Oh, weekend imeshawaendea vibaya!

Oh, weekend imeshawaendea vibaya!

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,447
Hata hawakutarajia ingekuwa hivi!

Wengine hata najua wazi hawana taarifa na kinachoendelea juu yao. Lakini kaamua, liwalo na liwe.

Mmefanya vema mliofanikisha juhudi za kumpa majina ya ziada; atakuwa aliudhika kukuta aliowaamini nao ni nyoka.

Kafanya jambo jema; lakini kama atafanya hivi bado wale jamaa watalegeza kamba? Kuongezeka kwa watuhumiwa kutaleta neema kwetu kama nyumba?

Naam, weekend imewaendea vibaya; ambao hawakutarajiwa ndo watalia na kusaga meno. Mwaka unaisha vibaya kwao!

Lakini, kilio chao ni kicheko cha wengine! Wenye macho wameona... Wengine vaeni miwani mtaweza soma!
 
Mkuu Invisible: Lifunue na umwage hapa. Hakuna wa kutuhukumu!!!!!!
 
Nasubiri kupambazuke,nitakuta mwezi umeondoka na jua limechomoza huku giza limetawanyika
 
Lakini, kilio chao ni kicheko cha wengine! Wenye macho wameona... Wengine vaeni miwani mtaweza soma!
Invisible;

  1. Kilio au kicheko vyote vyangu.
  2. Ninayo macho, bahati mbaya sijaona.
  3. Navaa miwani, lakini sijaweza kusoma.
Vyovyote viwavyo, weekend njema.
 
Last edited by a moderator:
Amechelewa sana jumapili uchaguzi serikali za mitaa wangetumia kama hoja ya kuombea kura the damage has been done!

Afanye tu kuwafurahisha wafadhili hao ndo wanaogopwa kwa sasa kuliko wananchi na bunge lao!
 
Seth hakanatikia hata kwa dawa

WALE JAMAA WA whitehouse watapumzishwa huku wakiendelea na fedha za esrow
 
Better late than never.

Hata hivyo, nae wanaweza kuja kumlipua mbele ya safari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom