Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,691
Wimbi la mabadiliko limesambaa,kusini na kaskazini,Magharibi na Mashariki..Katika Jimbo la Isimani,ngome ya chama cha Mapinduzi kwa miaka 20 sasa imetikiswa.Jimbo la Isimani,CCM na mgombea wake Lukuvi amekuwa anapita bila kupingwa kwa miaka 20 sasa,lkn mwaka huu kakutana na upinzani toka kwa kijana Patrick Ole Sosopi toka CHADEMA.Ni ajabu na kweli kuwa wanaoyashabikia mabadiliko haya ni kina Mama na Vijana wa eneo hilo.

Ndugu Ole Sosopi amefungua kampeni zake ktk kata ya Migoli ilipokuwa ngome ya CCM kwa miaka 20,amejizolea wanachama wengi wake kwa waume,vijana na wazee.Uwanja ulifurika watu waliojaa hamasa,wakiimba nyimbo za mabadiliko kwa hamasa kubwa,kina mama walijitolea michango yao ili kumuwezesha ktk kampeni zake.

Jimbo la Isiman ni moja kati ya majimbo masikini sana Tanzania,wakazi wake wengi wanaishi ktk mazingira magumu ya huduma za afya,maji na miundombinu.Kwa miaka 20 limekuwa kama halina msemaji ndani ya Bunge,hivyo wameazimia sasa kufanya mabadiliko ili sauti zao zisikike ndani ya Bunge na matatizo yao kutatuliwa.

Ole Sosopi ameanza kampeni ktk jimbo la Isimani,jimbo lilikokuwa ngome kubwa ya CCM na halikuwahi kuwa na upinzani mkubwa ktk kipindi cha uchaguzi kama mwaka huu.Kwa wanaolifahamu Jimbo la Isimani,hali hii na umati huu unaashiria mabadiliko makubwa ya siasa za Jimbo hilo.