Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,221
- 1,788
Baada ya ccm kuzidiwa kila kijiji,leo Naibu Waziri wa Ardhi Ole Medeye,akiwa na gari ya Serikali,alifika Kata ya Mbuguni,akiwa kwenye kikao cha ndani cha kutoa rushwa,ndipo wananchi waliokusanyika kumsikiliza naibu waziri,walishangaa kupewa rushwa ya shilingi 20,000,kila mmoja,badala ya kupokea wakaanza kumshambulia Ole Medeye,na kumweleza kuwa walifikiri anakuja na majibu ya matatizo yao ya ardhi na si kuwapa hela,Medeye alifanikiwa kutoroka na kukimbilia shuleni ambako umma ulizidi kumkimbiza,ndipo akaomba msaada wa polisi na aliondoka chini ya ulinzi mkali wa polisi.