Ole Medei Azimiwa Kipaza Sauti Kanisani.

Tatizo la viongozi wa makanisa siku hizi halifuati maadili ya madhehebu yao,hakuna kanisa lolote hapa duniani lenye jukwaa,katika makanisa kilichoko ni MADHABAHU,haiwezekani(Haipendezi) madhabahuni pawe sehemu ya kufanyia siasa,viongozi wa madhehebu wanaoondekeza njaa zao ndio pekee wanaokubali kuwaita viongozi(waliokua) wachafu kujisafishia katika makanisa yao.
 
Kikwete na harakati ya kuipunguza team ya Lowasa kwenye nafasi nyeti ndio imemponza Olemedeye.

huyu ni majeruhi wa uteuzi wa uwaziri ndiomaana akipata fursa ya kuongea mbele ya umma anajitahidi kutoa stress zake.
hongera sana mzee wa usharika uliyezima mic husika.


cc to Mama Yeyoo
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa nishawahi kuona video yake ya ukabila humuhumu JF nafurahi walivyomzimia hiyo maiki vinginevyo angepoteza uwepo hapo kanisani. Na hayo makanisa mengine Dah! hivi wanakosa wakualika?
 
Baada ya kutoswa kuwa naibu wa waziri wa ardhi.... sasa ni jimboni kwake

Nimesikia sasa hivi kwenye magazeti,
mh mbunge huyu amezimiwa kipaza sauti akiwa anahubiri kanisani kwenye kuchangia ujenzi wa kanisa la KKKT Arumeru na kutumia muda mwingi kuhubiri siasa na kujisifia zaidi

Ndio wakamzimia mic, sijui alikuwaje baada ya kuzimiwa, pole mh mbunge.

SOURCE: Magazeti


Huyu mtu ni mmbaguzi na hafai kuwa kiongozi ,anawagawa Watanzania hasa tamko na azimio la wazee wa kimasai na yeye ndani yake ni hatari sana na walipaswa wamfukuze kabisa basi tu kanisani sio jeshini.
 
Anahubiri siasa kanisani na kusifia utumbo alioufanya akiwa waziri? Akapimwe akilihuyu!!
 
Huyu jamaa ingekuwa kuna kufukuzwa kabila basi angefukuzwa umasai......sijui angehamia kabila gani
 
Back
Top Bottom