Ofisa alipwa mara 10 mshahara wa JPM

Ofisa alipwa mara 10 mshahara wa JPM

Mwandishi, athibitishe kuwa Rais analipwa 9.5m/ month
 
Mshahara wa raisi ndo kima cha juu zaidi kuliko vyote au??
 
kwa huyu jamaa Wa 97mil, maana yake kila (a) Sekunde 112.26Tsh (b) 6736.11Tsh kila dk (c). saa 404,166.6Tsh (4k) (d) day 3,233,333.33Tsh (Massa ya kazi (3mil) (e) week 22,633,333.33Tsh (f) monthly 97,000,000 Tsh.
Hapo ni nje ya marupu rupu na allowance zingine kama nyumba, Gari, mafuta, Umeme
Kwa maana nyingine huyu anauwezo Wa kujenga nyumba kubwa yenye kila kitu kila mwezi,
mtu huyo pia kama hiyo 97mil atalipwa kwa noti za elf 2, basi Pesa zake zinajaa kwenye Noah, na kama atalipwa kwa noti ya elf moja basi atatakiwa zijae kwenye Coaster!!!
Wee unafikiri ndungai ni fala ripoti.ya bunge kumkabidhi rais?..anaogopa majaliwa atawajibika kama alivowajibika lowasa.inshort kila kamati itakayoundwa lazima itatikisa mawaziri maana ndo walewale mwaka juzi na mwaka wanachobadilika ni wizara tu ila aliyekoraga kwenye madini anapelekwa kwenye utalii..ndungai sio mjinga nyie.umeona kina chenge bado wapo.kwenye madini walikuwepo na kwwnye ripoti hii bado yupo na bahati mbaya mmenda kuchunguza uvuvi ambayo magufuli alaishwahi kuwa waziri huko hahahaha nacheka lakini yajayo yanasikitisha.huenda kamati imebaini uwozo wa magufuli ikashauri ripoti apewe yeye mazima.
 
Ni mshahara wa around USD 500,000 kwa mwaka ambao unaendana na kiwango ambacho top managers wa multinationals hulipwa.
 
Kamati Maalum ya Uchaguzi wa gesi iliyoundwa na Spika Job Ndugai, mwishoni mwa mwaka jana, imewasilisha ripoti yake jana na katika mambo iliyobaini ni mmoja wa watumishi wa Kampuni ya PanAfrican Energy kulipwa mshahara wa sh.. Milioni 96, ambao ni mara 10 ya mshahara wa Rais John Magufuli ambao ni sh. milioni 9.5 kwa mwezi.


Kwani kuna tatizo gani akilipwa zaidi ya Rais? Mbona kuna watu wengi tu wanalipwa mishahara mikubwa zaidi ya Rais? Au Rais ndiyo anatakiwa kulipwa zaidi ya watu wote?? Lakini hoja nyingine muhimu ni mwamba Rais anahudumiwa kila kitu na Serikali nje ya mshahara wake, kwahiyo ukipiga hesabu unaweza kuta malipo kwa Rais ni makubwa zaidi ya hiyo mil96
 
Kwani shida iko wp? acheni ale tu! mbona waliopiga 1.5 tri hawasemwi? mbona waliopiga escrow, epa, na mengineyo wanadunda tu..kila mtu ajilie kwa kadri anavyoweza maana imeshakuwa tabia ya nchi yetu!
Kunywa na kula chochote bill nalipa,hata kitimoto kula bill ije kwangu!
Hata dada poa chukua bill ije kwangu
Hata chumba bill nalipa mm!
Jiachie tu mkuu!
 
Kamati Maalum ya Uchaguzi wa gesi iliyoundwa na Spika Job Ndugai, mwishoni mwa mwaka jana, imewasilisha ripoti yake jana na katika mambo iliyobaini ni mmoja wa watumishi wa Kampuni ya PanAfrican Energy kulipwa mshahara wa sh.. Milioni 96, ambao ni mara 10 ya mshahara wa Rais John Magufuli ambao ni sh. milioni 9.5 kwa mwezi.

Chanzo: NIPASHE
Pan African Energy sio kampuni ya serikali, ni wawekezaji.
CCM umasikini unewajaa, mnataka watu wote wawe China mbaya kama nyie
 
Yaani Watanzania tushaonekana wajingawajinga kwahiyo wanatuletea sinema kila siku kusogeza siku mbele huku wanaendelea kutupiga.

Yaani kuwaongoza Watanzania rahisi sana.
Hasa ukiweza kuchunga ng'ombe
 
Pan African Energy sio kampuni ya serikali, ni wawekezaji.
CCM umasikini unewajaa, mnataka watu wote wawe China mbaya kama nyie
Ndo maana wanaangaika na MTU kumiliki vigari vidogo 19 ambavo havifikii hata thamani ya v8 ya bashite.
 
Back
Top Bottom