Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Soweto mjini Moshi yateketezwa kwa moto

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Watu wameipiga moto ofisi ya mtendaji wa kata ya Soweto mjini Moshi na kuteketeza vyote vilivyokuwepo ndani.

========

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, amesema watu kadhaa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa tuhuma za kuchoma moto ofisi ya Kata ya Soweto iliyopo Moshi.

Awali tukio hilo liliripotiwa kufanywa na watu wasiojulikana, ambapo wamechoma moto ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Soweto usiku wa kuamkia jana Novemba 10, 2019, ambapo pia wamechoma nyaraka zilizokuwa ndani ya ofisi hizo.

Mkuu wa Mkoa Anna Mghwira, amesema kuwa moto huo ulianza majira ya saa 7 usiku, na baada ya moto huo kuwaka majirani waliokuwa karibu na ofisi hiyo walianza kuuzima na baadaye kutoa taarifa polisi.

Aidha Anna Mgwhira amewataka wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi.

Moto Moshi.jpg


Moto Moshi 2.jpg

Pia, soma:

 
Juzi ililetwa habari mashamba ya mtendaji wa kata yaneteketezwa
Wapinzani wakafurahi sana
Leo tena wanafurahi

Je mtaweza kuhimili mapigo?

Tusiwaumize watu wasio na hatia Kwasababu ya ulafi wa madaraka kwa mtu mmoja

Watanzania tupendane tuache Chuki
Umekuwa ukishabikia upumbavu wa CCM leo unahimiza kuacha chuki wakati mmejaa chuki hadi kwenye kope?
 
Wale woooooote mliowakata kugombea hamjawaumiza bila hatia?

Wafuasi wao mliowazuia kuchagua wanaowataka hamjawaumiza bila hatia?

Nyie mnapendana na wanaokuwa opposite na nyinyi?

Kwa mliyoyaanzisha na mnayoyashabikia mnajenga Taifa lisilo na Upendo kabisa. Sahau kuhusu upendo tena.

Hivi aliye mlafi wa madaraka hapa ni nani mkuu?

Muhimu kujiandaa Kwa yatokanayo Tu sasa
Juzi ililetwa habari mashamba ya mtendaji wa kata yaneteketezwa
Wapinzani wakafurahi sana
Leo tena wanafurahi

Je mtaweza kuhimili mapigo?

Tusiwaumize watu wasio na hatia Kwasababu ya ulafi wa madaraka kwa mtu mmoja

Watanzania tupendane tuache Chuki
 
Juzi ililetwa habari mashamba ya mtendaji wa kata yaneteketezwa
Wapinzani wakafurahi sana
Leo tena wanafurahi

Je mtaweza kuhimili mapigo?

Tusiwaumize watu wasio na hatia Kwasababu ya ulafi wa madaraka kwa mtu mmoja

Watanzania tupendane tuache Chuki
Mmeinjinia uhalifu sasa unaanza ku-backfire mnasingizia upinzani mnalo hilo kama nawaona the Hague.
 
Back
Top Bottom