Ole Sabaya Yuko Wapi? Kila Mahali Haonekani!

Ole Sabaya Yuko Wapi? Kila Mahali Haonekani!

MtuHabari

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
321
Reaction score
1,020
Toka atenguliwe na itangazwe anachunguzwa DC mwenye tuhuma Ole Sabaya haonekani popote sio nyumbani sio vituo vya polisi.

Sisi watu wa habari tulitaka kufanya naye mahojiano naye kupata habari zake za ukweli tofauti na mahojiano aina ya Clouds media.

Sasa hivi Sabaya ni mtu maarufu sana hasa katika nyanja ya kuwa Mwanasiasa Jambazi hivyo kupata mahojiano naye atashare na wengine uzoefu wake kwenye nyanja hiyo.

Au naye kesha chukuliwa na watu wasio julikana?

Anayefahamu atujulishe tumfate tukamilishe lengo letu
 
Labda hajamaliza kuoga
IMG_20210514_132013.png
 
Moja ya mambo tulitaka kumhoji ni hili la ubilionea wake!
Kwamba iweje miaka 2 iliyopita alikuwa anaishi kwa kunywa bia na nyama za kukopa pale Arusha au kutumia kitambulisho bandia cha TISS na leo ni bilionea?
Alikuwa anafanya biashara gani Hai? Au mihandarati?
 
Atakuambia amefanya kazi kubwa kwa wana hai kwa kumuondoa mbowe,na atakutuhumu kuwa hilo swali umetumwa na mbowe umuulize, kwa hilo swali moja tu anaweza akamtaja mbowe mara 80
Moja ya mambo tulitaka kumhoji ni hili la ubilionea wake!
Kwamba iweje miaka 2 iliyopita alikuwa anaishi kwa kunywa bia na nyama za kukopa pale Arusha au kutumia kitambulisho bandia cha TISS na leo ni bilionea?
Alikuwa anafanya biashara gani Hai? Au mihandarati?
 
Toka atenguliwe na itangazwe anachunguzwa DC mwenye tuhuma Ole Sabaya haonekani popote sio nyumbani sio vituo vya polisi.
Sisi watu wa habari tulitaka kufanya naye mahojiano naye kupata habari zake za ukweli tofauti na mahojiano aina ya Clouds media.
Sasa hivi Sabaya ni mtu maarufu sana hasa katika nyanja ya kuwa Mwanasiasa Jambazi hivyo kupata mahojiano naye atashare na wengine uzoefu wake kwenye nyanja hiyo.
Au naye kesha chukuliwa na watu wasio julikana?
Anayefahamu atujulishe tumfate tukamilishe lengo letu
Kuna mahali walikuwa wamejifungia Jana kwa ajili ya kuanzisha topic za kujitetea as if wanaccm hawakupendezwa kwa kutumbuliwa kwake.
Ushauri wangu kama mwanaccm mwenzangu awaombe msamaha wote aliowakosea ili aweze kuwa huru ili mtaani aonekane la sivyo dhamira itamtesa sana na nwisho wake hautakuwa mzuri
 
Mungu ana makusudi mema na nchi hii. Baada ya kuona tumeteseka vya kutosha akatuondolea mwendazake.

Kisha Mungu akapandikiza roho mtakatifu kwa mama SSH, naye anaendeleza kazi nzuri ya kuondoa uozo

Mama alianza na Dr. Bashiru......out
Kakoko mbeba hela za bandari kupeleka kwa mwendazake. ...out
Dotto James aliyekuwa anachota tu mihela na kuipeleka CHATO ....out.
Biswalo aliyekuwa anawasukia watu mashitaka fake ...out
Gen. Mbung'o aliyekuwa anabambikia watu watu tuhuma za rushwa ..out
Sabaya mpenda ubabe na ujambazi...out

Kazi iendelee.!
 
Back
Top Bottom