Ole Sosopi, BAVICHA, CHADEMA acheni umbumbumbu, Wizara ya TAMISEMI ilikuwa chini ya ofisi ya Raisi kipindi cha Mkapa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Kwa mara kadhaa nimewasikia viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mbowe,Lissu na hivi karibuni nimemsikia Ole Sosopi akiongopea umma kuhusu Wizara ya TAMISEMI.

Kutokana na umbumbumbu wao pamoja na wengi wa wafuasi wao wamekuwa wakisema "Hakuna awamu ambayo TAMISEMI ilikuwa chini ya ofisi ya Rais" wakihalalisha kuwa Rais Magufuli kafanya hivyo ili kujilimbikizia madaraka.

Ni hivi ukweli ni kuwa Wizara ya TAMISEMI imekuwa chini ya ofisi ya Raisi katika awamu zote isipokuwa enzi za JK ambaye alihamishia Wizara ya TAMISEMI ofisi ya waziri Mkuu.Kwa kuweka kumbukumbu sawa enzi za Mzee Mkapa TAMISEMI ilikuwa chini ya ofisi ya Rais kwa miaka yote kumi (10).

Ninaambatanisha orodha ya baadhi ya Wizara na mawaziri wa serikali ya Benjamin Wiliam Mkapa kuweka kumbukumbu
sawa.
Screenshot_20191114-192713.jpeg
Screenshot_20191114-193816.jpeg
Screenshot_20191114-194011.jpeg
Screenshot_20191114-194003.jpeg
Screenshot_20191114-193954.jpeg
 
Mkapa naye aliwaita watendaji ikulu na kuwaagiza waharibu form za wagombea wa upinzani??

Tuanzie hapo kwanza.
 
Baada ya kuona mleta mada ni Wakudadavua nikashiti kusoma ulichoandika!
Nikajua tu humo ndani lazima anamzungumzia Mbowe na Chadema.
Mlio soma mada hii pls niambieni kama kuna jipya!
 
Ndugu zangu,

Kwa mara kadhaa nimewasikia viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe,Lissu na hivi karibuni nimemsikia Ole Sosopi akiongopea umma kuhusu Wizara ya TAMISEMI.

Kutokana na umbumbumbu wao pamoja na wengi wa wafuasi wao wamekuwa wakisema "Hakuna awamu ambayo TAMISEMI ilikuwa nchini ya ofisi ya Rais" wakihalalisha kuwa Rais Magufuli kafanya hivyo ili kujilimbikizia madaraka.

Ni hivi ukweli ni kuwa Wizara ya TAMISEMI imekuwa chini ya ofisi ya Raisi katika awamu zote isipokuwa enzi za JK ambaye alihamishia Wizara ya TAMISEMI ofisi ya waziri Mkuu.Kwa kuweka kumbukumbu sawa enzi za Mzee Mkapa TAMISEMI ilikuwa chini ya ofisi ya Rais kwa miaka yote kumi (10).

Ninaambatanisha orodha ya baadhi ya Wizara na mawaziri wa serikali ya BMW kuweka kumbukumbu sawa.View attachment 1263255View attachment 1263256View attachment 1263257View attachment 1263258View attachment 1263259
Sawa tumekusikia dada, kalale sasa
 
Back
Top Bottom