Ofisi ya msajili wa vyama na madudu yake.

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Nimekuwa nikipitia kwenye website ya msajili wa vyama vya siasa hapa nchini,na baada ya kufanya peruzo nimekuta mambo ya ajabu sana sana .

kwanza ni juu ya majina ya viongozi wa vyama vya siasa -ambao kimsingi hawapo kwenye vyeo vyao ila bado msajili anawatambua.

Hili limenistua sana na inawezekana kabisa kuwa kama mambo yanaweza kuwa hivyo kwenye nchi hii basi taifa hili liko kwenye wakati mgumu sana na haswa ikizingatiwa kuwa tunashindwa hata kufanya masuala ya kimsingi.

Kuna kila sababu ya kuliangalia hili kwa umakini mkubwa sana kwani kama ofisi ya msajili ina mtu aliyeajiriwa kwa ajili ya kuangalia website yao na mpaka sasa anawatambua viongozi ambao wengine ni wafu na wengine hawapo kabisa kwenye hivyo vyama ni aibu na huyo mwajiriwa anapaswa kufukuzwa kazi kutokana na kosa la uzembe mkubwa na uliokidhiri.

pitieni kiambatanisho chini.
 

Attachments

  • ORODHA YA VIONGOZI WA KITAIFA.pdf
    34.3 KB · Views: 242
Kama tukiacha ofisi zetu zikafanya kazi kwa utaratibu huu inaweza ikafikia mahali siku moja tukajikuta kwenye nyaraka zetu Rais wa Nchi bado ni Nyerere kama ilivyo kwenye nchi za ulaya wanaotambua Tanzania kama Nyerere Country.
 
Mpaka Kieleweke,

Unashangaa nini hapa? Tanzania na sisi Watanzania ni wababaishaji tu kwenye mambo mengi. Pitia website hata za mashirika binafsi, tena ya maana utakuta ubabaishaji huo huo.

Halafu utamkuta Mtanzania anaona mtu kama hana website basi huyo mbabaishaji. Mimi hubaki kucheka tu.

Kama huwezi kuitunza website yako afadhali usiwe nayo. Angalia links mbalimbali unakuta zinaenda kusiko na kitu.

Mimi nafikiri labda tuanze kuchapana viboko kwi kwi kwi!!
 
Kama tukiacha ofisi zetu zikafanya kazi kwa utaratibu huu inaweza ikafikia mahali siku moja tukajikuta kwenye nyaraka zetu Rais wa Nchi bado ni Nyerere kama ilivyo kwenye nchi za ulaya wanaotambua Tanzania kama Nyerere Country.

Ndiyo, nchi imejaa uswahili, ila Tanzania kuitwa Nyerere Country si kwa kutokujua ila ni kuonyesha kuwa Tanzania bado hajaweza kupata kiongozi mbadala wa kiwango cha Nyerere.
 
website za tz haziko updated, mashirika makubwa kama breweries hayana website. hata vyama vya siasa havi update website zao.

jamii forum inajitahidi....
 
website za tz haziko updated, mashirika makubwa kama breweries hayana website. hata vyama vya siasa havi update website zao.

jamii forum inajitahidi....

Huu ni ugonjwa mkubwa sana Tanzania, kuanzia serikalini mpaka sekta binafsi
 
Mnashangaa hilo mbona ni dogo? Website ya kikwete/shein waziri mkuu ni Lowasa mpaka sasa na shughuli za maendeleo zilizopo ni zile alizofanya Lowasa? Hii ina maana kuwa Pinda toka alipoingia madarakani hakuna cha maana alichofanya ili kiingizwe kwenye mtandao. Sijui kwa nini tunadakia vitu ambavyo hatuna uwezo navyo kuviendeleza au ndio njia ya kula hela za kumaintain website wakati hakuna kinachofanyika? Pia wakuu wa idara husika inaonekana hawapitii website zao kujua kama taarifa sahihi na update zimewekwa huko.
 
Back
Top Bottom