Je, huyu anastahili kuwa mke?

Je, huyu anastahili kuwa mke?

jichopevu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
406
Reaction score
248
Alikuwa ni mke mtarajiwa wa one of my best friends...baada ya rafiki yangu kuhangaika sana kutafuta atakaemfaa ndo akaangukia kwa huyu dada. At first, the girl was good, too humble na kiukweli alionyesha tabia nzuri sana kwa jamaa. They met, they discussed and decided to be long life partner (kwa maana wafunge ndoa) na huu ndo ulikuwa mwaka wa kufunga ndoa.

Walikuwa wanaishi sehemu tofauti, bi dada akiwa chuoni mkoa flani hivi na mshkaji wangu akipiga kazi zake pale central zone. Jamaa alianza kuhisi mabadiliko kwa yule bi dada...first alikuwa hana tabia ya kuomba omba hela ovyo na jamaa ndo alikuwa anamtumia tu ila kama akiishiwa huwa anamwambia jamaa na jamaa anatuma. but ikaja time bi dada alipitiliza sana kuomba fedha hadi jamaa akashangaa. Pili, alianza tabia ya kumuongopea mshkaji na kuweka mapozi sana, simu ikipigwa ichukue mda kupokelewa na akipokea mara nimechoka nipigie baadae mara Oooh subiri kata piga baaada ya dakika 5. Jamaa akajiuliza sana akaamua afanye uchunguzi wake mdogo.

Uchunguzi ulipokamilika akagundua kwamba huyu dada maeshikwa masikio na mashosti zake ambao kwa lugha nyepesi naweza kuwaita ni mcharuko na ndo walikuwa wanamfundisha hayo eti kumpima jamaa kama anampenda kweli au la. Pia walimwambia ya kwamba wanaume siku hizi ni kuwalia chao tu, so kamua nae akawa ndo anakamua kweli. Jamaa akabwaga manyanga akaachana nae.

Dada amekuja kuomba msamaha kwamba marafiki zake ndio waliompoteza na kusababisha afanye yote yale. Jamaa anajiuliza maswali kadhaa

1: Kama marafiki wameweza kumteka na kuingiza maneno kiasi hiki na yeye akakubali na kuwafuata, na hii katika uchumba tu, je katika ndoa si itakuwa hivi hvi au zaidi?

2: Dada kama huyu anaweza kweli kuficha siri za ndani za nyumba? maana ameshaonyesha udhaifu

3: Jamaa anajiuliza hivi nguvu ya marafiki si itakuwa kubwa kuliko yake kwa mkewe? maana inaonekana huyu binti ndo alivyojiweka

Je, mdau kama ingekuwa ni wewe na ndo yametokea haya ungefanyaje? na je anastahili kuwa mke?
 
Mi nadhani la msingi ni yeye afuate moyo wake unavyotaka,kwani kila utakayempata hawezi kuwa perfect 100%,ila kwa kweli ni bora kuwa na mke asiyejichanganya sana na marafiki kuliko anayejinganya hovyo hovyo,ndoa nyingi zina migogoro kwa ajili ya kusikiliza ushauri wa nje ambao saa nyingine unapotosha.
 
mwambie apige chini uyo,hakuna kitu apo.
 
Always we learn through mistake so she might be a good wife in future......lakini dalili ya mvua ni mawingu....so afate moyo wake unamwambia nini na Mungu amuongoze ktk kufanya maamuz ya busara.
 
Hili la mke ni suala gumu sana kibinadamu........!
sometimes linachosha.
Mungu tupe mongozo vijana wako tupate wake wataofaa.
 
Nitamfikisha huu ujumbe rafiki yangu ili achuje mwenyewe

Mi nadhani la msingi ni yeye afuate moyo wake unavyotaka,kwani kila utakayempata hawezi kuwa perfect 100%,ila kwa kweli ni bora kuwa na mke asiyejichanganya sana na marafiki kuliko anayejinganya hovyo hovyo,ndoa nyingi zina migogoro kwa ajili ya kusikiliza ushauri wa nje ambao saa nyingine unapotosha.
 
Wakati mwingine "ushamba" au umri na uelewa mdogo katika masuala ya marafiki na mapenzi hupelekea mtu kufuata ushauri mbaya. Kama huyu dada alikuwa anafanya yale kwa kukupima, bila yeye kujihusisha na wapenzi wa nje au kufanya mambo machafu akikuzunguka wewe mpenzi wake; basi anaweza kuwa mke bora maana ni udhaifu tu wa kufuata ushauri mbaya. LAKINI kama aliungana na marafiki na kutenda uzinzi na mengine, ACHANA NAYE.
 
Hamna ki2 hapo kaka. Huyo demu ni mambo mengi (tunawaita 'unga wa ngano'). Huyo alibadilisha channel, sasa katumika huko then akaachwa kizani, now anarejesha majeshi kwa mshikaji. Kuna msemo unasema hivi ''When You lost the way, go back to the beginning''. So akili kumkichwa mkuu
 
Unazungumzia mke wa ndoa,yaani kama mama zetu!!!????Mwambie aaendelee kummega kisela,hafai kwa matumizi ya ndoa huyo...
 
Kama kosa kalijua huyo bidada, fine. Kaka mpe takecare, then mpe nafasi tena, hatoichezea. Mkomeshe kuhusu marafiki hao, atajitambua. Atapoingia kwenye ndoa atatulia
 
Kama mimi ningechukulia poa tu kwani hujafa hujaumbika hii dunia tunapita.........ukiamini kila binadamu ana mapungufu yake basi utachukulia hayo ndo mapungufu yake na kuendelea na safari kwa sababu muda hausubiri
 
kama hakugegedwa kwingine its ok.....haya mengine yanaokea tu...ila mshauri amrudishe na onyo kali...kama hajagegedwa kwingine lakini kwa kipindi hicho alichobadilika...
 
Kama ni mashoga zake basi anafaa ila achunguze vizuri Kama hawajamshauri kuongeza kidumu.
 
Hakuna binadam aliye kamilika,,kwanza tuliza kichwa then usikilize moyo wako unataka nini,,,kwa upande wa pili,,.kila mwanamke ana matatizo yke,,mpe nafasi ya kujielezea itakueongezea jambo.!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom