Oleksandr Usyk amtwanga Tyson Fury na kuwa Undisputed Heavyweight Champion...

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,814
15,740
Oleksandr Usyk anakua UNDISPUTED CHAMPION wa kwanza wa Heavyweight (Boxing) kwenye 4 belt Era, mara ya mwisho Undisputed Champion kwenye division hii alikuwa Lennox Lewis mwaka 1999 wakati wa mikanda mikuu mitatu, heshima kwake
IMG-20240519-WA0016.jpg
 
The Kingdom Arena in Riyadh
1716080594220.png

Uchambuzi toka kwa nguli wa mchezo wa ngumi jinsi walivyowaona mabondia hawa kabla ya pambano hili:


"Mtu huyo yuko juu, Oleksandr Usyk amejifua hadi kufikia uzani wa juu. [Paundi 221] bila hata wakia ya mafuta kwenye mwili wake. Mtu huyo ni mnyama. Nadhani kuna shinikizo kwa mabondia wote wawili. Watapata nafasi ngapi kwenye ubingwa wa uzito wa juu duniani usiopingika?”
 
Last two fights za Fury nilijua hatatoboa kwa Usyk.

Fury alimpiga Wilder kwa KO lakini hakupata ushindani uliotakiwa, Wilder alikuwa mwepesi na hakuwa na stamina, kuanzia round ya 7 kwenye fight yake na Fury alichoka akawa anasubiri kuangushwa dakika yoyote, na ndicho kilichotokea.

Baada ya pale, Fury akaja kucheza na Ngannou, jamaa aliyetokea kwenye MMA, fight yake ya kwanza kwenye boxing bado aka manage kumuangusha Fury kwa konde moja zito. Japo Fury alikuja kushinda baadae kwa pointi, lakini nilijua tu huyu akija kukutana na bondia anayejielewa lazima apoteze.

Hiki ndicho kilichotokea kwa Usyk, Fury hawezi kumpiga Usyk hata kwenye rematch mwezi wa kumi, naamini bado atapigwa tu, kwasababu;

- Kwanza Usyk ana stamina, ana uwezo wa kumaliza round zote kiushindani, hachoki kizembe.

- Anajua kujilinda, umbo lake fupi anajua namna ya kulitumia pale anapokuwa akishambuliwa, utaishia kumchezea maeneo mengine ya mwili kama mbavu, lakini kichwa chake utakitafuta sana...
 
Pambano lilipaswa kuisha raundi ya 9 ila refa aliamua kumbeba Fury.

Usyk akija kumpiga Wilder, atakuwa kamaliza kila kitu kwenye Heavy-Weight boxing.
Wilder hana ishu sahivi
 
Back
Top Bottom