Kweli inaumiza na inatesa, ila msamaha una faida kwako kuliko yule unayemsamehe,kwanini uishi na uchungu maisha yako yote?
Ukiwa na hasira hata huyo mtoto hutampenda....ulikosea kufanya mapenzi na mwanaume asiyekuwa na kiapo nawe,matunda ndo hayo....usimlaum yeye tu...unapaswa kujua ulipaswa kujilinda....Kukimbiwa/kuachwa na mwanaume aliyekupa mimba si mwisho wa maisha....tuna wanawake wengi tu mifano....ukianguka unasimama,unajipanga,unasonga mbele kwa umakini zaidi.
matunda ya uzinzi hayo unalalamika nini? Na ukipewa ngoma je?
Yaani! Ingekuwa ni miaka ile ya 19 kweusi mtu ataeleweka.Mwanamke au msichana wa miaka hii yenye UKIMWI na magonjwa mengine, mtu unapataje mimba tu? Mwanamke mwenye kujiheshimu hatajiachia kupata mimba ovyo ovyo....Ukiachwa au kukataliwa mimba ni halali yako.Hata ukinuna, haikusaidii maana jamaa anaangaza mbele na dua la kuku halimpati mwewe.Mimi ni mwanamke lakini jwa hili wala sioni huruma.Labda kama ni msichana mdogo sana kama wale JK aliosema wana kiherehere, au kama umebakwa ukapata mimba.