Ofisa Mtendaji adaiwa kumpa mimba mwanawe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,795
2,000
MKASA wa mwanafunzi wa Kidato cha Pili kukatiza masomo yake, umechukua sura mpya, baada ya baba wa kambo, Ignas Katula kutuhumiwa kumpa ujauzito.

Mtuhumiwa huyo ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mirumba Kata ya Kibaoni wilayani Mlele mkoa wa Katavi.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16, alikuwa akisoma Shule ya Sekondari Kibaoni Kata ya Kibaoni.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Focus Malengo alithibitisha tukio hilo. Amesema mtuhumiwa amekamatwa na yuko Kituo cha Polisi Inyonga, akiendelea kuhojiwa.

Kesi hiyo itapelekwa mahakamani baada ya upelelezi wa shauri hilo kukamilika.

Akizungumza na HabariLeo kwa njia ya simu, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaoni, Alicko Kaminyoge alisema mwanafunzi huyo alibainika kuwa mjamzito baada ya kufanyiwa vipimo katika Kituo cha Afya Usevya.

Baba mzazi wa mwanafunzi huyo, amevalia njuga suala hilo na anataka mtuhumiwa afikishwe mahakamani. Alisisitiza kuwa shauri hilo haliwezi kuisha kwa maelewano nje ya Mahakama.

“Tulipobaini ni mjamzito, taarifa ilitolewa katika Kituo cha Polisi Kibaoni kwa hatua zaidi za kisheria. Pia taarifa ilitolewa katika Ofisi ya Ofisa Mtendaji Kata Kibaoni”, alisema Kaminyoge.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mirumba, wakiwemo majirani, walidai kuwa mtuhumiwa baada ya kubaini mtoto huyo ana ujauzito, alikuwa akihaha kumtoa ujauzito huo ili kuvuruga ushahidi, lakini alikwama.

“Hata hivyo jitihada zake hizo ovu ziligonga mwamba baada ya binti yake wa kambo kumkatalia, akidai kuwa anaogopa kufa iwapo atajaribu kutoa,”alisisitiza mtoa taarifa, ambaye ni ndugu wa karibu wa mama mzazi wa binti huyo.

Kwa upande wao, mashuhuda kutoka eneo la tukio, walidai kuwa mtuhumiwa huyo amemweka kinyumba mama mzazi wa binti huyo kijijini Mirumba, baada ya kuachana na mumewe.

“Msichana huyo aliendelea kuishi na mama yake mzazi kijijini Mirumba huku baba yake mzazi akiishi mjini Mpanda, lakini alipotaarifiwa kuhusu mkasa huu alilazimika kuja kijijini hapa na kumchukua binti na kwenda kuishi naye Mpanda baada ya kuripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Kibaoni”alisema mtoa taarifa.

Ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo, alikamatwa na kushikiliwa kituoni hapo kwa saa kumi na mbili na akaachiwa huru kwa dhamana.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Katavi, zimethibitisha kuwa mtuhumiwa huyo juzi alikamatwa na baada ya saa 12 aliachiwa kwa dhamana.

“Lakini jana saa saba mchana mtuhumiwa huyo alikamatwa tena kwa mara ya pili na kusafirishwa hadi mji mdogo wa Inyonga ambako yupo mahabusu” alisema Ofisa wa Jeshi la Polisi, ambaye hakutaka majina yake yaandikwe gazetini, kwa kuwa si msemaji.

Inadaiwa mtuhumiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa mara ya pili, kufuatia shinikizo la baba mzazi wa binti huyo, aliyetishia kufungua mwenyewe mashitaka mahakamani.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mirumba, Japhet Bundara alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ikiwa ni mara ya pili.

“Leo (jana) wakazi wa kijiji hiki walijitokeza kwa wingi wakishuhudia mtuhumiwa akipandishwa kwenye gari la polisi lililomsafirisha hadi mji mdogo wa Inyonga ambako yupo mahabusu... Kwa kweli sijui kwa undani mahusiano baina yake mtuhumiwa na mama mzazi wa binti huyo,”alisisitiza.
Awali, Jumatatu wiki hii gazeti hili liliripoti habari ya binti huyo aliyetoroka kuozwa, amepachikwa mimba.

Alikimbia tukio la kuozwa akiwa na umri wa miaka 12. Lakini, miaka minne baadaye alipachikwa mimba na mtuhumiwa huyo, ambaye ni baba wa kambo.
Mwanafunzi huo alikuwa akiishi na wazazi wake katika Kijiji cha China wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Mwaka 2013 akiwa darasa la sita Shule ya Msingi kijijini hapo, aligundua baba yake mzazi alikuwa na mpango wa kumuozesha kwa mfugaji mwenye umri mkubwa, hivyo alitoroka kwao.

Baada ya kutoroka kwao, alikimbilia Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nkasi mjini Namanyere, akimtuhumu baba yake mzazi kuwa na mipango ya kumuozesha kwa mfugaji mkoani Shinyanga kwa mahari kati ya ngo’mbe 40 na 50.

Ilidaiwa kuwa baba yake, alitumia mbinu ya kumhamishia binti yake huyo mkoani Shinyanga, kwa madai kuwa ataendelea na masomo yake huko, kumbe lengo lake ni kumuoza.
 

chipalila1

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
258
225
Hizi habari zikitoka zinavuta hisia za watu sana. Afisa Mtendaji ni mtuhumiwa hajathibitika kutenda kosa ( inasemekana mzazi wa Mtoto haelewani na Mtendaji huyo hivyo amelitumia hili ili kupata Public sympathy, Binti ana mimba lakini hajapewa na huyo jamaa). Mwezi uliopita kwenye hiyohiyo Halmashauri kuna binti alidai amebakwa na Muuguzi wa Kituo cha Afya Mamba,.. Lengo likiwa nikutaka wamalizane ili Muuguzi atoe hela alipokataa yule mama akapiga simu Polisi,. RPC akatangaza kwa Mbwembwe kuwa Muuguzi huyo amekimbilia kusiko julikana ili hali sio kweli Muuguzi hakukimbia. Baraza la Wakunga wameenda wamefanya uchunguzi na kukuta Muuguzi hakuwa na Hatia. Ni Vema tukawa makini sana na hawa Wananchi Matukio ya kuzua dhidi ya Watumishi yamekuwa mengi sana awamu hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom