OILCOM Tabata Segerea mmezidi jamani!

Mimi siangalii mita naangalia mkono akiweka hakuna kuachia ama kubonyeza mpaka yakatike. Yakikatika ndio nasoma mita. Nafanya hivyo kwa kumuonuesha kabisa kwamba namtazama kwa makini. Huwa wanaogopa sana.
 
Jipe pole mwenyewe. Mi nakaba hadi penalty hawaniwezi hao wezi wako.

Pale ambapo huo mpira hutokea kuna wakati usipokuwa makini jamaa anabonyeza na mita husoma haraka na ndo umeshaibiwa!! Urefu wa kamba!!!!
 
wakuu hawa jamaa naona kuna jinsi wanavyocheza na ile pampu ya kuwekea mafuta imenitokea mara mbili oil com ya kipawa na total yapale banana ,nimeweka mafuta ya 30,000 kutoka banana na natumia alteza kufika vingunguti taa inawaka na kulikuwa hakuna foleni na wakati anaweka nilikuwa naangalia kabisa
 

Alteza baadhi zinabugia mafuta hasa za four cylinder
 
Shell ni kampuni la mafuta la kiitaliano, lilikuwa na vituo vingi vya mafuta nchini kiasi kwamba watu wakahisi vituo vya mafuta vinaitwa shell. Kwa sasa sijui kama wana tena vituo hapa nchini ila wanauza vilainishi.
 
yaani ile oilcom petrol station ni balaa, nakushauri kaweke mafuta lake oil, we chunguza tu utaona watu wana ruka ile oil com wanaenda pale lake oil sanene kupanga folen.
mi nshalizwa si chini ya mara tatu maana naishi jirani na hapo.
 
Shell ni kampuni la mafuta la kiitaliano, lilikuwa na vituo vingi vya mafuta nchini kiasi kwamba watu wakahisi vituo vya mafuta vinaitwa shell. Kwa sasa sijui kama wana tena vituo hapa nchini ila wanauza vilainishi.

Walishafungasha Virago hapa, nimewakuta Uganda.
 
Bodaboda na washikaji zangu pale Rose Hill ndiobwalinitonya juu ya Oilcom Segwrea kuwa wadokozi wa mafuta.
sawa na Camel pale Sanene jirani na kwetu pazuri,,the same drama....udokozi japo nasikia hivi karibuni wamejirekebisha.

LakeOil nasikia si wadokoZI,MAHILI ILA WAZEMBE NA WAVIVU, JUZI NIMEKWAZIKA KWA UJINGA WA DADA MUHUDUMU
 
Point of correction.

hakuna eneo la kijiografia au la kiutawala linaloitwa Tabata Segerea.
Tabata ni Tabata, Segerea ni Segerea.

Kata ya Tabata, Kata Ya Segerea
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…