GE2025 Olengurumwa: Mfumo wa CCM unazaa wabunge waoga

GE2025 Olengurumwa: Mfumo wa CCM unazaa wabunge waoga

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Anaandika Mkurugenzi wa THRDC Onesmo Kasale Olengurumwa kupitia ukurasa wake wa Instagram:

====

Sijajua tunataka wabunge wa aina gani - nilisifia hizi kanuni mpya za Chama Cha Mapinduzi CCM upande mmoja kuwa imeongeza watu wengi kupiga kura na kupunguza rushwa ila nikaonesha hatari ya utaratibu wa kurudisha majina matatu kwamba italeta shida sana kwa wale wabunge wanaosimamia haki za jamii na kusema itatuletea wabunge waoga zaidi kwa kuwa wanajua kuna kukatwa (kuenguliwa kwenye mchakato).

Mimi nilidhani kila anayeomba ubunge angepigiwa kura ndani ya chama ndio uteuzi ufuate badaye ili kuwapa nafasi wanachama wa CCM wachague mtu wanayemtaka. Naamini kabisa wana CCM mfumo huu mpya wa kurudisha majina matatu inaweza leta mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM kama usipoangaliwa upya.

Baada ya uchaguzi huu nashauri CCM wafanye mapitio ya kanuni hizi mpya za uchaguzi ili kutoa zaidi demokrasia ndani ya chama. Malalamiko ya watu kukatwa kwa ngazi ya Wilaya ni mengi - pamoja na kwamba wilaya sio hatua ya mwisho lakini ina sehemu kubwa kushawishi uamuzi na pia kumbuka hawa ndio watasimamamia pia uchaguzi na ndio watakuwa muda wote na wagombea.

Soma Pia: Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwahiyo hata mtu waliyempendekeza tofauti akirudishwa sijui watashirikiana naye vipi. Kukatwa Wilayani inawezekana kabisa na badaye kurudishwa, hata mimi wakati nagombea uenyekiti UVCCM Ngorongoro nikiwa chuo mwaka 2008 walikata jina Wilaya na kurudishwa huku juu badaye. Ni matumaini kuwa haki itatendeka katika hatua zinazofuata na watu kama kina Mpina wakarudishwa."-Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.
 
Attachments

  • 1752327138036.jpeg
    1752327138036.jpeg
    119.3 KB · Views: 20
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Onesmo Olengurumwa ameonesha hofu yake kuhusu mfumo mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani kupitia utaratibu wa kurudisha majina matatu kutoka ngazi za chini kuelekea juu.

Kupitia maoni yake ya kiuchambuzi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Olengurumwa amesema kuwa ingawa mfumo huu umeongeza ushiriki wa wanachama wengi kupiga kura na kupunguza mianya ya rushwa, bado kuna hatari kubwa inayoweza kujitokeza. Anasema kuwa mfumo huo unaweza kupelekea kuchipuka kwa wanasiasa waoga na wasioweza kusimamia haki za jamii kwa ujasiri, kwa sababu wanakuwa na hofu ya “kukatwa” kwenye mchakato wa uteuzi.

"Mimi nilidhani kila anayeomba ubunge angepigiwa kura ndani ya chama ndipo uteuzi ufuate baadaye, ili kuwapa wanachama wa CCM nafasi ya kuchagua mtu wanayemtaka," alisema Olengurumwa.

Aliongeza kuwa utaratibu huu wa kurudisha majina matatu unaweza ukazua mpasuko mkubwa ndani ya CCM kama hautafanyiwa tathmini ya kina mara baada ya uchaguzi.

Olengurumwa ametoa mfano wa hali halisi katika maeneo mbalimbali ambapo malalamiko ya wagombea kukatwa katika ngazi ya Wilaya yamekuwa mengi. Ingawa anakiri kuwa ngazi hiyo si ya mwisho, anaeleza kuwa ina ushawishi mkubwa kwa sababu viongozi wa Wilaya ndio wasimamizi wa uchaguzi wa ndani na watakuwa karibu zaidi na wagombea wakati wa kampeni.

"Unapomkata mtu wilayani, halafu jina lake lisirudishwe, halafu wajumbe wake wa Mtaa au Kata walimpendekeza mtu mwingine, watashirikiana vipi wakati wa uchaguzi?" alihoji kwa uchungu.

Akirejea historia yake binafsi, Olengurumwa alisema kuwa mwaka 2008 alipokuwa mgombea wa uenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro akiwa bado chuoni, jina lake lilikatwa ngazi ya Wilaya lakini baadaye likarudishwa juu. Kwa uzoefu huo, anaamini bado kuna nafasi ya haki kutendeka kwa wagombea waliokatwa awali ambao ni wabunge jasiri wanaopaswa kuendelezwa na CCM.

Ametoa wito kwa CCM kufanya mapitio (review) ya kanuni mpya za uchaguzi mara baada ya uchaguzi huu ili kuimarisha demokrasia ndani ya chama. Anasisitiza kuwa ni muhimu kwa CCM kuendelea kuwapa nafasi watu wenye uwezo wa kusema ukweli na kusimamia maslahi ya umma bila woga, ili kuaminika zaidi kwa wananchi na kuendelea kuwa na Bunge lenye nguvu na tija kwa taifa.
 
Anaandika Mkurugenzi wa THRDC Onesmo Kasale Olengurumwa kupitia ukurasa wake wa Instagram:

====

Sijajua tunataka wabunge wa aina gani - nilisifia hizi kanuni mpya za Chama Cha Mapinduzi CCM upande mmoja kuwa imeongeza watu wengi kupiga kura na kupunguza rushwa ila nikaonesha hatari ya utaratibu wa kurudisha majina matatu kwamba italeta shida sana kwa wale wabunge wanaosimamia haki za jamii na kusema itatuletea wabunge waoga zaidi kwa kuwa wanajua kuna kukatwa (kuenguliwa kwenye mchakato).

Mimi nilidhani kila anayeomba ubunge angepigiwa kura ndani ya chama ndio uteuzi ufuate badaye ili kuwapa nafasi wanachama wa CCM wachague mtu wanayemtaka. Naamini kabisa wana CCM mfumo huu mpya wa kurudisha majina matatu inaweza leta mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM kama usipoangaliwa upya.

Baada ya uchaguzi huu nashauri CCM wafanye mapitio ya kanuni hizi mpya za uchaguzi ili kutoa zaidi demokrasia ndani ya chama. Malalamiko ya watu kukatwa kwa ngazi ya Wilaya ni mengi - pamoja na kwamba wilaya sio hatua ya mwisho lakini ina sehemu kubwa kushawishi uamuzi na pia kumbuka hawa ndio watasimamamia pia uchaguzi na ndio watakuwa muda wote na wagombea.

Soma Pia: Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwahiyo hata mtu waliyempendekeza tofauti akirudishwa sijui watashirikiana naye vipi. Kukatwa Wilayani inawezekana kabisa na badaye kurudishwa, hata mimi wakati nagombea uenyekiti UVCCM Ngorongoro nikiwa chuo mwaka 2008 walikata jina Wilaya na kurudishwa huku juu badaye. Ni matumaini kuwa haki itatendeka katika hatua zinazofuata na watu kama kina Mpina wakarudishwa."-Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.
Wazo zuri ila wenye chama chao ndio wenye maamuzi
 
Back
Top Bottom