Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) yakiri ajira sekta binafsi zimepungua kwa 42.6%, serikalini zimepungua kwa 78.1% ndani ya mwaka mmoja

Sijui wewe unasoma mambo namna gani jamani. Unarudia lile lile nililokanusha. Unalinganisha ajira za sekta binafsi na serikali, wakati mimi nakwambia ni ulinganisho baina ya ajira za sekta binafsi na zile za kwenye makampuni yanayojenga hiyo miradi mikubwa.

Halafu unaposema kuwa hiyo miradi mikubwa zinatoa ajira chache, unakuwa unapingana na takwimu ambazo ziko wazi kabisa kwenye hiyo chati ya NBS!

Kuelewa maandiko ni tabu??
 
Sio kwamba sijakuelewa ila wewe hujaelewa au hujaona mantiki ktk hoja zangu.
Kuna sehemu hapo nimekuambia udanganyifu ulikuwa mkubwa sana miaka iliyopita.
Idadi unayo iona sasa ya ajira binafsi na ajira zitokanazo na miradi mikubwa ya maendeleo ya serikali ndio takwimu ambazo zina uhalisia kutokana na ukali na umakini wa serikali ya sasa.
Na hizo takwimu za miaka ilyopita kama 2013/14 hazina uhalisia sababu waliajiriwa wengi na serikali haikuwa na taarifa sahihi.
Hiyo ilisababishwa na waajiri na wakati mwingine waajiriwa kuomba wasiwekwe kwenye mfumo rasmi wa pension na ulipaji kodi ya PAYE.
Nikakupa mifano ya watu kulipwa commissions na consultancy fee.
Nina ushahidi wa watu wengi sana kuajiriwa sekta binafsi huku walikuwa hawalipi kodi na makato ya pension funds. Hawakuingizwa ktk kumbukumbu za serikali hawakulipa mikopo ya elimu ya juu. Ukiachana na hao wa wasomi elimu ya juu wengine wengi wa elimu ya stashahada hadi wasiosoma kabisa lakini walistahili kuingizwa ktk rekodi za serikali na kulipa kodi hawakuingizwa taarifa ktk mifumo ya serikali.
Hiyo idadi unayo iona hapo ktk chati ya miaka ya 2015 kurudi nyuma ni robo ya watu halisi walio ajiriwa miradi mikubwa sekta binafsi na miradi mikubwa ya maendeleo inayotoa pesa serikalini.
Shida ni wewe kutonielewa sio mimi kuto kukuelewa.
Pia hao sekta binafsi wengi walikuwa wanaingiza pesa nyingi sana tofauti na iliyokuwa inajulikana ktk rekodi za serikali.
Ushahidi wa haya niyasemayo ni ile taarifa iliyopo ktk flash disk ya Mh. Raisi aliyokuja nayo kwenye kikao chake na wafanyabiashara wakubwa toka kila wilaya. Benki ipo ripoti tofauti ya hesabu za ukaguzi na ya TRA.

Ushahidi wa pili ni ile taarifa ya HESLB ya wadaiwa sugu iliyotoka karibuni. Wadaiwa waliofikishwa mahakamani ni chini ya 8 wakati hali halisi kwenye makabrasha yao wapo wengi. Hawa 8 ni wale tu waliokuja kunaswa baada ya kuingia ktk mifumo ya serikali sasa baada ya ajira mpya au waajiri kuwaingiza sasa. Kiuhalisia wapo wengi huku mitaani waliokuwa wanalipwa mamilioni na hawapo ktk walipaji wa mikopo au kodi za serikali wala hawakuwepo ktk kumbukumbu za wizara ya kazi na ajira.
Wengi walioweza wameenda nchi za jirani kama DRC, n.k.
MY POINT IS 'HIZO TAKWIMU ZA ZAMANI SIO HALISI' sababu NBS vyanzo vyao vya takwimu ni toka ktk mifumo rasmi ya serikali ambayo haikupewa taarifa zote na halisi toka sekta binafsi.
Hiyo chati nusu ina tawimu halisi na nusu nyingine sio kamili ni zenye mapungufu. Serkali ilikuwa imelala.
Kwa kutumia chati hiyo kutafsiri kilichomo ni kweli upo sahihi yote usemayo lakini huku mtaani kuna takwimu halisi zisizo ongopa ktk maisha halisi ya wengi.
 

Sawa; nimekuelewa na samahani! Ila sasa uchumi huo wa kudanganya namba ndio tunaoupinga sasa
 
Sawa; nimekuelewa na samahani! Ila sasa uchumi huo wa kudanganya namba ndio tunaoupinga sasa
Ni kweli kabisa.
Huo uchumi mbaya na mbovu sana.
Tungewndelea kuwa nchi masikini sana na tofauti ya masikini na matajiri ingekuwa kubwa sana.

Huduma za afya, maji safi na elimu kwa masikini ilikuwa ni kama anasa sio mahitaji ya lazima.
 
Kuchumia tumbo yataka moyo maana lazima wajitoe ufahamu then wauvae unafiki na ubinafsi.
Tuna safari ndefu sana tuendako hasa unapokuwa na watu wa namna hii.
Wanachosahau ni kuwa "There is no permanent situation"
 
Namba hazidanganyi you have to call aspade a spade, eti soma takwimu kwa furaha mbona unaleta siasa kwenye namba?
 
Kwa tafsiri rahisi ni kuwa kwa sasa Serikali yetu ni tajiri kuliko watu wake ndio maana inamudu kuijenga nchi kama tunavyoona au?
Ni mikopo, na tutalipa mpaka vitukuu vyetu waliopo Serikalini wanakopa na pia wanachukua 10% kwenye miradi hiyo tutakao umia ni sisi ambao hatupo Serikalini wenyewe wanafaidika na 10% ya kila mradi au ununuzi wa ndege
 
IKulu wamezifunga NGOS 148.

Hawa jamaa ndio real ya definition ya mwenye shibe
 

Uchumi unakua kwa kasi sana!

Awamu bora kabisa ya Tano!

Buuaaaaaah
 
Huu ni ushauri wa mwaka. Big up comrade
 
Wanaosema serikali imeongeza ajira wasome taarifa hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…