Ofisi ya CAG ifutiliwe mbali

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Kutokana na mambo kadha wa kadha kufanywa na ofisi hii ikiwemo ukaguzi wa hesabu za serikali bila kuwepo udhibiti wa wizi kwenye ofisi zetu za umma, basi nilikuwa naonelea kufutwa kwa majukumu ya CAG na kuondolewa mara moja kitengo hicho serikali.

Sababu kubwa ni kuwa ofisi hii imekuwa kama inatuambia Watanzania tunaibiwa ila hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya wahalifu hawa.

Mathalani wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya CAG hivi karibuni jeshi la zimamoto lilishiriki kupitishia fedha ambazo si za umma kwenye akaunti zake hivyo kuleta taswira ya uhalifu wenye sura wa kutakatisha fedha.

Licha ya taarifa zote za uhalifu na ubadirifu huu mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa mbali ya baadhi yao kutajwa mpaka majina ama vyeo vyao akiwemo Mhasibu wa jeshi la zimamoto, afisa maduhuli wa TANAPA, wizara ya mali asili na utalii, Clouds Media, TBC, wasafi media n.k. na wote wamepokea fedha haramu. Nchi ya kipumbavu sana hii.
 
Kikubwa jinai haiozi. Ssi tunatunza mafile tu. Siku yao hao majizi itafika. Hata kama wamekufa tutachukua mali walizoacha.
 
Wewe hata hujui kazi ya CAG. yeye anatoa recommendation after audit.

Kama kuna watu wa kufukuzwa powa, wa kubaki powa.

Lakin its down to central goverment kufanyia laxi hayo mashauri au lah.
 
CAG ni kama mbwa asie na meno, anabweka kutisha wezi lakini wezi wameshamzoea wanaendelea kuiba tu ajabu na sisi tunashangaa tu tunavyozidi kuibiwa.
 
CAG ni kioo Tu chief, kinaonyesha uchafu ulipo, Ila kazi ya kuutoa uchafu ni juu yako ewe mwananchi kupitia serikali yako uliyoiweka madarakani Kwa mjibu wa katiba. Kimsingi mchawi hapo ni katiba , full stop
 
CAG ni kama daktari wa hospitali anayekuambia unaumwa nini na dawa za ugonjwa wako ni upi ila wewe utajua pa kuzipata na kama utazitumia au hutazitumia ni juu yako.
CAG ni kama mbwa asie na meno, anabweka kutisha wezi lakini wezi wameshamzoea wanaendelea kuiba tu.
 
Back
Top Bottom