku huwa anakuwa mzima,
  akimaliza kuzungukazunguka, huwa anaenda kupooza koo pale kona bar, afrika sana.
  Pitapita usiku utamuona.
   
 20. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Unanitia hasira sana kama ni kweli,yaani watu watoke jasho kwaajili ya mzembe kama huyu,ole wake nimuone leo ni mikwaju kwa kwenda mbele!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...