Old Boys wa Old Moshi Sekondari Shule Kongwe

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
20180209_154222.jpg


Kwa wale Old Boys wa Old Moshi Secondary School (Moshi Secondary School),

Bila shaka tunaikumbuka shule yetu. Shule hii pasi na shaka inastahili kutambuliwa kwamba ni Shule Kongwe. Kwa tuliosoma hapo shule hii imegusa maisha yetu. Asante sana walimu wote na wafanyakazi wengine wote wa shule hii.

Kwa harakaharaka, shule hii inatuhitaji sisi wahitimu wa zamani (alumni) tuchangie maendeleo ya hali na mali ya shule hii. Tuulize vipaumbele, na tuone wapi tunaweza kujumuika.

Kwa wale wenye fursa ya kuieleza serikali, muiombe iiweke shule hii katika mipango yake ya kuboresha shule kongwe, na kutekeleza maboresho hayo ikiwa imo.

Sote kwa pamoja tutafute namna endelevu ya kuiinua shule yetu hii maridhawa.

Mwaonaje?
20180209_153752.jpg

20180209_152859.jpg
 
Nalikumbuka bweni la Kibo 4 a lot.Pasipo kusahau mabweni ya Shengena ,kibo bungalow na mawenzi bungalow.Hakika old is Gold!
 
Yale mengine ni meru na Hanang kama sijakosea.Shambani na Leyland ilikuwa ni pale machine tools,barabara ya Machame.Hakika ulikuwa ni wakati mzuri!
 
Shambani na Leyland ilikuwa ni pale machine tools,barabara ya Machame.Hakika ulikuwa ni wakati mzuri!
 
Huu uzi ni maalumu kwa wahenga .

Ukitembelea DH, Madarasa, Vyoo hadi Mabweni ukaipata historia na mchango wake hapa Tz utasikitika sana.
 
Shengena 1 bweni langu.... Daa nlipigwa suspension kisa mgomo, ila nimewamiss watoto wa ushirika na club Alberto, kila nkienda likizo marangu lazima nifike old kucheki mazingira
 
Back
Top Bottom