Okoa mtoto huyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Okoa mtoto huyu

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Kaitaba, May 18, 2011.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukifika getini muhimbili national hospital, utakuta mama mmoja kichaa mweupe hivi kiasi, sio mchafu sana kama vichaa wengine, ila anafanya vituko kama wafanyavyo vichaa wengine.

  Tatizo langu, amebeba mtoto mdogo mgongoni, na wakati mwingine huwa anamuacha peke yake wakati anapoenda barabarani kufanya vituko vyake.

  Nawaomba wote wanaohusika na haki za watoto wamchukue huyu mtoto jamani.
   
 2. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukifika Muhimbili hosipital, MNH kwenye lango kuu, kuna mwanamama mmoja kichaa, cha hajabu kabeba mtoto mgongoni, na wakati mwingine huwa anamuacha peke yake pindi anapoingia barabarani kufanya vituko vyake.

  Kinachoniuma ni huyu mtoto, maana jua lake, mvua yake na sijui kama anapata chakula.
  Nawaomba wanaohusika na haki za watoto watembelee hapo wamnusuru huyu mtoto.
   
 3. VISIONEER

  VISIONEER Senior Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huwa naingiwa na roho ya huruma inapokuwa ni suala la mtoto aliye katika mazingira magumu, tatizo la nchi yetu umasikini umezidi utamsaidia mtoto yupi umwache yupi na kama ni MUHIMBILI we unafikiri hawajamuona huyo mtoto. Kwa nchi zilizoendelea council inamchukua mtoto wa namna hiyo na kumtunza. Lakini kwa tanzania sidhani kama kuna utaratibu huo.   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mie nafikiri at one stage, kuna haja ya watu wenyewe kujitolea ku adopt watoto wa aina hiyo, tatizo nchi yetu na watu wake wabinfsi saana.
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,774
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 180
  usiseme hivyo. Kuna wengine ni uwezo tu hauruhusu.
   
 6. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,743
  Likes Received: 832
  Trophy Points: 280
  waziri wa watoto yuko wapi?
   
 7. N

  Nebukadreza New Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wanaohusika kuwasaidia wanaohitaji msaada ni pamoja na wewe, tatizo letu wa tz tunataka watu fulani au serikali ndio itoe msaada, kumbuka kutoa ni moyo na hakuna binadamu asiye na uwezo wa kutoa kwa nafasi yake. hebu fikiria unatumia sh. ngapi kunywea bia,kuhonga,kutoa ofa kwa washikaji. hebu anza wewe na mungu atakulipa
   
 8. N

  Nguto JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,274
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Tatizo kuadopt mtoto kuna procedures "cumbersome" ile mbaya eti wanataka kujiridhisha kuwa mtoto hatapata shida. Namjua mtu alijaribu akaacha baada ya kukumbana na utaratibu huo ambao ni mrefu sana.
   
 9. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nnaamini government yetu inauwezo mzuri tuu wa kuweza kushughulikia tatizo hili la watoto wa mitaani wala hakuna haja ya wananchi kujitolea...
   
Loading...