Ofisi za watendaji wa mitaa kutoza asilimia 10 za mauzo ya viwanja/mrahaba bila kutoa risiti, manispaa zinahusika?

kijanamdogo

JF-Expert Member
Feb 25, 2018
231
176
Wadau kwa aneelewa utaratibu sahihi wa kununua kiwanja /shamba lisilopimwa na kwenda kuandikiana Ofisi ya Serikali ya mtaa .

Binafsi nimebaini kuwa SERIKALI za mtaa ambazo ziko chini ya Halmashauri hutoza fedha kwa WANANCHI wanaofika pale kuandikiana kwa gharama ya asilimia 10 ya MAUZO fedha ambayo haitolewi RISITI.

Najiuliza je Kiwango cha asilimia 10 kipo kisheria ? Je kwanini hizo fedha hazitolewi RISITI?

Ile ni Ofisi ya Serikali kwanini watendaji wa SERIKALI wanawatoza fedha WANANCHI na Halmashauri husika haitoi RISITI?
 
Kwa uelewa wangu, tozo ya asilimia kumi haipo kisheria isipokuwa ni taratibu serikali za kijiji/mtaa wamejiwekea.

Hiyo pesa huwa wanagawiwa wajumbe serikali ya mtaa.

Wale wajumbe huwa wanakuwa kama mashahidi kwa pande mbili mlizokubaliana kuingia makubaliano ya mauziano.

Faida kubwa ya kutoa hiyo asilimia kumi ni kuwa kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kama utapeli au kuuzwa kwa shamba zaidi ya mara au kwa zaidi ya mtu mmoja, wanasaidia endapo watabaini unaingizwa chaka watakujulisha ingawa wapo wajumbe wa mitaa matapeli pia, ila kikubwa pia hata ikitokea utahitaji kwenda mahakamani au mabaraza ya ardhi wakati kuna mgogoro huwa wanasaidia sana.

Kabla ya kutoa hiyo asilimia kumi hakikisha unajiridhisha vya kutosha makubaliano au biashara unayoifanya.
 
Exactly
 
Daaa umemjibu vizurisana
 
Mleta uzi alilenga kujua, "kama kitendo hicho ni kosa ama sio kosakisheria" basi.

Masuala ya mazoea ama utaratibu wamejiwekea ni "Afterthoughts" ambayo hutegemea jamii/kabila husika. Ila HOJA YAKE NILIVYOELEWA MM, je ni kwa mujibu wa sheria ama la??

JIBU: Ni kosa kisheria (chini ya kifungu cha 31 cha sheria ya Rushwa Na. 11/2007.

Pia kwa kuwa wengi tumezoea kutumia WENYEVITI WA VITONGOJI NAO HAWAHUSIKI ANAEHUSIKA NI VEO. Rejea hii hukumu ya hapa.

Kwa kuwa waTZ tuna historia ya UVIVU wa kosoma hasa maandishi marefu bas NENDA 1 kwa 1 ukurasa wa 11 wa hukumu hii. View attachment Land case - No. 50 of 2016.pdf
 
Mimi binafsi huwa napinga sana kitendo hicho kwan kimeachwa bila kuchukuliwa hatua, na madhara yake kinakosesha Halmashauri ya kijiji husika Mapato.

NINI KIFANYIKE?
Suala sio kupinga tozo HAPANA. Kinachotakiwa kufanyika, H/Kijiji ndo msimamizi wa Ardhi ya Kijiji kwa mujibwa wa Sheria Na. 5/1999, so inatakiwa kutunga SHERIA NDOGO (By laws) ambazo zitaweka utaratibu wa kuuza na kununua Ardhi ya kijiji pamoja na kuweka tozo % ya mauziano, halaf pesa hiyo inaingia kwny mfuko wa kijiji km mapato ambayo yangetumika kujenga vyoo mashulen (S/M) n.k

N.B Sheria ndgo za Kijiji hutungwa na wajumbe wa H/K na kupitishwa na Baraza la Madiwan la H/W.

TATIZO LIKO WAPI?
1. Uelewa mdgo wa watendaji wa H/kijiji (wengi wao ni STD VII na form 4 with certifiacte)
2. Uzembe wa H/W husika kuwapa Elimu (Capacity building) kwa hawa watumishi wa H/Kijiji.
 
Kwa uelewa wangu, tozo ya asilimia kumi haipo kisheria isipokuwa ni taratibu serikali za kijiji/mtaa wamejiwekea.

Hiyo pesa huwa wanagawiwa wajumbe serikali ya mtaa.

Wale wajumbe huwa wanakuwa kama mashahidi kwa pande mbili mlizokubaliana kuingia makubaliano ya mauziano.

Faida kubwa ya kutoa hiyo asilimia kumi ni kuwa kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kama utapeli au kuuzwa kwa shamba zaidi ya mara au kwa zaidi ya mtu mmoja, wanasaidia endapo watabaini unaingizwa chaka watakujulisha ingawa wapo wajumbe wa mitaa matapeli pia, ila kikubwa pia hata ikitokea utahitaji kwenda mahakamani au mabaraza ya ardhi wakati kuna mgogoro huwa wanasaidia sana.

Kabla ya kutoa hiyo asilimia kumi hakikisha unajiridhisha vya kutosha makubaliano au biashara unayoifanya.
Unaepushaje migogoro wakt viongozi wa Vitongoji hata kumbukumbu hawatunzi???. After 7 yrs barua ya mauziano HAIONEKANI. Aliyekusaini akimwaga uga cheo basi ndo mwsho wa taarifa zako.

Pia vijiji vingekuwa vinapata mapato kupitia hizi tozo badala ya kuishia mifukoni mwa watu.
 
Back
Top Bottom