Chief bachelor napita. Uwe kwenye ndoa, uwe peke yako kama hujajiunganisha na wewe mwenyewe upweke utakutafuna, kuna saa utalia, kuna saa utatamani utoke ndoani, kuna saa utatamani uingie ndoani.
Upweke ni episodes na si full time life experience. Ukimkuta full time loner huyo ni mgonjwa wa akili; hata ndoani wapo.
Kuogopa uzee wa peke yako ni woga tu. Wee sasa hivi waza ukizeeka utakula vipi, utatibiwa vipi na utalala wapi kwa jasho lako. Hesabia watoto au mwenza at your own risk. Kuna field marshal mmoja wa kike dar amefariki hivi karibuni akiwa na miaka 93 lakini hakuwahi kupungukiwa katika uzee wake. Alikuwa na watu hata wasio ndugu waliokuwa wakimtunza, alikuwa ameajiri dereva wa kumpeleka anakotaka, mtu wa kumfanyisha mazoezi ya viungo n.k. Swala ni umecheza vipi ligi yako.
Kuchanganya kuosha vyombo na ndoa au ubachela ni udhaifu katika kupambanua. Mimi ni chief bachelor lakini sifui wala kuosha vyombo. Kuna wanandoa hawafui, kuna wanaofua. Kupika, kufua au kuajiri mpishi au kula magengeni ni uchaguzi binafsi, ni life style ya mtu. Kuhusianisha kazi za nyumbani na kuoa ni kusema mwanamke anaolewa ili akafulie au kupikia mwanaume tafsiri ambayo haina tofauti na ujakazi.
Kusema wanaume wasiooa hawawezi kupewa majukumu makubwa yakiwemo kuongoza nchi kwa sababu wameshindwa kuongoza familia ni ufinyu wa fikra uliosababishwa na jamii kuwaza ngono na kutotambua maana na thamani ya kiongozi. Kuna field marshall kusini mwa afrika anaongoza nchi vizuri tu, nchi ndogo lakini inaongoza ku-export nyama ya ng'ombe wakati idadi yao ya ng'ombe ni chini ya robo ya ng'ombe wetu, na kuna mwanaume mwanandoa mmoja kwenye nchi nyingine hapa hapa kusini mwa jangwa la sahara ananyanyasa mke, kazaa na mtoto aliyekabidhiwa amlee, ana hasira balaa lakini kapewa nchi anaongoza. Pia asilimia kubwa ya wanawake waliofanikiwa hata katika uongozi ni field marshals au divorcees lakini wao wanaitwa women of substance. Double standards.
Binafsi naheshimu waliochagua ndoa na waliochagua kuwa peke yao. Yote ni maisha mazuri na changamoto zake ni zile zile japo zinaweza kutofautiana sura, mfano, wote wanakabiliwa na changamoto za committment na uaminifu kwenye machaguo yao. Sitaponda ndoa kwa sababu nimeona ndoa zenye machungu na mahangaiko mengi (nimewahi kufanya hivyo) kwani zipo nzuri, na sitaponda wanaoishi peke yao kwani wapo wenye amani sana. Wote wanahitaji kitu kimoja tu: kulenga vitu vya thamani kwenye maisha. Ukipita njia ya ndoa, huyu akapita isiyo ya ndoa makutano ni mamoja. Afterall siku ya mazishi hali ya ndoa hutajwa kwenye mstari mmoja tu "marehemu ameacha mja/gane na m/watoto kadhaa. Vile vinavyochukua sehemu kubwa ya wasifu wa marehemu ndo vya muhimu. Hivyo tunaondoka navyo.