Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,157
Alipoteuliwa Ole Sendeka kuwa msemaji wa CCM Niliwahi kusema hatua ambayo CCM imefikia inahitaji mtu wa aina yake.Haihitaji mtu mweledi kwa kuwa ataona aibu ya kujidhalilisha.Inahitaji mtu asiye na aibu mwenye uwezo wa kusema au kufanya lolote kwa kujitoa ufahamu hata kama anao kidogo aliobakiza. Sitaki kujadili matokeo yake yale ya kidato cha Sita ambayo C ziligeukiana katika masomo yote na kutengeneza duara masomo yote na kupata S ya General Studies tu,Hapana.Sitaki kujadili hilo
Ila angetumia hata Elimu yake ya Uraia kuelewa kwamba Udikteta ni hali ya mtu kujilundikia mamlaka na kufanya maamuzi yasiyohojika au kukosolewa huku akijitahidi kudhoofisha taasisi muhimu kama Bunge na Mahakama.Hali ya kutozingatia katiba au kufinyanga katiba iwe ya kidikteta.Huwa dikteta ni adui wa demokrasia na Vyombo vya habari ni kero kwao.Hizo ni baadhi ya sifa za madikteta
Tumekua tukikemea,kukosoa,Kulaani na kushauri kuhusu muenendo wa Utawala usifike huko. Shutuma zake kwa upinzani kuwa tunamchafua Rais Magufuli kwa kumuita Dikteta na Fashisti ni dalili za kuingiwa na Kiwewe kuhofia Ziara za Viongozi wa Upinzani kuzunguka nchi nzima inayoanza leo.
Hatutaki nchi ielekee kubaya na tusipokuwa makini na kuchukua hatua za Kumzuia Rais au kiongozi yeyote kuwa dikteta tutafedheheka kama taifa na tutaliangamiza taifa letu tukufu.
Ni watu wasioelewa vituko,madhara na kadhia ya kuulea udikteta tu anayeweza kuutetea. Na madikteta silaha yao kuu ni wananchi wanapokosa elimu ya Uraia
Kule Uganda Idd Amini alipoingia madarakani alisema atapambana na rushwa na kuirudisha nchi kwenye mstari ndipo aitishe uchaguzi.Kilitokea nini? Mzee huyu ajisomee historia au awe anajiandaa basi ili akijitoa ufahamu ajitoe vizuri bila kujidhalilisha na kuifanyia heshima yake Damage beyond recovery.
Nimekumbuka vituko vya madikteta kadhaa. Kuna huyu Ne Win aliyekuwa Rais Burma kuanzia 1962-1981. Yeye alikua anafanya maamuzi bila kuhojiwa.
Washauri wake wakuu walikuwa wataalamu wa elimu ya nyota,Unajimu na Wapiga Ramli Mashuhuri.Na hawa walikuwa Crazy kwelikweli
Alipoanza kushutumiwa kuwa Serikali yake inaegemea mno mrengo wa kushoto yaani ukomunisti aliamua kuwafuata wapiga ramli kuwauliza ni hatua gani achukue ili arekebishe mambo asiwakasirishe mataifa ya Magharibi.Wao walimshauri ageuze Barabara zote Left -Hand Lane ziwe Right-Hand Lane na yeye akakurupuka akatangazia taifa watu wote wanaotumia barabara kwa upande wa kushoto wapo Wrong Side.
Pia wakamshauri kila apitapo juu ya Daraja awe anashuka kwenye gari anavuka kinyumenyume ili afukuze mizimu mibaya inayoliandama taifa na pia awe anaogea Damu ya Nyangumi ili awe kijana zaidi. Pia walimshauri namba yake ya Bahati ni 9.Teuzi na mambo ya kiserikali alikua akifanya Tarehe 9,19,29 .H
Pia akabadili denomination ya Currency kukawa na sarafu za 15,30,45,90 na akatangaza kuwa sarafu na noti nyingine kama 100,200, kuwa sio malipo halali( Illegal Tender) na kwa kuwa Raia wengi hawakua wakihifadhi fedha benki wakafilisika ndani ya usiku mmoja na kuvunjilia mbali uchumi
Sasa kuna huyu Waziri Mkuu Mwingine wa Nchi ya Albania anaitwa Enver Hoxa. Yaani yeye aliona cheo hakimtoshi akaamua kujilundikia madaraka na kujipa cheo cha kuchekesha kweli yeye ndio akawa anaitwa "Kamaradi-Mwenyekiti-Waziri Mkuu-Waziri wa Mambo ya Nje-Waziri wa Vita-na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Watu Enver Hoxa(Comrade-Chairman-Prime Minister-Foreign-Minister-Minister of War-Commander in Chief of the People's Army Ever Hoxa)"
Alichekesha sana.Alifikia hatua ya kujijengea hekalu la Dola Bilioni 10 sawa na Sh.Trilioni 22 baada ya kuvunja makanisa 19,Masinagogi 6 na nyumba 30,000 za Raia .Baada ya kifo chake Hekalu hilo ni Bunge la Sasa la nchi hiyo na inatumika asilimia 30 tu ya jengo hilo kwa bunge zima. Kuna huyu Nicolae Ceausescu wa Romania yeye nae alivunja bunge na mahakama na amri yake ikawa ndio sheria na ndio maamuzi ya wananchi
Albania ndio taifa liloishia kuwa fukara zaidi bara Ulaya. Alipendwa kweli na mataifa ya Ufaransa na Uingereza kwa kuwa aliruhusu makampuni ya nchi hizo kupora mali kule Romania hadi Malkia wa Uingereza akampa Cheo cha Heshima .Aliitwa Sir Nicholae .Akajiongezea akajiita Geniul din Carpati au Genius of Carpathians.
Mwisho akaomba mkewe Elens ambaye ni kilaza zaidi apate fursa ya mwendokasi kufundisha New Your Academy of Science na nchini mwake akamtungia bonge la jina Comrade-Academician-Doctor Engineer. Pia akalazimisha watafiti wawe wanaongeza jina la Mkewe katika machapisho yao. Nicholae alipinduliwa na kuuawa na wananchi waliochoka udikteta wake na maisha magumu huku akiipendelea familia yake mwaka 1989
Mobutu Seseko yeye aliposhika madaraka alivunja bunge na kuahirisha kutumia katiba. Kim Jong-Un wa Korea ya Kaskazini yeye hahojiki kwa vyovyote vile.Kwanza aliposhika madaraka alimuru watu wote wenye jina kama lake wabadili na wanaume wote wanyoe kiduku kama yeye. IDD Amin Wa Uganda yeye ni funga kazi .Ndoto zake kuu ilikua kutamani kumuoa Malkia ili yeye aje awe mfalme wa Scotland
Kukosekana taasisi za kumhoji na kumshauri akaamua kujiita "His Excellency,President for Life,Field Marshal,Al Hadji,Doctor Idi Amin,VC,DSO,MC,Lord of All the beasts of the earth and fishes of the seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular".
Kwa hiyo sisi hatutaki taifa lifike huko,hatutaki Mkuu wa nchi aturudishe huko kwenye primitiveness. Ole Sendeka ajenge tabia ya kujielimisha kwanza.
Mwezi Ujao nikipata fursa nitamuazima mzee huyu vitabu "Pinochet's Diaryictator's Favorite Book", "The Rise of Totalitarianism" cha Hannah na "Defeating Dictators:Fighting Tyranny in Africa and Around the World" Cha George Ayyttey. Mzee huyu anahitaji kusaidiwa na vijana huko afanye kazi kwa weledi na sio kumuacha akadhalilike kwa matamshi yake